Mume anapo-support ujinga wa mkewe!!!!

kiukweli hizi ujumbe hazileti picha nzuri. Ila kwa upande wa pili ujumbe unakuhusu umeletea nini jamvini mambo ya nyumba za watu
 
Nakubaliana na wewe Ashadii. Labda ni shule ndogo kama alivyosema mchangiaji mmoja hapo. Na kwa kuongezea ni kuto kujiamini.Nimeshaona nyumba za watu wamebandika eti "am the boss in this house and my wife has the right to say so" Upuuzi mtupu. Nani kakuuliza kama wewe ni bosi au kidampa? Watu wamekaa kiugomvi ugomvi tuuuu. Nani asojua kuwa wewe ni bosi ndani kwako mpaka uweke tangazo. Mimi watu kama hao wala siwaulizi ila nawaweka kwenye kundi la watu ninaowadharau. Kweli watu hawajuhi kuishi na watu; wanakaribisha ushari na unaona dalili mpaka masebuleni kwao.

NK sometimes hio ndio the best solution... Ukizingatia ni watu wazima, kaweka kibao kama hicho, kitu gani utamwambia akuelewe?? Labda kama ni rafiki yako saana na ni muelewa unajaribu maana anakua anakusikitisha jinsi anavojichora....
 
Ustaarabu huna mkuu kajipange upya, maana kuja na hiyo generalization ya kuwa wanawake wa ukanda wa pwani wanapenda mipasho kwenye kadamnasi kubwa namna hii inaonyesha kuwa huna ustaarabu.

Pili kuingia hapa na heading hiyo ya "mtu anapo-support UJINGA wa mkewe" inaonyesha kwako ustaarabu ni sufuri. Huwezi kuwa mstaarabu ukamwambia mtu mkewe mjinga

Tatu wewe si mstaarabu kwa sababu uliuliza masuala personal ya wanandoa bila kujua kikomo chako

HESHIMA yako mkuu lakini mie sipo ktk malumbano ingawaje nafahamu kwamba UJINGA sio tusi na kuhusu wanawake wa pwani, nawafahamu kv mimi mwenyewe ni mtu wa pwani na hata hapa ninapokaa naishi na watu wa pwani; siwatukani wala kuwakejeli kwani kufanya hivyo itakuwa ni kumfanyia hata mama yangu. Ninachofanya, ni kusema tabia zetu watu wa pwani!!! By the way, sikumuuliza mbona mke wake hapati mimba au kwanini akiondoka anachelewa kurudi (kwa mtizamo wangu usiokuwa wa kistaarabu hayo ndo naona mambo binafsi na ya kindoa); nilichofanya ni kumshauri nini perception ya maandiko kama yale kwa jamii! take the note MR. CIVILISED!
 
Hiyo inaitwa "power of a woman" utaelewa vizuri inavyofanya kazi ukishaoa.
Teh! Teh! Teh! Teh! tangu nijiunge JF leo ndiyo kwa mara ya kwanza nimechekeshwa mpaka chozi limenidondoka. Unajua sisi "waswahili" mipasho ni sehemu ya jamii yetu na ni maisha yetu ya kila siku. sasa jamaa labda hana asili ya pwani ambako mtoto anaanza kupashwa tangu yuko tumboni mwa mama yake. Utasikia mjamzito anaambiwa "mimba ya mchina nini. mbona tumbo kubwa? sasa watu kama hawa bila ya kuwawekea vibao hawakomi. Pole sana NasDaz.
 
hata ujinga una vipimo vyake.......... yawezekana kwa waliowazunguka hao jamaa ndio nambari wani kwa ustaarabu
 
Kwa hiyo mi nikiwa mwanamke ndo inakuwaje? Ungepotezea tu bila kuandika chochote basi!

