Mukama asema mafisadi hawaponi ng'o! CCM yaunda kamati maalum

Kuna taarifa kwamba Mukama amekutana na waandishi leo na amerudia tena taarifa yake kuhusu magamba na kuapa kwamba hakuna fisadi aliyesafishwa Dodoma na badala yake magazeti yamekua yakipotosha kwa maslahi yao.
Usanii mtupu!
 
CCM bana, hivi wakikaa kimya wanapoteza nini kuliko kumwaga pumba ya mambo wasiyoweza kutekeleza? Wanaogopa nini na wana wasiwasi wa nini? Kiwango chao cha kushughulikia mambo ni kilekile, na bado wananchi wanawachagua sasa hii ogopa oigopa ya nini?

Hii inadhihirisha kuwa hawa jamaa wanaishi kwa wishful thinking juu ya mambo yaliyo ndani ya uwezo wao.
 
Ngoja tuone yatakayotokea. Ila naona wameamua kubadili mbinu maana ile ya kuitumia NEC inge backfire big time!!
 
Baada ya kikao cha Dodoma, katibu mkuu wa CCM bw. Wilson Mukama ameendeleza ngonjera kuwa mafisadi hawajasafishwa na kwamba watashughulikiwa. Nikiangalia ambavyo CCM imekuwa ikiwakumbatia mafisadi huku ikiendeleza kauli za kujivua gamba, inanifanya nikumbuke hadithi ya zamani ya "fisi na ngozi iliyokwamia shingoni"

Fisi alikuwa amealikwa kwa wakwe ambako alirimiwa ipasavyo. Alichinjiwa ngombe akala sawasawa. Kesho yake akifunga safari ya kurudi, kwa tamaa ya nyama aliomba apewe ngozi aende nayo. Alipofikiri namna ya kuibeba akatoboa tundu na kuingiza shingo yake na safari ikaanza. Ilipofika mchana kwa vile kulikuwa na jua kali, ngozi ikaanza kukauka na kumkaba koo. Hata hivyo kwa tamaa ya nyama hakutaka kuchomoa kichwa hata baada ya kuonywa na wasafiri wengine njiani. Matokeo yake ngozi ikazidi kukauka na kumkaba zaidi na hakuweza kutoa kichwa na hivyo akafa nayo.

Nionacho mimi ni CCM inayokufa na magamba yake yanayokaukia shingoni kwa vile hawataki kuchomoa kichwa na kuachana nayo. CCM wanajua vema wanavyofaidika na magamba (mafisadi) hayo. Hivyo kwa tamaa yao wanasubiria kifo ambacho ni dhahiri kutokea hata kabla ya uchaguzi wa 2015.
Kwa kifupi, kauli ya Mukama haina mshiko.
Nawasilisha
 
Huo ni mchezo wa kuigizwa,magamba yanatapatapa.Lakini wajue kwa kushindwa kuyavua magamba ndiyo sasa wamejipalia mkaa,ni lazima 2015 wang'oke.
 
So far najua ENL na kiungo wa katikati ( japo anafrustration za kunywan'ganywa uspika) wanataka hiyo siti ya mbele kabisa, hivi nani mwingine anataka?????
 
walikosa mabinti hadi wakawaweka wachina?

sera ya viongozi waliopo madarakani ni kuwapa tenda kubwa na ndogo watu wa nje kwa mawazo yangu labda siri ktk enda isitoke nje ,maanake ukimpa mtz kesho utaikuta jamvini yaani inauma halafu pinda ansema wtz ni wavivu

wakati serikali haina mpango wa kuwaendeleza wananchi wenzao ukisikia mikopo ya kilimo ujuwe wanzunguka wanchukuwa wenyewe
 
Kuna taarifa kwamba Mukama amekutana na waandishi leo na amerudia tena taarifa yake kuhusu magamba na kuapa kwamba hakuna fisadi aliyesafishwa Dodoma na badala yake magazeti yamekua yakipotosha kwa maslahi yao.

Mukama mnafiki mkubwa Mbona Fisadi '''MVI''' hakushughulikiwa hata kidogo?
Mbona Kuna mafisadi wengi tu lakini waliishia kumsimamisha katibu wa SISIEM Dsm?
Magamba hakuna kitu waongo wakubwa!
 
