Mukama(Katibu mkuu wa zamani wa CCM) yuko wapi?

Mukama(Katibu mkuu wa zamani wa CCM) yuko wapi?

KAUMZA

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2010
Posts
699
Reaction score
241
Katibu mkuu ndio injini ya chama chochote kile. Katibu mkuu makini, hufanya chama kuwa imara. Geuza na kinyume chake. Angalia kwa CDM chini ya Dk Slaa na CUF kabla maalim Seif hajawa makamu wa kwanza wa rais.

Katika historia ya CCM, haijapata kutokea katibu mkuu aliyefunikwa kama mzee Mukama. Watangulizi wake wote walikuwa machachari katika duru za siasa. Angalia enzi za Pius Msekwa, Marehemu Rashidi Kawawa, Marehemu Horace Kolima, Marehemu Lawrence Gama, Mangula na hata mzee Makamba. Hawa wote sauti zao zilikuwa zinasikika.

Au kawa katibu mkuu wa heshimu "ceremonial chief secretary"? Maana viongozi wa heshima ni nadra sana kupaza sauti zao, na hata wakipaza huwa ni ushauri/maoni tu. Kwa CCM, inavyoonesha katibu mtendaji ni Nape Nauye.

Mukama, ibuka kutoka huko ulikofichwa, uje ujibu hoja za Dk Slaa na M4C. Dk Slaa anasema Nape (Katibu wa uenezi) si saizi yake. Anakutaka wewe katibu mkuu mwenzake.
 
nape anamuingilia kazi zake ,jamaa kaamua kuzira kazi za chama!
 
He has given up; anangoja baada ya uchaguzi wa magamba aenguliwe kwani wenye chama wameona amekuwa mzigo!! Ameshindwa kuyavua magamba, kama mzee wa VIJISENTI alivyosema kuwa gamba limekwama kiunoni!!
 
Swali zur, manake hata mi nilitegemea kumuona kipindi hiki kigumu (Sensa) kwa Boss wake Jk...!! Nadhani kuna kitu kipo chini ya Kapeti..!! Wait & see..!!
 
baada ya kufa kwa ukomunisti, matokeo yake ni viongozi wengi wamejikuta hawajui kazi. Ona Pinda, Ona Nape, na sasa ona Mukama. Mukama yupo ila hajui kabisaa afanye nini.

Hao makatibu wa zamani unaowapa sifa kuwa walikuwa wanatamba sana, ukichunguza sana hotuba zao, utagundua zilikuwa Pumba sana na za kukera kichwa!

NImesoma SAUT na waandishi wa habari wengi sana. Walikuwa wana lalamika kuwa hao makatibu ukienda nao safarini huko mikoani, walikuwa wnalazimisha sana hotuba zao uzipambe na kuongeza maneno ya uongo na kusensa maneno memngine aliyokuwa anlaghai.

Unakuta katibu mkuu anampigia simu mwandishi wa habari asubuhi na kumlalamikia kuwa kaandika vibaya hotuba yake. Leo hii mambo hayo hayapo tena, litakiwa ni kuonesha ugenious wako ktk kulea wananchi na sio kuimalisha chama tena.
 
Atafanya nini wakati Nape anaingilia hadi kazi zake ameona akapumzike Dubai!
 
Kama kweli kaingiliwa kazi zake na Nape(katibu wa uenezi) na akakubali, sitakuwa nimefanya makosa nikiifananisha CCM na BATA "mzazi". Maana Bata "mzazi" always huwa anaongozwa na watoto wake. Katibu mkuu unaingiliwa na katibu wa uenezi? Shame!!
 
Nakumbuka aliingia kwa mbwembwe na msamiati wa 'GAMBA' ila tulielewa dhahiri katibu huyu hataweza kubadili kitu katika chama Sugu kilichozeeka cha CCM.

Tumejionea alivyoshindwa kazi, hasikiki nae akiwa ni miongoni mwa SAGAMBA yanayotakiwa yaingie mitini kwani 'ameprov failure' tofauti ya matarajio ya aliyemteua.

NASHANGAA KUMUONA AKIPIGA MAKOFI NA MWENYECHUKI WAKE WAKIIMBA,NAJIULIZA HIVI 'SIKU HIZI MUKAMA AMEKUWA KATIBU WA VIKAO NA NYIMBO ZA CCM'? Maana magamba kwa kuimba kwa kweli hapo chadema hatuoni ndani!!!
 
sasa hivi yeye na nape wanajigonga gonga tu. Si unaona nape alivyomdogo? Hata jina la lowasa halitamki tena
 
Anasubiri hatima yake baada ya uchaguzi! Uchaguzi ukikamilika, waliochaguliwa wataunda secretariate mpya. Ni muujiza tu ndio utakaom'bakiza!
 
Jamani yuko wapi aliyekuwa katibu mkuu wa CCM Wilson Mukama,mbona hackiki cku hizi,kweli magamba noma.
 
Jamani yuko wapi aliyekuwa katibu mkuu wa CCM Wilson Mukama,mbona hackiki cku hizi,kweli magamba noma.

Kweli mkuu Lundala, huyu jamaa katupiliwa wapi? Hivi alikosea nini hadi akaondelewa? Au kwa kuwa kijana paparazi alikuwa hawaivani na yeye alikuwa hayuko tayari kushabikia uongo wa chama chake!! Kweli magamba noma!
 
Kwani hajaenda kwenye matibabu mpaka leo?

3.%2BBalozi%2Bwa%2BChina%2Bna%2BKatibu%2BMkuu%2Bwa%2BCCM.jpg
 
Kwani hajaenda kwenye matibabu mpaka leo?

3.%2BBalozi%2Bwa%2BChina%2Bna%2BKatibu%2BMkuu%2Bwa%2BCCM.jpg
Alikuwa naumwa mkuu Safari_ni_Safari? Sikuwahi kusikia sana kama Mukama alikuwa mgonjwa kivile!!!! Naona kuna namna tu hakutakiwa na itabidi atulie kimya milele!!
 
Back
Top Bottom