"Mume wa mtu mtamu bana" ...

Eiyer

JF-Expert Member
Apr 17, 2011
28,268
2,000
Binadamu ana vijambo sana

Ni mara nyingi sana nimekuwa nikiwasikia vijana wakilalamika kuwa mabinti siku hizi hawawataki vijana na wamekuwa wakitoka na watu wazima au kama ni kijana basi wanahakikisha kuwa kijana huyo ana mke

Nimewahi kufanya mazungumzo na vijana wengi tu na malalamiko haya mara nyingi hutolewa na vijana ambao hawajaoa,hili kidogo lilinistaajabisha na kujiuliza sana maswali kadhaa

Nikasema inamaana sisi ambao hatujaoa "hatuuziki" tena kwa akina dada hadi tuoe?

Sikuamini hadi nilipofanya ka utafiti kadogo kwa wadada kadhaa

Majibu niliyoyapata kutoka kwa hawa wadada yalinistua sana,kati ya mabinti niliowauliza kuhusiana na hili mmoja tu ndio alikana kutoka na wanaume ambao wapo kwenye ndoa na wengine wote walikubali na kunipa sababu kadhaa

Kati ya sababu ambazo walinipa ni kuwa eti mume wa mtu anajua kutunza na anajua thamani ya mwanamke na matumizi,walidai kuwa vijana ambao hawajaoa wanakuwa na mambo mengi sana kama vile kujiimarisha kiuchumi na malego ya kuwa na familia hivyo mambo hayo husababisha wawe bahili sana

Nilikuna kichwa ilipofikia hapo kwani niliona kama wananisema hivi ....

Wakaendelea kudai kuwa waliooa wenyewe wamechoshwa na wake zao na wanatafuta pumziko na mara nyingi wanakuwa wanajua mahitaji ya mwanamke kwasababu wanae nyumbani

Kwa kifupi waliongea mengi sana na kufikia kuniambia Eiyer,"mume wa mtu mtamu sana nyie mabachela mtasubiri sanaaaa"

Kwa ufupi akina dada ndio wamekuwa na aina hii ya kuyatazama maisha siku hizi

Kaazi kweli kweli ndugu zangu .....!!
 
Daudi1

JF-Expert Member
Dec 14, 2013
6,815
2,000
Na hapo ndo utajua kuwa mfumo wa mke mmoja hata wanawake wenyewe hawautaki wanataka kuwa wawili au watatu kwa mwanaume mmoja,kama mwanamke unajua kuwa huyu mwanaume ana mke bado unasema mtamu huoni huo utamu ameupata kwa mwanamke mwenzio? maana mwanaume huyo huyo kabla hajaoa si mtamu na akishaoa ni mtamu

Halafu wanaponishangaza ni hapa ameshajua una mke maana yake yeye ameridhia kuwa wa pembeni sasa kitendo cha kulazimisha kuwa na wewe muda wote wakati anajua unafamilia ni sawa na kulazimisha ucheze dk 90 wakat umewekwa kama reserve
 
NAPITA

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
5,076
2,000
Yawezekana maana hata kuna baadhi yetu sisi wanaume tunasema mke wa mtu mtamu ila samahani sana tena sana kwa jamaa niliepita na mke wake masikini huwa naumia sana kwa kitendo hicho nilichofanya kabla na mimi sijawa na mke nashukuru jamaa akujua mpaka leo salam kwako uko Zanzibar.
 
Mkuu umenimaliza aisee!!
 
Ebanaeee!
 
Ennie

JF-Expert Member
Jan 15, 2011
7,140
2,000
Na wewe kazi unayo,uko busy kweli kutafiti mahusiano ...........lol
Kwa matokeo haya ya utafiti huu basi nyie single mkitongoza mseme mmeoa ili kujiongezea points!!!!
 
NAPITA

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
5,076
2,000
Ebanaeee!

Vp mkuu usishangae sana haikuwa dhamila yangu ila Yeye ndo alitaka iwe ivyo baada ya kuwa na Matatizo kwenye ndoa Yake akaitaji pumziko la roho yake ili apunguze stress.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom