Mukama aviabisha vyombo vya Usalama: Adai CDM imeingiza mamluki toka ng'ambo

...Uwezo wa mtu kiuongozi unapimwa kwa kupiti namna anavyotoa matamko kwa umakini,mfumo huu wa viongozi wa CCM kutoa matamko bila kuwa na tafiti za kudhibitisha unawashushia heshima viongozi wengi wa CCM na hata serikali....Utashangaa kauli nzito kama hii itachukuliwa kawaida na vyombo vya usalama,na hapo ndipo uwa shaka inaingia kuwa ilikuwa ni danganya toto kuchafua chama kingine au ni uwezo mdogo wa vyombo vyetu vya dola kufanya uchunguzi wa hoja kama hizi...Mwisho wake,unafanya hitimisho kuwa CCM inakosa viongozi wa hulka kama za Mwalimu JK,Kawawa,Sokoine nk...
 
Kinachonishangaza ni kuwa wanasema wanao ushahidi, basi naomba wawakamte kisha wawafungulie mashitka na kuthibitisha tuhuma zao? Hili jambo siyo la kulipuuza, nionavyo tayari JK atakuwa ameshampigia Mkama kumuonya aache ujinga wa kuropoka hovyo!
 
Kweli kwa serikali ya CCM kuna kazi sana .Hawa usalama wa Taifa wasivyo naupeo wa kufuatilia mambo wanafikiri mukama na viongozi wengine kama kina nape wapo juu ya sheria.Hili ni tatizo kubwa sana ,usalama wa Taifa upo kama vile ni usalama wa CCM.
 
Real,, Mukama anatakiwa awe tayari na taarifa/RB ya polisi, ni madai mazito kuacha yanaelea tu. Ila kwa polisi iliyoegemea upande wa ccm utashangaa wamekaa kimya kabisa
 
Mwanzo wakati anapewa kipenga cha umagamba alijua ni kazi rahic sana.Sasa hv namuona na UTANDO MWEUPE MDOMONI.

Kama chadema wameweza kuwaingza hao makomandoo hewa,vyombo vyetu vya ulinzi havijui ni wazi TZ haina ulinzi wa mipaka zaidi ya mali zao za ndani

Nimemsikiliza kwa Makini sana.Mukama ila sijaona cha Maana ktk kinywa chake,Amejaa jaziba ambazo zimewapelekea kuunda uongo bila kufikiria kuwa kuna vyombo husika.

Kama wamepita vyombo vya ulinzi na usalama vikajua na kukaa kimya hyo ni ishara ya Magamba kuchokwa kwa nguvu zote.
Hakuna Marefu yasiyo na nukta.
 
Viongozi wa CHADEMA wafanye haraka kuwasiliana na balozi za Libya, Afghanistan na Paksitan wazitaarifu juu ya jambo hili nafikiri John Mnyika atanisoma.
Ila Mukama unatuchanganya nilifikiri magaidi wametoka Vatican kumbe nchi za kiislam sasa CDM na waislamu wapi na wapi, ukiwa mwongo jaribu kutunza kumbukumbu. Halafu najua kwanini ameitaja Libya guess what?.......
 
Hivi huyu Mukama anaelimu gani na amesomea nini?
Yaani hata ukiwa kama malaika ,ukiingia CCM tu basi ..kwisha kazi yako! Andrew Chenge amepiga postgraduate Harvard..lakini maamuzi yake ni kama topical/ritz/ami/malaria sugu....! hiyo ndiyo CCM.
 
Nilikuwa siku zote tangu RA atangaze kujivua gamba kwa kusema amechoshwa na siasa uchwara za ccm na istaajabu kauli hii. Leo mukama amenifumbulia alichomaanisha RA. Kuwa ccm inaongozwa na viongozi uchwara, wenye siasa uchwara, mikakati uchwara na kubwa zaidi kauli uchwara. Hivi viongozi wa aina ya mukama si wana siasa uchwara kweli? Huyu ni kiongozi wa juu wa chama tawala anataka tuamini kuwa uwezo wa kujilinda wa nchi yetu ni saizi ya makomandoo 30 tu. Naamini hata hawa wa uwt wa kitengo cha propoganda hapa jf wameishiwa nguvu. Utawabebaje viongozi hawa na chama hiki, hawabebeki, hakibebeki.
 
Mkama hana tofauti na kilaza Makamba ...CCM imezeeshwa na magonjwa sugu mawili,ugonjwa wa kwanza ni Makamba na ugonjwa wa pili ni Mkama
 
Nilimsikia kwa mara ya kwanza Mukama akifafanua hoja ya kujivua gamba, nakumbuka alieleza sana kwa mifano mpaka akafanisha jinsi mtu anavyofungua kifuniko cha chupa mara damu inavyo zunguka mwilini nk. Lakini mpaka anamaliza sikumwelewa, nilijua ni mgeni kwenye chama ila leo ameniacha hoi kumbe Mukama hajielewi kiasi hicho, nimemkumbuka Y. Makamba pamoja na blanda zote ila kidogo alijenga chama huyu Mukama anakibomoa yaani ametapika nyongo. Jamani hivi ccm hakuna mwenye uafadhali kila anaejitokeza anafuka moshi. Nimeamini ccm imeshikwa pabaya yaani wanatapatapa kutafuta huruma. Ukweli Cdm ikishinda Igunga basi wabunge wengi wa ccm wajiandae kupoteza majimbo 2011.
 
Saidi Mwema anapaswa kumuhoji Mukama kwa nia ya kuwakamata hao makomandoo wavamizi kwa sababu ushahidi anao Mukama na anawajua kwa majina na mahali walipo. Kama ni uongo tutajua maana najua hii taarifa hii itapotezewa na jeshi la polisi kwa sababu ni utunzi wa Nape huu.
 
Kutojua na kutosoma nyakati ndo tatizo lililoko hapo NYINYIEM(ccm) there is one school of thought that these people do ignore WHEN POWER IGNORE WARNINGS IT WILL BECOME POWERLESS.
 
kuna hatari kubwa iwapo wanasiasa watafanya mzaha na mambo ya kiusalama na kuyatumia kujinufaisha kisiasa. ina maana huko mbeleni likitokea jambo hatari kiusalama tutshindwa kuelewa tofauti ya propaganda na uhalisia. kuna hatari ya kujenga ujasiri uliopitiliza kwa raia hivyo kupata ugumu hapo baadae wa kutoa amri au tahadhari ya kiusalama na ikazingatiwa
 
i have bad feeling too, they must have something behind mukama's word...

 
hizi taarifa nilitumiwa na mwana jf mmoja akiniambia kuwa ccm wanajipanga kutumia mbinu hizi pamoja na kuwambambikia madawa ya kulevya nilizipuuza mnaana niliziona za kitoto/kijinga mno wasingetumia...lakini siku ya 2 baada ya kupata kweli njia moja wameitumia bado ya madawa ya kulevya..
 
Mkama hana tofauti na kilaza Makamba ...CCM imezeeshwa na magonjwa sugu mawili,ugonjwa wa kwanza ni Makamba na ugonjwa wa pili ni Mkama
Tofauti yao ni kwamba Makamba alikuwa mdomo mwingi baadae anawaruka mlininukuu vibaya, huyu Mukama alianza kwa ustaarabu, ni kama mlevi wa gongo anapoingia kilabuni alivyo mstaarabu na tai shingoni mwangalie wakati anatoka tai kiunoni shati kifua wazi. Mambo Mkama aliyoyakuta humo kumbe ndivyo yasivyo hajui aseme kipi aache kipi anajikuta anaropoka hovyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…