AT least kwa hapa TZ, hususani ukanda wa pwani, wanawake ni watu wanaopenda sana mipasho na maongezi ya mafumbo!!! Bila shaka ni wahitimu wazuri wa baadhi ya tanzu za fasihi simulizi. Last week, nilimtembelea rafiki yangu mmoja ambae mwenzangu ameoa (mie bado hivyo natoa offer kwa mwana-jf single wa kike apendae kuwa na mume!).
Ile kuingia tu sebuleni, nikakutana na kibao kilichoandikwa "UKIJA UJE NA YAKO, UMBEYA NYUMBANI KWAKO!" Kwa bahati shemeji yangu (mke wa mshikaji) alikuwa hayupo kwa muda huo hivyo tukapata nafasi ya kutosha kujadili masuala ya kimaisha. Baada ya mimi kuona kibao hicho, nikamuuliza mshikaji kwanini ameweka hicho kibao.
Akajibu, aliyeweka si yeye bali ni mke wake! Nikamuuliza kawalenga akina nani; akajibu "sijui yeye mwenyewe!" Baada ya majadiliano ya hapa na pale, nikamshauri akiondoe kibao hicho kwani anafanya embrassement kwa wageni wake! Jamaa akadai kwa kuwa alikuwa ni mke wake basi asingeweza kukiondoa yeye mke wake na yeye ana haki na hiyo nyumba!
Kimsingi, nilishindwa kabisa kumshawishi kukiondoa kibao hicho! Na kama ningekuwa nina mazoea ya kwenda kwenda pale nyumbani au kukutana na huyu rafiki yangu basi bila shaka ningejisikia vibaya sana kuhusu ujumbe ule! Sasa swali ninalojiuliza na kuwauliza wadau, je; ni muhimu kuwa na vibao vyenye ujumbe wa aina hii kwenye nyumba zetu?
Hivi hatuoni tunaanza kumsuta mtu ambae hata kuongea hajaongea tayari unamkaribisha kwa masimamngo? Wengine unakuta wanaweka vibao vyenye ujumbe aina hii kwenye sehemu zao za biashara kama vile "HAPA CASH TU, KUKOPA HUKO HUKO!" HIVI ni busara kuwasimanga watu ambao hata mdomo hawajafungua?
NAWASILISHA!!!