Mume wa mtu ananitesa

Wapo wanawake wazuri wenye tabia njema na wanaojitambua sio kama huyu mwanampotevu

Duh
Wanaojitambua wakoje?
Huyo yupo katika kipindi cha mpito.. akionja nje atatulia. Hakufaidi ya gf na bf na kuwachanganya kabla ya kuolewa.
 
Wee ni zero brain kumbe, no more comments

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe na mke wa mtu na yeye ni mume wa mtu, tulia kwa mumeo kama alivyokushauri wewe na muache atulie kwa mkewe.
Kama ungekuwa hujaolewa tungekushauri uolewe mke wa pili kama misingi yenu inaruhusu mambo ya uke wenza.
Jaribu kuepuka mawasiliano na yeye yasiyokuwa na maana. Kinyume chake unachokitafuta utakipata(fedheha)

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acheni kumtaja taja Mungu kwenye ishu kama hizi!! eti namuogopa Mungu na wakati huo huo unataka kusaliti ndoa yako..!! Jina la Mungu ni Holy/tukufu sasa unapolitaja akati unataka kuchepuka na mnatumiana picha za uchi nashindwa kukuelewa!!
 
Wewe wala huna pepo wala nini ni katabia tu ambako kalikuwa introduced sasa kamekuwa ni mazoea sasa ndo yanakutesa, katika jamii yetu ya kimahusiano kitu kinachoitwa chatting ni kibaya sana sana yaani kinapenya mpka uvunguni mwa moyo, mahusiano yanajengwa sana kwa asilimia kubwa na mawasiliano, na hasa sisi wanawake ugonjwa wetu upo hapo kwenye mawasiliano,the more mtu anavyokuweka karibu sana unajikuta unampenda unampenda mpka basi,unapigwa upofu haswaa mpka yule aliyekaribu nawe unamuona si lolote na utaanza kuona madhaifu yake kama wewe hapo ushaanza kuona kama hulizishwi,Mara kama mrefu utamuona mrefu sana,kama mfupi utamuona mfupi Sana yaani utatafuta vitu kibao vya kukupa uhalali wa wewe utoke nje. Dhambi huanza mawazoni kama tamaa,kisha wazo lile ukiendelea kulilisha linakupa nguvu ya kusema,nguvu ya kuongea inaenda kuzaa tendo.

Huyo jamaa kiukweli humpendi kabisa basi tu mawasiliano yamekufanya udate na inavyoonekana jamaa ana maneno matamu kama asali,mpaka hapa ulipofika uko kwenye mstari wa 0.9999 Kuanguka,so unanafasi ya 0.1 tu kujiokoa, kama kweli jamaa kakushauri hivyo ujue amesoma kitu kwako kashindwa kukuambia ukweli wako kwamba hufai akaona tu akwambie kwa uzuri stick na mume wako.

Cha kufanya kama kweli unataka kujiokoa na una hofu ya Mungu kweli na unampenda Mume wako kidhati na unajipenda mwenyewe na unawapenda watoto wako,fanya yafuatayo block jamaa huyo katika njia zote mnazowasiliana,Utateseka wiki moja tu baada ya hapo utakaa sawa. ule muda uliokuwa unatumia kuchat na huyo jamaa utumie kuchat na mumeo na Ibada,yale maneno matamu uliyokuwa unamwambia jamaa yako mwambie Mume wako na Mungu wako. kama mume mzito kujibu mwambie tu vile unavyojiskia ukiwa unachat naye. Jikite zaidi kwenye ibada na ujipe ubize haswaaa jitahidi usiwe idle,kila wakati uwe na jambo la kukupa ubize,tumia muda wako zaidi na Mungu na familia yako na kazi zako, mwili usipoupa kazi wenyewe utakupa kazi,wazo chafu likiingia akilini mwako la kumkumbuka jamaa crash hilo wazo haraka Sana waza vitu vingine,anza kuliona hilo lijamaa libayaaaa likosoe uwezavyo,lina mke,limekutumia dudu fake,yaani tafuta yote mabaya vile utakavyoilisha akili yako juu yake ndivyo itakuwa ni wiki 2 tu utakuwa sawa hadi utajiona jinsi gani ulivyokuwa mjinga ukataka kujiangamiza. Mwisho jikite kwenye ibada kama wewe ni Mkristo soma zaidi Biblia,nenda kanisani,kaa na wanao wape story za Biblia na fanya nao ibada na ufatilie mambo yao ya shule,nenda kafanye huduma kanisani,toka out na mumeo si unafanya kazi bana siku moja msuprize,tafuta marafiki wapya wazuri wakukujenga kiroho, Hayo mawazo machafu yote yanayokunyemelea utayashinda. Kila la heri.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Fata ushauri wa muheza aliokupa dada. Usiwe kama mwanamke mpumbavu wa kubomoa nyumba yako kwa mikono yako mwenyewe

Umebahatika kua na ndoa yenye amani basi linda amani hiyo kwa gharama yoyote mana ikipotea ni ngumu kuirudisha

Umesema una hofu ya Mungu basi behave kama mwenye hofu ya Mungu kweli,usiruhusu tamaa/hisia negative kuharibu amani mliyonayo kwenye ndoa yako....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…