Naheshimu sana wanawake hivyo naogopa kuwajibu ki2 ninachohisi kitawakwaza, ni hivyo tu kipipi and am telling u from deep inside my heart! Nakumbuka long time back, kuna dada mmoja humu humu JF mara kwa mara alikuwa anapenda sana kuchangia post zangu kwa matusi (sijui ugomvi wetu ulianzia wapi). Hata hivyo, nilimuomba aache hiyo tabia kwani naheshimu sana wanawake hivyo nilichelea nisije nikatumia lugha ambayo yeye alikuwa anaitumia! Sisemi ww umenitusi; ila nilihisi kukujibu sawa na ulivyochangia ingepelekea kujibu isivyo busara!
 
Umeona eeh. Nyumba kama hizo zinaweza sababisha mabinti kudoda wakaanza kutafuta mchawi kumbe mabango.

Mimi kama ningekuwa natafuta mchumba,ndio tumeenda nyumbani kwa mchumba tukakuta kibao hiko....

Lazima ndugu zangu wangeniambia duh...huu ukoo umekaa kimipasho na kishari

kazi unayo......
 
HESHIMA yako mkuu lakini mie sipo ktk malumbano ingawaje nafahamu kwamba UJINGA sio tusi na kuhusu wanawake wa pwani, nawafahamu kv mimi mwenyewe ni mtu wa pwani na hata hapa ninapokaa naishi na watu wa pwani; siwatukani wala kuwakejeli kwani kufanya hivyo itakuwa ni kumfanyia hata mama yangu. Ninachofanya, ni kusema tabia zetu watu wa pwani!!! By the way, sikumuuliza mbona mke wake hapati mimba au kwanini akiondoka anachelewa kurudi (kwa mtizamo wangu usiokuwa wa kistaarabu hayo ndo naona mambo binafsi na ya kindoa); nilichofanya ni kumshauri nini perception ya maandiko kama yale kwa jamii! take the note MR. CIVILISED!

Bado pale pale ustaarabu huna, na ndio maana unakuja na sababu nyepesi kutetea maneno yako.

Ujinga si tusi lakini akitokea mtu akakwambia mama yako ni mjinga in black and white atakuwa si mstaarabu japo kuwa inaweza kuwa kweli. Kumwita mtu mjinga si ustaarabu na naamini umeweza kumwita mke wa mwenzio hivyo licha ya kuwa unashindwa kumwita mzazi wako hivyo

Pili, hao wanaodhalilisha wanawake kila siku si kama hawajazaliwa na wanawake, lakini kuzaliwa huko pekee hakuwazuwii kukosa ustaarabu kama kulivyoshindwa kukuzuwia wewe kwenye thread hii.

Majibu ya kuwa " wewe ni
Mwanamke kwa hiyo sikujibu" yapo wazi kuonyesha ukosefu Wa ustaarabu uliotukuka kwako
 
Nilikua sina maana kua what you did was wrong... NO! Ulifanya vizuri kumueleza (thou i have a feeling the way ulimueleza kwa mtu ambae ame condone mkewe aweke such kibao) labda kidogo haikuwa effective.... Na I bliv hii thread ni moja ya topics ambayo ni constructive, vyaweza onekana kama vitu vidogo but huleta maana kubwa saaana kwa observers wengine hasa wageni....

Hata mimi nilikuelewa kabisa ingawaje nakiri kwamba ktk muendelezo wa maelezo yangu VS ur post it was like nilikuwa na-justfy kwa kuhisi umenielewa vibaya! i knw wht u really meant.
 
Boss hilo ni kweli kabisa. Familia makini uwa wanafanya research kabla kutoa baraka za vijana wao kuoa. Sasa haya mabango yanarahisisha saana kazi ya kupata ukweli kuhusu koo zisizo karimu na koo zenye mdomo mchafu.
Hakuna mtu anataka mwanae aoe binti aliyelelewa na mama mwenye kuweka bango kama hilo sebuleni including me. Maana najua huyo mkwe amekuja kuvuruga upendo kwenye familia yetu.

