ladyfurahia
JF-Expert Member
- May 10, 2011
- 14,758
- 9,592
- Thread starter
-
- #41
Swali lako ni gumu na "complex" kidogo kwa sababu kwa maoni yangu lina-cover sio tu psychology lakini hata spiritual matters.Majibu yangu ntayagawa katika maeneo ya kiroho na ya kisaikologia kama ifuatavyo:
1;SIFA UNAZO?:Ili kumpata mume/mchumba mwema....jiulize "wewe ni mwema?' na unadhani mume mwema ana vigezo gani?wewe unavyo?Kwa sababu utaidanganya nafsi yako bure kama umeweka viwango ambavyo hata wewe huna!Kumbuka ndege waliofanana huruka pamoja.
2;UMRI:Mwanaume kijana mwenye umri kati ya miaka 32-35 mpaka 40 ni mwenye uzoefu na mambo mengi na anaweza kuhimili misukosuko ya ndoa na maisha.Kwa lugha nyingine huu ni umri ambao mwanaume anajua vipaumbele vyake na nini anatakiwa afanye na ni kwa wakati gani!Huu ni wakati ambao hata kama alikuwa ni mwenda disco sana basi anweza kupunguza na kuacha kabisa na kuwa tayari katika maisha ya ndoa...tofauti kabisa na kijana wa miaka 25,28 nk.
3;ELIMU:Dunia imebadilika na ina changamoto nyingi sana.Ni muhimu kwa mume unayemtaka awe na elimu angalau ya advance diploma/bachelor degree.Hili litasaidia sii katika changamoto za kifedha hata katika malezi ya watoto na mahusiano yenu.Lakini elimu pia inasaidia hata uelewa wa mambo complex kama ya kiimani na kupunguza uhafidhina(unoko usio wa lazima).
4;NGUVU YA MAOMBI:Prayers are very powerful tools.Funga na kusali kwa imani utafanikiwa tu.Biblia ilishasema "Mke mwema hutoka kwa bwana"LIKEWISE mume mwema hutoka huko huko kwa bwana.Sio rahisi kuanza kumtafuta tu mume/mke mwema...na ukampata ni vizuri kumtanguliza Mungu ktk hili.
ukitaka mume mwema acha kufanya uchumba wa surprise, mi nilichumbia mke wangu au niseme tulikua marafiki kwa zaidi ya miaka saba, we enjoy it now ( sisemi kuwa hakuna ups and downs zipo)
Hebu fafanua zaidi tunatumikaje siye dadavua nielewe maana umeweka kiudadisi
Nimeipendaje hii comment yako kweli imenifanya nijue kuwa kuwa kunawatu wanaowatakia wenzao yaliyo mema sana nimefurahishwa sana na mawazo yako mazuri uliyonipa hapa , na vilevile umenielewesha vyema na nami nimekuelewa sana yaani sina cha kuongea hapa asante sana NA Mungu akubariki
Mkuu naona una hamu sana na hayo maandiko, ngoja nijaribu kupekua pekua bible kama nitafanikiwa nitakujuvya! lakini simply ni kwamba kama ilivyoandika kwa mwanaume,basi the vice versa is also true kwa mwanamke :smiling:yaani hapo sasa umenena mwana nashukuru kwa kunimaanishisha na kunielewesha ila bado hujaingia sana katika vifungu vya neno la Mungu kwanini hakuna kifungu ambacho kinaelezea KUMPATA MUME MWEMA vingi vinasema kumpata mke mwema why? nidadavulie kidogo best
kwa maombi tu mwanzo mwisho.
ivi unakutana wapi na mume mwema?
Ndiye mimi sema ukaniacha!!!
Hahahahahaha............. Mme mwema hafumaniwi banaKwa kufanya ngono utamjua tu.
