Mukama asema mafisadi hawaponi ng'o! CCM yaunda kamati maalum

Kuna taarifa kwamba Mukama amekutana na waandishi leo na amerudia tena taarifa yake kuhusu magamba na kuapa kwamba hakuna fisadi aliyesafishwa Dodoma na badala yake magazeti yamekua yakipotosha kwa maslahi yao.
MUkama anapaswa kutuacha watanzania tushughulike na masuala mengine maana tuna matatizo mengi sana binafsi zaidi ya hayo magamba yao. Kama anadhani wanaweza kuyasafisha magamba, basi wafanye watakavyo na hakuna haja ya kututangazia. Au anadhani watu hatuna akili?
 
sasa si watofukuzwa karibia 70% maana karibia wote ni mafisadi, walio serikalini wanawapelekea wajumbe wa mikutani, wenyeviti, na makatibu wa taifa, mkoa, wilaya mpaka tawi. kuna wengine ndio hivyo wana saini kandarasi mbovu mbovu, wanachukua fedha kutoka taasisi zilizo chini ya wizara zao, wengine dada zao wanawatafutia fedha toka kwa wachumba zao ili baadae mchumba apewe eneo la uekezaji, mpaka auditor general na chief secretary nao wanaingizwa kwenye ufisadi, na sasa tunaona pia tanil anatumiwa kuwalainisha wana usalama wetu, sasa sijui kwenye mahakama thetu kukoje huko?
 
Mukama aache kutuuzia chai vijiweni hivo juu ya UFISADI, kwa mujibu wa katiba ya CCM Mukama hana mamlaka ya kumfukuza yeyote barabarani.:embarassed2:

Kwa kuwa mambo hayo yalishashindikana kwenye vikao halali ya maamuzi ya chama ndio basi tena Wa-Tanzania ndio hivo tumeshaupokea ujumbe wao huo KWAMBA KUMBE UFISADI NI SERA RASMI YA CCM ambayo tuhuma zitokanazo na swala kama hili wala si kitu cha kumfukuzia mtu chamani.
:embarassed2:
Kuna taarifa kwamba Mukama amekutana na waandishi leo na amerudia tena taarifa yake kuhusu magamba na kuapa kwamba hakuna fisadi aliyesafishwa Dodoma na badala yake magazeti yamekua yakipotosha kwa maslahi yao.
 
Ni kweli ameongea na waandishi na amesema magazeti yamepotosha sana na mimi naongeza humu nako kuna watu wako kazini, duh!! Hadi raha maana unaona kama sinema vile
Kiranja umepatia 100%; hivi huyu Mukama ndiye yule aliyewahi kuongoza Jiji au ni mwingine? Mwenye jibu hebu juza!! Hivi huyu Mukama na Makamba yupi afadhali ndani ya sisiemu!!!!!!
 
Sio bure....
Inawezekana matokeo tunayotazamia sisi sio matokea wanayotazamia wao
 
Wanafanya kudanganya wanadhani waTZ bado tunadanganyika kiivyo tutawaonyesha muda sio mrefu
 
Katibu mkuu wilson mkama amesema kamati hiyo yenye wajumbe 12 itakuwa na mamlaka ya kuchunguza na kuadhibu bila kuihusisha nec wala cc. Source TBC1 taarifa ya habari inayooendelea saa hiz.

Nawasilisha.
 
yote hiyo ni kumkwepa EL na mzee vijisenti!mara gamba,mara cc,mara kamati na sasa tume ya maadili. HAKUNA MWANA CCM MWENYE MAADILI HATA PUNJE!
 
wananchi tungefurahia kama mwenyekiti angekuwa wa kwanza kushuhulikiwa.
Hivi hii kamati ya watu 12 wakuchaguliwa inaweza kutenda haki?mukama hebu jaribu kuja na plan nyingine hii tumeshajuu mchawi ni nani anatafutwa
 
Hiyo kamati inaundwa na watu nje ya ccm? make ccm yote imechafuka. Mukama. mtu mzima hovyo!!!!!!!!!
 
Maadili ya CCM na yepi? Na hao wanakamati ni nani?


Wanakamati hawajatajwa mkuu,ila alivyokuwa anasistiza inaonekana walengwa ni wale watuhumiwa wa ufisadi maana karudia tena ile kauli ya kujipima na kujiondoa kwa wakiuka maadili kabla ya kuitwa mbele ya kamati
.
 
Kwanini waunde kamati mpya ya maadili wakati wanayo kamati yenye majukumu kama hayo? Hizi zote ni dalili za chama kuyumba kwasababu ya kutokuwa consistent in decision making!!
 
yote hiyo ni kumkwepa EL na mzee vijisenti!mara gamba,mara cc,mara kamati na sasa tume ya maadili. HAKUNA MWANA CCM MWENYE MAADILI HATA PUNJE!

Ndiyo bongolala..!Lengo ni kuyatoa majina makubwa kwenye mamlaka ya ulimi wa nape...!
 
Back
Top Bottom