Mume aliyekuacha, akikuingilia kimwili talaka inabatilika?

unlucky

Senior Member
Aug 9, 2011
199
56
Kutokana na matatizo mengi yaliyonikuta mpaka sasa nahangaika nimekuja na swali ambalo hata sie wengine kati yetu hatujui ambalo linahusu talaka.

Swali langu ni: Mume ambaye amekupa talaka ya tatu na uko kwenye Eda, Je kama anakubaka au kufanya tendo la ndoa hapo itakuwa talaka haipo au mmefanya haramu au mmezini? Na je hiyo itakuwa haihesabiki kama kakuacha?

Naomba ushauri.
 
Eda maana yake mume anapokuacha unakaa miezi mitatu halafu ndo baada ya hapo uolewe tena na mume mwingine
 
Kwa sheria ya Allah katika Qur'an tukufu, ukimuacha mke kwa taraka tatu, huwezi kumuoa hadi aolewe tena na mume mwingine, halafu huko alikoolewa akiaachika ndo wewe unaweza kumuoa, tofauti na hapo mkikutana kimwili mnakuwa mnazini,,,,wenye kujua zaidi wataongezea
 
Kwa sheria ya Allah katika Qur'an tukufu, ukimuacha mke kwa taraka tatu, huwezi kumuoa hadi aolewe tena na mume mwingine, halafu huko alikoolewa akiaachika ndo wewe unaweza kumuoa, tofauti na hapo mkikutana kimwili mnakuwa mnazini
Hakika. Hilo ndilo lifamikalo
 
si halali kama alikubaka ! basi huna makosa ,, kama mlikubaliana hapo mmefanya zinaa! as long zilishatoka talaka tatu ..

ndio maana tunashauriwa usitoe tatu mpigo..
 
Kwa sababu kuna uzushi siku hizi eti ukifanya hivyo talaka inabatilika jamani hata ikiwa talaka tatu eti haihesabiki tena jamani hivi nani anajua dini kamili aseme
 
Hapo mtakuwa mmezini na sio vibginevyo. Pili ili mrudiane na mume huyo ni.mpaka uolewe na uachike na hili lisipangwe ili kutimiza hizo haja. Yani itokee tu kwa bahati mbaya kuwa umeolewa na.bwana mwingine na ukaachika bila ya ushawishi wa aina yoyote kutoka kwa bwana wa awali. Mkipanga tu kuwa uolewe na mtu halafu akuache.ili yeye aje.akuoe hapo hakuna ndoa ni zinaaa tu mtakuwa.mnafanya.
 
Mleta mada kagegedwa kakorezwa anatafuta uhalali wa uzinifu wao.HUYO mumeo si alikuacha imekuwaje akarudi mkazini.Ni mazingira yapi alikubaka.mmetamaniana mkazini.na mumeo anaonekana alikurupuka kukupa hizo tatu.
 
unapopewa talaka tatu ina maana wewe sio mke tena wa aliyekupa na Hata mkifanya mapenzi mtakuwa mnazini tu. ili kurudi kuwa mke tena ni mpaka pale utakapoolew na mwanaume mwingine then ukaachwa ndio anaweza kukuoa tena
 
Kwa sheria ya Allah katika Qur'an tukufu, ukimuacha mke kwa taraka tatu, huwezi kumuoa hadi aolewe tena na mume mwingine, halafu huko alikoolewa akiaachika ndo wewe unaweza kumuoa, tofauti na hapo mkikutana kimwili mnakuwa mnazini,,,,wenye kujua zaidi wataongezea
SOMO TAFADHARI:
Hivi talaka tatu maana yake nini? Je kuna talaka moja, mbili, nne?? Kama zipo, zina maana gani??

Alafu hiyo talaka, ni nani ANAITHIBITISHA kuwa sasa wameachana?? Maana nimeshuhudia watu wanaandikiana tu ktk karatasi na "kukubaliana" kuwa wameachana.
 
Unapopewa Talaka ya 3 hakuna mjadala hapo inakuwa ushaachika moja kwa moja na kama mmefanya basi mmezini, kumbuka hiyo ni Talaka ya mwisho haina Marejeano kwa hali yoyote, labda uolewe na mwanaume mwengine uachike ndo yeye mumeo aje akuoe tena, huyo Mwanaume msahau kabsaa, tubu kwa ulivyozini nae, baada ya miezi 3 ikiisha ondoka (Hiyo miezi 3 ni kuhakikisha hakuna kiumb au mimba yake na hekma nyingine), Na kam anakubaka ondoka hapo ila hakikisha huzidi huko nje mpaka miezi 3 iishe utahesabu siku ulofanya nae sasa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom