Mume anasa mimba ya ajabu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mume anasa mimba ya ajabu

Discussion in 'Jamii Photos' started by MziziMkavu, Aug 10, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Aug 10, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  [​IMG]UNAAMINI katika miujiza? Kilombero, Morogoro kuna mtikisiko mkubwa kufuatia habari kwamba kuna mwanaume aliyenasa mimba ya ajabu.

  Mwanaume ana mimba! Habari zinadai kuwa Said Mohamed Kapita, 40, ametundikwa mimba kishirikina, ikiwa ni adhabu baada ya kile kinachodaiwa ni kumpa ujauzito mwanafunzi (jina kapuni).

  Inadaiwa kuwa Kapita ambaye ni fundi ujenzi wa
  nyumba anayejitegemea, alimpa mimba denti, hivyo kuibua mtafaruku mkubwa kati yake na wazazi wa mwanafunzi huyo.

  MADAI YALIYOPO
  Inaelezwa kuwa hivi karibuni, Kapita akiwa amekaa kibarazani, jirani na nyumbani kwake, alifuatwa na baba mzazi wa denti huyo na kumhoji kuhusu ujauzito uliomo kwenye tumbo la bintiye.

  ...tumbo la bwana Kapita.

  Rafiki wa Kapita (jina tunalo) ambaye ni mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo alisema: “Ulitokea mvutano mkubwa. Baba wa yule mwanafunzi ni babu kabisa na siku ile aliongozana na mwanaye ambaye tumbo lake lilishachomoza. Mimba ilikuwa inaonekana wazi.

  “Mwanafunzi alimtaja Kapita kwamba ndiye mhusika wa ule ujauzito, baba naye akasisitiza ni lazima akubali kuhudumia. Kapita akakataa kata kata. Unajua haya mambo, hata kama ni kweli huwezi kukubali mimba, yule ni mwanafunzi, miaka 30 jela nani anataka?

  “Alipokataa baba mtu akawa mbogo. Mwisho akamwambia kuwa hawezi kumshtaki polisi, isipokuwa adhabu yake ni kuihamisha mimba kutoka kwenye tumbo la binti yake kwenda kwa Kapita.

  “Sisi tulidhani utani lakini baada ya siku mbili tukaona mabadiliko. Ndugu yetu akavimba tumbo kama mjamzito. Hii ikasababisha gumzo lipae, kila mtu Kilombero akapata habari kwamba ndugu yetu ni mjazito.”

  HEKAHEKA HOSPITALI YA MIKUMI
  Katikati ya wiki iliyopita, Kapita alipelekwa Hospitali ya Mikumi, lengo likiwa ni kupata tiba juu ya matatizo ya tumbo lake.
  Hata hivyo, baada ya kufika hospitali na kufanyiwa uchunguzi, tumboni hakuonekana mtoto, badala yake ilibainika kuwepo na kiasi kikubwa cha maji.  Kutokana na hali hiyo, madaktari walimnyonya maji yote ambayo yalijaa ndoo mbili lakini baada ya muda tumbo lilirudi vile vile.
  Uwepo wa Kapita hospitalini hapo, ulisababisha vurugu nzito kutoka kwa wananchi waliomiminika wakitaka kumuona ili wajue kama ameshajifungua au la!

  Zikawepo habari kuwa Kapita amejifungua mtoto kwa njia ya upasuaji, kitendo ambacho kilizidi kukusanya umati wa watu hususan wakazi wa Mikumi, waliofika hospitalini hapo kutaka kumuona.

  Kutokana na vurugu hizo ambazo zilisababisha shughuli za kutoa huduma hospitalini hapo kusimama, madaktari waliamua kumkabidhi Kapita kwa ndugu zake na kupitishiwa mlango wa nyuma kumrudisha nyumbani kwake, Kilombero.

  NENO LA DAKTARI
  Ofisa muuguzi wa hospitali hiyo, Dk. Joseph Masenga alilithibitishia gazeti hili kumpokea mgonjwa huyo lakini akafafanua kuwa uchunguzi wa kitaalamu haujabaini kuwepo kwa mtoto ndani ya tumbo lake.

  “Alilazwa hapa, alifika hapa akiwa na tumbo kubwa kama la mama mjamzito lakini baada ya kumfanyia uchunguzi tukabaini tumbo lile lilijaa maji. Tulimtoa maji mengi zaidi ya ndoo mbili.

  “Alikuwa amepungukiwa maji mwilini, tukamuongezea. Tumeambiwa kwamba ana ujauzito, eti huko kwao alikorofishana na watu ndiyo wakamfanyia mambo ya ushirikina, sisi hatuamini ushirikina, tulichoona tumboni ni maji, hatukuona kiumbe chochote,” alisema Dk. Masenga.

  USO KWA USO NA KAPITA
  Baada ya kutoka Mikumi, Uwazi lilivuka mitaa, likapanda milima na kuteremka kwenye mabonde hadi Kilombero, ndani kabisa katika Kijiji cha Kidogi, lilikoelekezwa ndiyo anakoishi Kapita.

  [​IMG]

  Hata hivyo, baada ya kufika nyumbani kwake, lilielezwa amepelekwa kwa mganga wa tiba za asili anayeitwa Lungu.
  Uwazi lilimkuta Kapita kwa Dk. Lungu na baada ya utambulisho alisema: “Bora umekuja wewe mwandishi, nimezushiwa eti nimejifungua mtoto wa kike. Kuna watu hawanitakii mema na nawajua, hao ndiyo wanatangaza.”

