"Mume amefariki leo, Mke anaolewa kesho"...!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

"Mume amefariki leo, Mke anaolewa kesho"...!!!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mwita Maranya, Mar 16, 2012.

 1. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #1
  Mar 16, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Wadau wa MMU, habari zenyu bana.

  Juzi kati nilikuwa nimekaa kwenye kiti kirefu mahali fulani katikati ya jiji, pembeni yangu kulikuwa na meza wamekaa mashostito wawili wanapiga stori huku wakilamba vimiminika na mdudu.

  Mwanzoni walikuwa wanazungumza kwa kunong'ona, lakini baadae kadri stori ilivyonoga na kinywaji kukolea, ndipo mmoja wao aliyekuwa anaonekana kutoa masimulizi muda mrefu akafyatuka kwamba;
  "Siku mume wangu akifa, kesho yake naolewa. Tafadhali sana msije kuniuliza huyo mchumba nilimpata lini na wapi". "Tena natamani life hata leo hii ili nipate furaha, kwanini niendelee kuteseka kwa sababu ya limmbwa lisilojua thamani ya mke?" Life is nothing if i'm not happy (akaweka msisitizo kwa kidhungu)!!

  Baada ya kusikia hivyo, sikutaka kuwa shahidi katika kesi inayoweza kumpa mtu life ban ama kitanzi, nikapiga funda la mwisho nikajiondokea zangu huku nikijiuliza huyo bwana kamkosea nini mkewe hadi amuombee kifo?

  MYTAKE:
  Akina dada na akina mama wa hapa JF naomba kufahamu kupitia kwenu, ni kosa gani huyu mume kamtenda mwenzenu hadi anamuombea kifo? Je tayari ameshapata mchumba/mume mwingine anasubiri tu kifo cha mumewe ili atimize ndoto zake?:scared::thinking:
   
 2. Dreamliner

  Dreamliner JF-Expert Member

  #2
  Mar 16, 2012
  Joined: Jan 17, 2010
  Messages: 2,034
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Hiyo mbona kawaida? Watu kuwa na nyumba ndogo na vidomola ndio maisha ya leo.
   
 3. Foundation

  Foundation JF-Expert Member

  #3
  Mar 16, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 1,458
  Likes Received: 256
  Trophy Points: 180
  Ulipata bahati ya kujua/kuhisi kabila la huyo mwanamke anayependa mumewe afe? Ukinijibu nitarudi tena
   
 4. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #4
  Mar 16, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Kweli nyumba ndogo siku hizi inaonekana jambo la kawaida na kwakuwa watu wengi wanaendekeza, lakini hili la kumuombea mume wake kifo limekaaje?
   
 5. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #5
  Mar 16, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  sina uhakika sana lakini kwa jinsi nilivyomsikia akizungumza alikuwa akitajataja sana makambako, bila shaka atakuwa from nyaluland!
   
 6. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #6
  Mar 16, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  Mmmh, nikikoment hapa, naweza shabngaza sana.
  Ngoja nipite.
   
 7. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #7
  Mar 16, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,506
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  MM, usipate presha. Mungu ana akili sana kuzuia kusoma ubongo wa mwenzio manake siku ukijaaliwa kujua kila dakika nini kinapita moyoni mwake, utakufa siku si zako. Umeshaona malalamiko meengi ya wanawake humu jamvini, yoote kwa ujumla yake, yanaweza kuchangia kwa kiasi kikubwa kuwa na ndoto hizo.

  Ila usishtuke, mkeo hataolewa next day yake ili wasimsumbue na mirathi, ata-lay low kwanza ahakikishe anavuna,lol!
  Its friday, keep smiling.
   
 8. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #8
  Mar 16, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Mkuu,
  Familia nyingi sana ziko kwenye mtindo huo unaoendana na hadithi/simulizi lako!
  Aidha, couples nyingi(approx 65%)zilishatengana zamani sana, na wanaishi pamoja kwa vile ni aibu kila mtu kurudi kwao, na labda mwingine wazazi wake walishatangulia kunako haki, hivo anakuwa hana pa kwenda.

  Sasa hali hii inapokuwa Backed up na uwepo wa mtu wa nje(kimada au Buzi) basi inakuwa amplified, maana mtu anajua hata akiachwa, au mwenzake akifariki, basi yeye hatokufa njaa, maana ana mtu atakayegharamia maisha yake.
   
 9. s

  sawabho JF-Expert Member

  #9
  Mar 16, 2012
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 4,504
  Likes Received: 946
  Trophy Points: 280
  Naweza kuwa na nyumba ndogo, lakini siwezi kumwombea mwenza kifo ili niioe/olewa na hiyo nyumba ndogo. Kwanza ieleweke kwamba mtu wa nje anakupenda tu kwa sababu haingii gharama kubwa kukutengeza, uanakuja kwake ukiwa unawaka kutokana na gharama za mke/mume uliyenaye ambaye unaona anakuudhi. Kumbuka kuwa hata kama anakuudhi vipi, kitendo cha yeye kuwepo kuna nafasi fualani anachukua katika maisha yako.
   