Ni kweli watu wa pwani (wenye elimu ndogo lakini) wanapenda mipasho. Kuna binamu yangu alioa pwani; yani yale makawa anayotumia kufunikia chakula cha wageni ukisoma meseji huwezi kula.

Shangazi na wifi wakawa hawaivi kwa sababu ya mdomo wa wifi na mumewe alikuwa na pesa sana na anategemewa na mama yake.

Mwisho wa siku waliishia ku divorce though after 20 years of marriage is when the husband alipoanza na yeye kuona tatizo
wapo wadada wana sifa zote za kuolewa
but wanaume wanaambiwa ukoo gani ule.....
Utasikia binti hana tatizo but ule sio ukoo ,achana nao...
Yapo saana mitaani...
 
Bado pale pale ustaarabu huna, na ndio maana unakuja na sababu nyepesi kutetea maneno yako.

Ujinga si tusi lakini akitokea mtu akakwambia mama yako ni mjinga in black and white atakuwa si mstaarabu japo kuwa inaweza kuwa kweli. Kumwita mtu mjinga si ustaarabu na naamini umeweza kumwita mke wa mwenzio hivyo licha ya kuwa unashindwa kumwita mzazi wako hivyo

Pili, hao wanaodhalilisha wanawake kila siku si kama hawajazaliwa na wanawake, lakini kuzaliwa huko pekee hakuwazuwii kukosa ustaarabu kama kulivyoshindwa kukuzuwia wewe kwenye thread hii.

Majibu ya kuwa " wewe ni
Mwanamke kwa hiyo sikujibu"
yapo wazi kuonyesha ukosefu Wa ustaarabu uliotukuka kwako
Muhusika niliyemwambia hivyo nimemfafanulia naamini atanielewa. Naomba mheshimiwa, NIKO CHINI YA MIGUU YAKO, TAFADHJALI SANA, USIJIBU NINACHOKIANDIKA especially kwa lugha unayotumia unless kama kuna ki2 unatafuta!
 
boss hilo ni kweli kabisa. Familia makini uwa wanafanya research kabla kutoa baraka za vijana wao kuoa. Sasa haya mabango yanarahisisha saana kazi ya kupata ukweli kuhusu koo zisizo karimu na koo zenye mdomo mchafu.
Hakuna mtu anataka mwanae aoe binti aliyelelewa na mama mwenye kuweka bango kama hilo sebuleni including me. Maana najua huyo mkwe amekuja kuvuruga upendo kwenye familia yetu.

Ni kweli watu wa pwani (wenye elimu ndogo lakini) wanapenda mipasho. Kuna binamu yangu alioa pwani; yani yale makawa anayotumia kufunikia chakula cha wageni ukisoma meseji huwezi kula.

Shangazi na wifi wakawa hawaivi kwa sababu ya mdomo wa wifi na mumewe alikuwa na pesa sana na anategemewa na mama yake.

Mwisho wa siku waliishia ku divorce though after 20 years of marriage is when the husband alipoanza na yeye kuona tatizo

yaani haya yapo mno,
halafu ni culture.....kwa mfano kuna culture hasa watu wa tanga,wadigo
neno dogo kwao ni kuubwa....
Sasa mkikutana na watu wengine wasiopenda maneno kabisa...ni mzozo.....
Kuna culture kama hizo ambazo watu wana expect hila,hata kama its nothing...
 
Ni kweli wao kwa wao wamezoea maneno.

Sasa ukutane na mtu wa bara utaongea kitu wewe unakiona kidogo yeye atageuza simulizi kuwa ametukanwa. Cultural differences ni kazi sana ku cope nazo.

Watu wa bara inabidi ufanye calculation ya kila unachomwambia mtu alokuzidi umri especially mkwe.

yaani haya yapo mno,
halafu ni culture.....kwa mfano kuna culture hasa watu wa tanga,wadigo
neno dogo kwao ni kuubwa....
Sasa mkikutana na watu wengine wasiopenda maneno kabisa...ni mzozo.....
Kuna culture kama hizo ambazo watu wana expect hila,hata kama its nothing...
 
