Mume mwenza simuelewi ananitafutia jela

Mume mwenza simuelewi ananitafutia jela

Wewe kweli kubwa jinga!sasa mpaka sasa haujui nin kinaendelea apo?unamegewa!kinachokufanya ukashindwa kumface na kumpiga marufuku kuja home kwako ni nini?embu tumia busara na hekima...suala hili ni dogo sana.
sasa nipe ushauli ni fanye nini mimi bado sijagundua kitu nipo kwenye wasi wasi tu
 
Yani mimi siku ameleta mguu wake hiyo asubuhi, ningemfurumushia huko mfyuuu zake

Unaibiwa hapo, live bila chenga na wameanza muda. .
 
Hakuna mwanaume aso koloni lake, Hilo koloni lake anapanga jinsi ya kulitumia atakavyo
 
Hakuna Awali mbovuu ndugu!!!
Baba John kakuzidi maarifa, pole yako..
Kitendo cha wewe kumwacha na mkeo eti unawahi mihangaiko ni ubashite tosha. Yaani umwache mkeo na mwanaume ndani???
 
Uvumilivu wako hata shetani anauogopaa aisee ukisikia mume bwege ndo ww inshort umeshaibiwa saana tena hapo hapo Kwenye kitanda chako dm
mkuu mbona mimi mwenyewe najitambua sio bwege wewe nipe ushauli nifanyaje niache mke au nimpige stop baba jonh
 
Duh! Ukiona manyoya ujuwe.......STUKA Mkuu STUKA tena sana.

Habari wadau
Naanza kuandika kisa hiki kwa maskitiko makubwa
Mwenzenu nina mke nimebahatika kuzaa nae mtoto mmoja lakini mke huyu wakati huo naanza nae mahusiano yetu nilimkuta na mtoto mmoja wa umri wa miaka 5

Kama mjuavyo nilivutiwa na bibie na sikuona uzito wa kumlea mtoto nilifurahi kujua huyu mke ni mlezi na waswahili wanasema ukipenda boga penda na ua lake

Mwezi uliokwisha aliibuka bwana mmoja asubuhi kabla ya mimi sijakwenda kwenye shughuli zangu akakaribishwa mimi nikatoka ukumbini nikamkuta huyu bwana amekaa na watoto wote wawili kwenye kochi, nikamuuliza mama watoto akanijibu nilikuwa nasubiri nikufahamishe huyu ni (baba john) si jina rasmi,nikamsalimia tukaletewa chai tukajumuika pamoja kunywa chai na maandazi tukaongea kuhusu maisha kidogo na akanieleza dhumuni la kufika hapa ni kumuangalia mwanawe ,siku zimekuwa nyingi nikawaacha mimi nikaondoka kuelekea kwenye mizunguuko yangu

Swali linalonisumbua kichwa huyu bwana alipajuaje hapa nyumbani na kwanini alikuja asubuhi hana shughuli huyu mtu, na pia hivi sasa nasikia mimi nikitoka na yeye anafika mara mbili kwa siku kuangalia mtoto na akifika anaacha mizigo anaondoka sasa juzi ndio ilikuwa kali nilikuta chupa za bia nikaambiwa nililetewa na mume mwenzangu na yeye ameshakunywa zake nikamuuliza mke akanijibu nisiwe na wasiwasi yule anampitia mwanawe na yeye ni mtu mzima hawezi kutuchanganya,lakini jamani mtu na mtuwe ni kama gari na mteremko

Ok kwa sababu ya likizo ya viroba nikajinoma bia lakini kwa shingo upande na kengele ya tahadhari ikinililia kichwani
Leo hii asubuhi mke ananiaga kuwa kuna shughuli sijui inaitwa kitchen mada kama nimekosea mta sahihisha ya mdogo wake baba john nikamkubalia lakini kwa shingo upande anasema kulingana na ratiba za shughuli atarudi kesho

Jamani mpaka kufikia hapa mimi naona mume mwenzangu ananizunguka mbuyu na sitaki afike hapa kwangu naweza kuua na nikapelekwa jela

Wadau naomba mchango wenu niache mke lakini bado nampenda au amchukue mtoto wake lakini john mwenyewe bado mdogo ili anipe amani ,nitaua mimi

assanteni nasubiri ushauri wenu
 
Utachapiwa hivi punde unatakiwa uwe mkali ikiwezekana mpige biti bana John awe anakuja weekend tu tena sio kila siku kama vipi amchukue mwanae

Kumbe ndio mana wanaume hawataki kuoa single mothers

Mkuu kwa nini umetumia jina la John?
 
Penzi halichachi kwakweli.....limerudi kwa kasi ya 4G
 
Hakuna Awali mbovuu ndugu!!!
Baba John kakuzidi maarifa, pole yako..
Kitendo cha wewe kumwacha na mkeo eti unawahi mihangaiko ni ubashite tosha. Yaani umwache mkeo na mwanaume ndani???
mkuu sakayo nilijua ile ziara yake ya siku moja tu.
 
Utachapiwa hivi punde unatakiwa uwe mkali ikiwezekana mpige biti bana John awe anakuja weekend tu tena sio kila siku kama vipi amchukue mwanae

Kumbe ndio mana wanaume hawataki kuoa single mothers

Mkuu kwa nini umetumia jina la John?
kwa mimi naona kama tayali washafanya aya mambo
 
Back
Top Bottom