Mulugo unavumiliaje kashfa hizi?

Mulugo unavumiliaje kashfa hizi?

mathabane

JF-Expert Member
Joined
Jan 27, 2013
Posts
2,405
Reaction score
1,898
Mulugo unatakiwa kutoa majibu kwa utata uliogubika mtiririko wa elimu yako. Kimya chako au majibu butu kwa mtu mmoja mmoja inatia shaka kwa umma wa watanzania.

Kwa akili ya kawaida nilitegemea mtu kama wewe mwenye wadhifa na dhamana ya kusimamia elimu uichukulie hii kama kashfa na kuvipeleka mahakamani vyombo vya habari vnavyokuchafua ama uitishe press conference ili kumaliza kadhia hii.

Sitegemei kwa mtu mwenye wadhifa kama wako awe na kashfa ya aina hii ukitilia maanani umuhimu wa Wizara unayo iongoza.

Yawezekana kimya chako sio upole wa kawaida bali kuvpoza vyombo vya habari ili visifichue uozo zaidi tusofahamu. Fahamu kuwa kimya chako kinahalalisha kashfa kwako binafsi, uwaziri na wizara yako, aliekuteua uwaziri pamoja na wapiga kura wako.

Kama waziri mwenye dhamana ya elimu, elimu yako ni ya mashaka (kughushi), hali ikoje kwa maofisa walioko chini yako. Wizara yako ni miongoni mwa znazo kabiliwa kiwango kikubwa cha wafanyakazi kughushi vyeti, je kama wewe si msafi utapata wapi nguvu na uhalali wa kuwanyooshea vidole wahalifu na matapeli wa elimu?

Mkuu tunasubiri kutoka kwako la vyombo vya dola vfanye kazi yake bila hiana!
 
Kama ingekua ni mara ya 1 kwa mulugo sawa,ila kuna utitiri wa wadhalim,yeye aanze tu kuwajibika.THUBUTUUUUU
 
Halafu mimi ninashangaa, kiwango cha elimu hiki unakuwa boss wa Prof. Rwekaza Mukandala( vice Chancellor wa UDSM)?
 
Mulugo unatakiwa kutoa majibu kwa utata uliogubika mtiririko wa elimu yako. Kimya chako au majibu butu kwa mtu mmoja mmoja inatia shaka kwa umma wa watanzania.

Kwa akili ya kawaida nilitegemea mtu kama wewe mwenye wadhifa na dhamana ya kusimamia elimu uichukulie hii kama kashfa na kuvipeleka mahakamani vyombo vya habari vnavyokuchafua ama uitishe press conference ili kumaliza kadhia hii.

Sitegemei kwa mtu mwenye wadhifa kama wako awe na kashfa ya aina hii ukitilia maanani umuhimu wa Wizara unayo iongoza.

Yawezekana kimya chako sio upole wa kawaida bali kuvpoza vyombo vya habari ili visifichue uozo zaidi tusofahamu. Fahamu kuwa kimya chako kinahalalisha kashfa kwako binafsi, uwaziri na wizara yako, aliekuteua uwaziri pamoja na wapiga kura wako.

Kama waziri mwenye dhamana ya elimu, elimu yako ni ya mashaka (kughushi), hali ikoje kwa maofisa walioko chini yako. Wizara yako ni miongoni mwa znazo kabiliwa kiwango kikubwa cha wafanyakazi kughushi vyeti, je kama wewe si msafi utapata wapi nguvu na uhalali wa kuwanyooshea vidole wahalifu na matapeli wa elimu?

Mkuu tunasubiri kutoka kwako la vyombo vya dola vfanye kazi yake bila hiana!

like,hapo umenena kiongozi wangu
 
hata kujibu tuhuma kama hizi inahitahi utashi wa hali ya juu na maneno yenye uelewa na yaliyopangika. ama sivyo unaweza kuharibu kabisa.
utashi, uelewa na manano yaliyopangika vizuri ya kueleweka mlugo hana. sasa anaomba msaada akimpata wa kumfundisha namna ya kujua kupangua hoja utamsikia atajibu.

ama la hawezi kupangua hoja hizo kama ni kweli atajitia aibu zaidi. ndio maana kaamua kujifanya kupotezea
 
Huyu ni waziri kichekesho! Amejidhalilisha mwenyewe na mamlaka iliyomteuwa.
 
naibu waziri wa elimu amechakachua elimu.

anaogopa asije akaongea kithungu kama hiki mbele ya waandishi"you myself didnt knew why"hahahaaaaaaaaaaaaaaa Tz yangu mieeeeeeeeeeeee
 
ngoja tusikilze tbc fm labda atajibu kupitia huku tehe tehe tehe
 
mtaalamu wa ma -A.K.A huyu, anatumia mpaka majina ya mababu zake, wajomba zake na wahenga!
 
atajibu nini,anatakiwa ni kuachia ngazi tu,kwani gazeti limeandika ukweli mtupu
 
Back
Top Bottom