Muhusika niliyemwambia hivyo nimemfafanulia naamini atanielewa. Naomba mheshimiwa, NIKO CHINI YA MIGUU YAKO, TAFADHJALI SANA, USIJIBU NINACHOKIANDIKA especially kwa lugha unayotumia unless kama kuna ki2 unatafuta!

Kwa kumalizia tu ungejua ustaarabu usingeandika kwa herufi kubwa :]
 
ni kweli wao kwa wao wamezoea maneno.

Sasa ukutane na mtu wa bara utaongea kitu wewe unakiona kidogo yeye atageuza simulizi kuwa ametukanwa. Cultural differences ni kazi sana ku cope nazo.

Watu wa bara inabidi ufanye calculation ya kila unachomwambia mtu alokuzidi umri especially mkwe.

na mizozo mingine inaanza siku ya harusi....
Harusi za siku hizi vishindo vitupu

utasikia zawadi ya upande wa mume ni gari.....halafu inasubiriwa zawadi ya upande wa mke
utasema mashindano hivi.....lol
 
yaani haya yapo mno,
halafu ni culture.....kwa mfano kuna culture hasa watu wa tanga,wadigo
neno dogo kwao ni kuubwa....
Sasa mkikutana na watu wengine wasiopenda maneno kabisa...ni mzozo.....
Kuna culture kama hizo ambazo watu wana expect hila,hata kama its nothing...
Tanzania nzima wenye culture hiyo umeona wadigo tu.....
 
...Last week, nilimtembelea rafiki yangu mmoja ambae mwenzangu ameoa ... Ile kuingia tu sebuleni, nikakutana na kibao kilichoandikwa "UKIJA UJE NA YAKO, UMBEYA NYUMBANI KWAKO!" Kwa bahati shemeji yangu (mke wa mshikaji) alikuwa hayupo kwa muda huo hivyo tukapata nafasi ya kutosha kujadili masuala ya kimaisha. Baada ya mimi kuona kibao hicho, nikamuuliza mshikaji kwanini ameweka hicho kibao. Akajibu, aliyeweka si yeye bali ni mke wake! Nikamuuliza kawalenga akina nani; akajibu "sijui yeye mwenyewe!" Baada ya majadiliano ya hapa na pale, nikamshauri akiondoe kibao hicho kv anafanya embrassement kwa wageni wake! Jamaa akadai kv alikuwa ni mke wake basi asingeweza kukiondoa yeye kv mke wake na yeye ana haki na hiyo nyumba! kimsingi, nilishindwa kabisa kumshawishi kukiondoa kibao hicho! ...

kama hujaombwa, si vizuri kutoa vilecture na ushauri juu ya maisha ya mwenzio, hasa yale yahusuyo mambo ya ndoa.

Hata kama watakuwa waswahili, hayakuhusu. Wewe endelea na 'ustaarab' wako na tafuta marafiki wastarab wa kuwatembelea.
 
Umenichekesha. Bora kushindanisha zawadi kwani ni faida kwa wanandoa.

Kuna zile za nyimbo za mipasho harusini. Oooh walisema amuoi mbona kamuo. Tena vidole wanawanyooshea wakwe na mawifi; si balaa ni nini?
Badala ya kuweka nyimbo za furaha na pongezi wanaanza mipasho. Oooh kwetu alikuwa anakula nyama msimpe kauzu.

Basi unakuta watu waanza kununiana toka siku ya harusi.

na mizozo mingine inaanza siku ya harusi....
Harusi za siku hizi vishindo vitupu

utasikia zawadi ya upande wa mume ni gari.....halafu inasubiriwa zawadi ya upande wa mke
utasema mashindano hivi.....lol
 
Back
Top Bottom