Lyagwa nimeona wito nami sina budi kuitika wito wako. Jinsi ya kumpata mume mwema . Kama mtoa mada alivyoainisha vifungu vya neno la Mungu na kutoa kidogo mashaka yake juu ya kwanini mwananmke hakupewa muongozo wa kumpata mwanaume mwema. Ni kweli ukiangalia kwa haraka unaweza kusema hivyo lkn tukirudi nyuma na kuangalia mazingira ya uandishi yalitumia utamaduni upi tunaweza kuelewa lkn hapa si mahala pake ngoja nirudi kwenye swali la msingi. Binafsi nilipokua naomba mume mwema nilitumia andiko la ombeni jambo lolote kwa jina langu nami nitafanya au njooni tusemezane eleza mambo yako ili upate kupewa haki yako n.k. Kwa kweli nilienda mbele ya uso wa bwana kwa ujasili mwingi na kumuomba Mungu mwanaume niliekua namuhitaji kwa kifupi nilielezea nataka mwanaume wa jinsi gani hasa nilipojifahamu tabia yangu. Mara nyingi huwa tunaenda mbele za Bwana kuomba tukiwa tayari na mtu yaani tunataka Bwana atoe kibali tu kwani tulisha chagua au tunamuomba mungu atupe mume wa kufanana nae. Sasa hii kusema wa kufanana nae ipo general mno . Ni vizuri kua specific let's say umeomba mume ukapewa mcha Mungu lkn akawa na tabia ambazo wewe hazikufurahishi kama vile labda yeye muda wote yupo kwenye huduma na wakati wote ana watu hana muda na wewe au labda muongeaji sana. Sasa ni vizuri kumueleza bwana ukiwa tayari na vision ya mume unaemtaka . wakwangu nilikua tayari ninae moyoni ie picha ya mume wa aina gani nilikua tayari ninayo. Kwa hiyo basi ucha Mungu ni kitu cha lazima kuanza nacho lkn pia uende mbele zaidi na kumuomba Mungu mume unaemtaka nafsini mwako. Mume mwema anapatikana kwa Bwana piga magoti omba na Bwana atakupa umpendae.Naamini mume atokae kwa Bwana utampenda na yeye atakupenda na kukuheshimu.Kama nilivyoeleza mimi Bwana alinipa niliekua namtaka na sasa nina miaka 14 ya ndoa na miaka 2 ya uchumba so naweza kusema tupo pamoja kwa 16 yrs. Na muda huu wote tumeishi ktk amani na furaha isiyoelezeka na tunampenda Mungu. Nakumbuka kuna mtumishi flani aliwahi kusema andika sifa ktk karatasi yako za mume/mke unaemtaka pengine list hiyo itakua na 10 points eg mrefu, mpole, msomi wa degree, mweusi,n.k sasa hii list unaenda nayo mbele za bwana na pia itakusaidia kupata picha ya mume/mke unaemtaka.
^^
Lyagwa
Asante kwa kuniita awali niliona list ndefu ya lady furahia nikaona niwape nafasi kwanza watajwa.
Back to the topic.
..
Bado naamini Mungu ndiye awezae kumpa mtu Mume mwema na siamini kuwa maandiko yamemtenga mwanamke Maana wote wamepewa nafasi ya kumuomba kwa nidhamu-atampa.
..
Tatizo linakuja kuwa Mtu anapata mchumba,,akishapata then ndipo anaenda kwa Mungu kuomba ila moyoni tayari ana choice yake ambayo ameamua.Ongeza tena yale mafunuo Oo! Nimeonyeshwa ni huyu! Oo! Ni yeye tu-Lakini Mungu anatazama tu.
Those who let choices in hands of God (to choose for them) will never go empty.
^^
Habarini bandugu marafiki zangu wote na wasio marafiki pia.
Naingia kwa ujio kama alivyokuja Raisi Obama kimkuku kuku na wakiana kwa leo wapendwa wangu
marafiki zangu ninaingia kiimani zaidi na ni vyema muelewe nilichoamua kukizungumzia hapa na sio
kufakamia bila hata kuelewa topic hii yasemaje: Kabla sijaenda mbele zaidi tazama picha hii hapa:
View attachment 100908 na hii View attachment 100909 hapa tena View attachment 100910 mwisho View attachment 100911
Kila mmoja wetu anajua kua Maandiko matakatifu yanavyosema sana jinsi ya kupata Mke kuliko Mume na maandiko maarufu ni kama-Mithali18:22-Apataye mke apata kitu chema; Naye ajipatia kibali kwa Bwana na Mithali.31:10-Mke mwema( Kiswahili imetumia neno moja tu .Mwema lakini Kiingerea ktk Bible mbalimbali imetumia maneno mengi yenye nguvu ya ajabu na kushangaza kujua kumbe Mwanamke mtarajiwa kuwa Mke ni kitu kizuri na cha ajabu sana hasa aliyetoka kwa Bwana. Maneno yaliyotumika ni kama. wife of noble character, capable, intelligent virtuous woman, a competent wife, worthy woman), ni nani awezaye kumwona? Maana kima chake chapita kima cha marijani. Tena Biblia ya King James na New King James ndizo zimetumia neno Virtuous woman ( notice: Ni woman!) na maana ya neno Virtuous ni good, moral, ethical, upright, honourable, excellent, pure, worthy, honest, righteous, exemplary, squeaky clean, blameless, praiseworthy, incorruptible, high-principled), pia Mwanzo.24:1-67.