Kwa kweli amenishangaza huyu katibu wa ccm kwani anaposema ccm haijamsafisha mtu, kilichotokea kwenye nec ni EL kujisafisha mwenyewe kwani alipotoa hoja yake ya kuchafuliwa na wanaccm wenzake si ndio amejisafisha. Tuwe makini na watu kama lowasa:spy:
 
Baada ya kikao cha Dodoma, katibu mkuu wa CCM bw. Wilson Mukama ameendeleza ngonjera kuwa mafisadi hawajasafishwa na kwamba watashughulikiwa. Nikiangalia ambavyo CCM imekuwa ikiwakumbatia mafisadi huku ikiendeleza kauli za kujivua gamba, inanifanya nikumbuke hadithi ya zamani ya "fisi na ngozi iliyokwamia shingoni"

Fisi alikuwa amealikwa kwa wakwe ambako alirimiwa ipasavyo. Alichinjiwa ngombe akala sawasawa. Kesho yake akifunga safari ya kurudi, kwa tamaa ya nyama aliomba apewe ngozi aende nayo. Alipofikiri namna ya kuibeba akatoboa tundu na kuingiza shingo yake na safari ikaanza. Ilipofika mchana kwa vile kulikuwa na jua kali, ngozi ikaanza kukauka na kumkaba koo. Hata hivyo kwa tamaa ya nyama hakutaka kuchomoa kichwa hata baada ya kuonywa na wasafiri wengine njiani. Matokeo yake ngozi ikazidi kukauka na kumkaba zaidi na hakuweza kutoa kichwa na hivyo akafa nayo.

Nionacho mimi ni CCM inayokufa na magamba yake yanayokaukia shingoni kwa vile hawataki kuchomoa kichwa na kuachana nayo. CCM wanajua vema wanavyofaidika na magamba (mafisadi) hayo. Hivyo kwa tamaa yao wanasubiria kifo ambacho ni dhahiri kutokea hata kabla ya uchaguzi wa 2015.
Kwa kifupi, kauli ya Mukama haina mshiko.
Nawasilisha

WAKATI MWINGINE NAONA VIONGOZI WA MAGAMBA WANA AKILI YA KUKU! '' Wanasahau kauli zao haraka'''
Si muda mrefu walituambia Wanatoa Siku tisini Magamba ya jiondoe chamani....Zikapita Siku tisini hakuna kitu bali Gamba Moja Ambalo hata hivyo lilipomeguka ....Wakaliokota kule Igunga Wakitaka Kulibandika....Wakaliomba Angalau Liwasitiri Maana Pale lilipoondoka Kidonga kilibaki kikawa hakikauki....Basi Gamba Likakubali...Wakalipaka Rangi nyeupe nyeupe ili watu wasistukie Kuwa gamba limerudishwa.........""" HAO NDIO MAGAMBA WATATA"""
Mukama alikosa cha kuongea akaona ngoja na yeye ajitokeze kwenye vyombo vya habari walau Asipoteze umaarufu kisiasa!...........................................'''MAGAMBA KWISHNY 2015'''

NOTE BY......""" GAMBA MVII"""
 
hivi Nape yuko wapi?

Mkuu kuna thread humu ilisema alikimbia huko Dodoma. Huenda amekasimu madaraka yake kwa Katibu Mkuu! Unadhani kumvua gamba mtu mchezo, unaweza kusababisha tetemeko la ardhi na kimbunga kikakuchukua mvuaji!
 
hivi Nape yuko wapi?
Wanasemaga, NAPE na SITA wamezila na hata mkutanoni walitoka JK aliposema waliomtamka vibaya EL watashughulikiwa, kama CCM wanabisha waseme kwanini sasa Mukama ndiyo amekuwa Katibu Mwenezi wa CCM??????????
 
mafisadi ni wale mawaziri tisa aliowataja Zitoi Kabwe kuwania Urais, Urais ni hela wao wanazipata wapi mapema hii, ndio hawa wanaouza wanyama pori hai, ndio hawa wanaotengeneza hela feki, ndio hawa wanamtandao wa madwa ya kulevya, ndio hawa wadini
 
Jamani uswahiba huu wa JK na washirika wake unaimaliza nchi, nadhani wote walio maswahiba wake nao waorodheshwe na kuunganishwas kwenye kesi za mafisadi,hii itamsaidia JK kuachana nao.
 
Wataunda kamati, bodi nk lakini hakuna gamba litakalovuliwa. Labda waanze kuvionea vidagaa lakini kwa manyangumi ni hadithi tu hata Mukama wakati anaongea moyoni analitambua hilo.
 
CCM ni sawa na mti mkubwa uliioteshwa siku nyingi kukiwa na matumaini ya matunda yake kuwa na vitamini kwa Watanzania, imekuja kugundulika kwamba matunda yake, mizizi, matawi na hata magamba yake ni sumu tena mbaya. Kilichobakia hapa ni kuufyekea chini huu mti, vinginevyo sisi na watoto wetu tutaendelea kula matunda ya huu mti mmbaya na tutaendelea kufa.

Sasa hapa Mukama akiwa juu ya huu mti alitudanganya kwamba watautoa magamba ili uwe mti mzuri, baadaye wakagundua wakitoa magamba mti unakufa. Sasa wamegeuza na wanatudanganya kwamba huo mti utakuwa mzuri iwapo watatoa baadhi ya matawi, huu ni uongo mkubwa maana mti wote una sumu. Pia Mukama hawezi kuukata mti maana yupo juu, akiukata na yeye anapiga chini.
 
Back
Top Bottom