 10. A

  Ave Ave Maria JF-Expert Member

  #10
  Mar 16, 2012
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 10,757
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Ukweli anaujua ye mwenyewe! Lakini naweza sema huyo dada ni mmoja wa watu wanaoishi kwa kutegemea mwanaume na wapo kimaterial zaidi, yaani anaomba huyu afe ili aolewe na yule?? Tena ukute hata mumewe hajamtenda kosa kubwa kivile, ila ni ushambenga tu na kufuata mkumbo ndo vinamsumbua! Mwanamke mwenye akili timamu na anaejielewa vizuri hawezi kuongea maneno kama hayo achilia mbali kwa marafiki tu......hata kwa ndugu zake labda na wao wawe chenjeu kama yeye!
   
 11. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #11
  Mar 16, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Haya mambo huwa yanashangaza sana.
  Kuna baadhi ya makabila mke akifiwa na mume anapata mume wa kumrithi fasta, lakini mume akifiwa anaweza kuchukua muda kidogo kupata jiko lingine.
  Kwa hiyo huyo mwanamke yuko sahihi akifiwa na mume leo anarithiwa na mume mwingine kesho na wala haigombi!
   
 12. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #12
  Mar 16, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Kongosho,
  Jaribu kutushangaza tu, usipite kimya kimya, mawazo yako ni muhimu hapa.
   
 13. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #13
  Mar 16, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Kuna mke wa jamaangu mmoja ambaye aliamwambia mumewe baada ya kutoelewana ndani..."Nimechoka, naenda kwa Mamaangu!"
  Familia hiyo ilikuwa na Watoto 7.
  Basi mumewe akamjibu..."Ni sawa tu, nenda kwa mama yako, Ila sasa hivi na mimi nimeamua kurudi kwa Mama yangu mzazi, lakini ili mambo yaende sawasawa, na hawa watoto wetu saba wote waende kwa mama yao!
  Mke yule kusikia hivyo akamwambia mumewe ..."Yaani Una maana watoto waje kwangu sio!"...Basi nimebadilisha mawazo siendi popote!
  Familia zetu hizi ziko flagile sana, hakuna upendo.
   
 14. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #14
  Mar 16, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Tatizo ni kuwa watu huharakisha sana suala la ndoa......unakutana na mtu hata hujamjua vizuri unatatfuta wazazi wake uoe......unapokuja kumjua vizuri too late......ndio haya ya kuombeana vifo
   
 15. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #15
  Mar 16, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Huyu shostito kwa maelezo yake anaogopa tu kusemwa na watu kwamba kamkimbia mume kwahiyo ameamua kuendelea kuishi naye lakini anaonekana amechoka kabisa. Kwahiyo anadhani suluhu ya matatizo yake ni pale tu mumewe atakapotangulia mbele ya haki.
   
 16. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #16
  Mar 16, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Kwa maelezo ya huyu shostito ni kwamba yeye ndiye anatunza familia, nadhani wana mtoto/watoto, anayo kazi nzuri inayomuingizia kipato cha kutosha(ofcourse alitaja mahali anapofanya kazi, ni kampuni kubwa hapa nchini).
  Kinachomtatiza ni kwamba mume haonekani kumjali kabisa, haonyeshi mapenzi yoyote kwake, anahisi kama ana mwanamke mwingine.
   
 17. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #17
  Mar 16, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Sasa ana uhakika gani kama nani kati yao atatangulia?...Hapo ndipo wazo la kumwekea mtu DIDIMAC kwenye chai linapozaliwa!...huh!
   
 18. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #18
  Mar 16, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  Yaani hapo pana maana sana.
  Kuna kisa nimekutana nacho wiki hii, nakihusisha sana na hapo, ila nimeshindwa jinsi ya kuwasaidia maana mie naye si mtaalamu wa usuluhishi.

   
 19. Foundation

  Foundation JF-Expert Member

  #19
  Mar 16, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 1,458
  Likes Received: 256
  Trophy Points: 180
  Hiyo ni njombeland. Inawezekana sishangai.
   
 20. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #20
  Mar 16, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Mkuu huyu mwanamke alikuwa hazungumzii kurithiwa, alikuwa anamaanisha kwamba ataolewa na mwanaume mwingine anayempenda.

  Utakumbuka alikuwa anamwambia mwenzake kwamba, tafadhali msije kuniuliza huyu mchumba nilimpata lini na wapi!!

  Kwahiyo tayari mume mpya keshapatikana, kinachosubiriwa ni kifo cha mume wa sasa.
   
Loading...