  KUHUSU KUMPA MIMBA DENTI
  Kapita alisema: “Ni kweli nilifuatwa na mzee mmoja akiwa na binti yake mjamzito, wakasema mimi ndiye mhusika. Nafikiri lengo lao ni kunitafutia kesi, kwa maana mimi sihusiki kabisa.

  “Nilipokataa, yule mzee akaniambia atahamishia ujauzito wa mwanaye kwangu. Hayo mambo siamini. Nachoamini mimi ni kwamba sina mimba na huyo mwanafunzi sihusiki naye kabisa. Mimi nina mke wangu na watoto, najiheshimu. Wanafunzi wa nini?
  “Nimeshafuatwa mpaka na walokole, wananiambia waniombee nipone eti nina mimba, hiyo si kweli.”

  DOKTA LUNGU
  Kwa upande wa Dk. Lungu, alisema kuwa Kapita ametupiwa vitu vya kishirikina ambavyo vimemfanya ajae maji tumboni.

  HII NI AJABU!
  MOSI: Kwa nini imetokea baada ya kuambiwa atahamishiwa mimba ya mwanafunzi?

  PILI: Kama ni mimba iweje vipimo vya hospitali visioneshe?
  TATU: Ikiwa siyo mimba ni maji, mbona tumbo limezidi kukua hata baada ya kunyonywa? (Uwazi lilimshuhudia akiwa na tumbo kubwa hata baada ya kufyonzwa maji Hospitali ya Mikumi.”

  Kapita akiwa nje ya nyumba ya mganga akisubiri zamu yake kupata tiba. Kulia ni kaka yake aliyejitambulisha kwa jina la Abdallah Kapita.

  NNE: Watu wakaacha shughuli zao na kujaa hospitali, eti mwanaume amejifungua.
  TANO: Majibu ya kitaalamu kuhusu matatizo ya Kapita hayajelezwa, zaidi ya kusemwa kwamba tumbo limejaa maji.

  KUTOKA UWAZI
  Gazeti hili limesikia mengi, wapo watu walioshauri Kapita aende kwa mzee aliyemuahidi atamhamishia mimba ya binti yake ili kulipa kisasi. Pamoja na yote, tunaamini zaidi katika Mungu.

  Tunamshauri Kapita ajikite zaidi hospitali kwa maana ndiko kwenye ufumbuzi wa matatizo yake ya tumbo. Kwenda kwa waganga wa kienyeji, wengine ni matapeli na wanaweza kuchuma fedha, huku wakimuacha na maradhi yake. Hospitali na kumuomba Mungu ndiyo suluhu. Tunampa pole kwa matatizo. Kweli hujafa, hujaumbika.

  Wiki ijayo, Uwazi litakuja na ripoti kuhusu binti ambaye inasemekana amepewa mimba na Kapita pamoja na baba yake aliyeahidi kuhamisha ujauzito wa binti yake kwenda kwa fundi ujenzi huyo. Yote yataanikwa.
  juma: MUME ANASA MIMBA YA AJABU
   
 2. Father of All

  Father of All JF-Expert Member

  #2
  Aug 10, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 3,093
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Kama ni kweli basi amevuna alichopanda. Amepanda mimba amevuna mimba. Laiti hii sayansi ingekuwa inapatikana kirahisi vijogoo wote wanaoharibu watoto wa shule walipaswa kutiwa mimba tena zenye kuchukua miaka mitano kuzaliwa ili watie adabu. Nchi yetu imegeuka ya kiharibifu ambapo jitu zima linaparamia kitoto cha shule eti kwa vile lina pesa litahonga na kitoto kuharibikiwa maisha. Ningekuwa na uwezo ningemshauri aliyemtundika hii mimba aiche hadi afe nayo kudadeki. Pia hata mzee wa matusi wa CCM Lushinde ningeshauri atundikwe mimba hata mafisadi wote na kiranja wao ambaye kila mtu anamjua.
   
 3. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #3
  Aug 10, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,591
  Likes Received: 797
  Trophy Points: 280
  Labda itakuwa fundisho kwa waharibifu wengine.
   
 4. UncleUber

  UncleUber JF-Expert Member

  #4
  Aug 10, 2012
  Joined: Apr 25, 2011
  Messages: 4,943
  Likes Received: 99
  Trophy Points: 145
  huyu mgonjwa tu nyie mnasema kahamishiwa mimba.....mbona ulaya sisikiagi mambo kama haya na wakati wao ndo wachawi balaa wangeshajaribu hata mara moja
   
 5. k

  kisukari JF-Expert Member

  #5
  Aug 10, 2012
  Joined: Jul 16, 2010
  Messages: 3,754
  Likes Received: 1,042
  Trophy Points: 280
  mbona kama ana kwasha koo?
   
 6. piper

  piper JF-Expert Member

  #6
  Aug 10, 2012
  Joined: Jan 17, 2012
  Messages: 3,260
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Mmmmmmmhh!!!!!!!!!!! kweli hujafa hujaumbika
   
 7. MATESLAA

  MATESLAA JF-Expert Member

  #7
  Aug 10, 2012
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 1,252
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Aiseeee baba yangu sijawai kuona mwanaume kanasa mimba labda itakuwa kwashako ou kiliba tumbo
   
 8. kanga

  kanga JF-Expert Member

  #8
  Aug 10, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 1,011
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Huyo mzee apewe kazi ya ajira na serikali kupunguza vidume vinavyowapa madent mimba
   
 9. ummu kulthum

  ummu kulthum JF-Expert Member

  #9
  Aug 10, 2012
  Joined: Feb 6, 2012
  Messages: 2,791
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  akome kabisaa yaan kibabu af kwa dent
   
Loading...