Katika Agano Jipya, tunakutana na neno kuchumbia au Mchumba wazi wazi ktk Luka.2:5 ingawa hatuambiwi Joseph (yusufu) alimpataje mdada Mary (Maria mama wa Yesu) Kwakua ni ivyo kwamba Bible imeongelea sana kuchumbia au Mchumba wazi wazi ktk Luka.2:5 ingawa hatuambiwi Joseph alimpataje mdada Mary. Kwakuwa ni ivyo kwamba Bible imeongelea sana kupata Mke mwema ambaye anapatikana tu kwa Bwana, mchumba bora je? anayepelekea mke mwema, tunampataje? kwa kizazi chetu cha leo cha DOT .COM ambapo hatuchanguliwi Wachumba/Wake zetu na wapendwa marafiki zetu, Viongozi wa Kanisa. Maparoko au Wazazi kama zamani, tunafanyaje kuwa salama?
Tutafanyaje kumpata mchumba mwema (mume) kwa kizazi hichi jamani na je kwanini haya maneno hayakuandikwa kwenye Bible? kwani sisi madada tunachanganyikiwa nami pia yameniconfuse mwenzenu kabisa wala sijaelewa, kwani Mume (Mwanaume) mwema hapatikani kwa Bwana? au ni versa vesa tu hapa.ambayo imewekwa, kwani hakuna wanaume wema wa kuolewa nao.? Ndo mana nimependa niwashirikishe jambo hili la kiimani tuchambue kidogo. kwani huwa nikisoma vifungu hivi vinanitatiza sana. Nakuwa sielewi kabisa my frendo. HAKUNA MWANAUME MWEMA TOKA KWA MUNGU?
Karibuni mabestito kwa uchambuzi zaidi hapa.
cc: Nicas Mtei, Ruttashobolwa, Erickb52, Mr. Rocky, Arushaone, Mtambuzi, Mamndenyi, lara 1,
stevoh, jouneGwalu, Kipaji Halisi, Jiwe Linaloishi, Filipo, Liverpool, Passion Lady, charminglady, Paloma, Mentor, Heaven on earth, everln salt, gfsonwin, Lady doctor, Asprin, Madame B, Lucas, @Rular Swaga, Lyagwa, Ben Saanane, mimisa, na marafiki zangu wote jongeeni
Mkuu ilibidi nitumie ushuhuda wakati mwingine ni ngumu kutumia theory. Nashukuru sana kama kuna watakaojifunza kupitia ushuhuda wangu . ubarikiwe sanaKwanza kabasa nafurahi na kukushukuru kwa kuitika wito na pia kuelezea mtazamo na pia kwa kutoa ushuhuda mzuri wa jinsi ghani wewe binafsi uliweza kupata mume mwema kwa mtizamo na matamanio yako, hakika inapendeza, na wala sikutegemea ungekwenda mbali hivyo hadi kutoa ushuhuda, hii inaonesha ni jinsi ghani ulivyoguswa na mada ya dada yangu ndg ladyfurahia. Nasema shukrani once again for your positive response.
Nje ya maada nichukue furasa hii kukupongeza binafsi kwa safari yako ya maisha, ulipofikia kila mtu mwenye mapenzi ya dhati na huu wito angependa kufika huko na zaidi, sisi tumo lakini hata nusu huenda hatujagusa, lakini tunamshukuru Mungu na kuzidi kumuomba yeye pekee maana kupitia yeye alituwezesha kuwa hivi tulivyo katika umoja wetu. Kila la kheri sana dada Ablessed na ubarikiwe sana.
Superlike...umpendae akupendi al that way...unaweza dhani ndo mwema huyo...kumbe ufikiliavyo wewe ni tofauti na Mungu akuchukuliavyoKwa ujumla vijana wa kike na kiume wana wakati mgumu sana wakati wa kumpata mwenzi wa maisha. Inakua rahisi kwa mwanaume cse yy ndo mfanya maamuzi japo nao wana wakati mgumu cse mapenzi ni. Vise versa : vile unavyo mpenda mwenzako sivyo atakavyo kupenda.
Kikubwa ni kumuomba Mungu tukiamini mume na mke mwema anatoka kwa Lkn tunapaswa kua na subira ktk kusubiri majibu. Usilazimishe tamaa zako kua majibu.