Luteni
JF-Expert Member
- Jan 9, 2010
- 2,274
- 302
Inasemekana kuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Willison Mukama anafanya kampeni ya kuzifanya kamati nyeti za bunge zinazoshikiliwa na wapinzani ziongozwe na wabunge wa CCM.
CCM ina wabunge wengi wasomi na wenye uwezo mkubwa sana kuliko hata wengine. Tunataka chama hiki kiwe wazi zaidi na kuisimamia karibu zaidi Serikali, sasa mimi nashangaa pamoja na kuwa na wabunge wengi hao kamati muhimu wanawapa wapinzani,.
Kauli ya Mrema:
Mwenyekiti wa Kamati Hesabu za Serikali za Mitaa, Augustine Mrema, amesema kampeni inayofanywa na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Willison Mukama, ya kutaka kuwangoa wapinzani katika kamati nyeti za Bunge, haina tija, alisema kamati hizo duniani kote zimekuwa zikiongozwa na vyama vya upinzani wala si chama tawala.
Mukama ajue hizi kamati zinaitwa over sight committee zinaongozwa na wapinzani na wala si chama tawala", alisema kisimgi, hata kama CCM wana wasomi lukuki ndani ya CCM hawaruhusiwi kuongoza kamati hizo.
Kauli ya Zitto:
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma, Zitto Kabwe, alisema utaratibu huo wa kuchagua viongozi kutoka kambi ya upinzani unatumika katika nchi za Jumuiya Madola, aliongeza kuwa Mukama hajui kuwa ni utaratibu uliowekwa kikanuni. Alisema kuuondoa utaratibu huo ni kurudi nyuma kwa sababu chama chenye serikali hakiwezi kujikagua chenyewe, Kamati hizi lazima zitazamwe na watu wengine,.
Kauli ya Kaimu Katibu wa Bunge
Kaimu Katibu wa Bunge, John Joel, alisema utaratibu wa kuunda na kuchagua viongozi wa kamati hizo unatokana na kanuni za Bunge. Kwa mujibu wa Kanuni za Bunge, kifungu cha 113(11), wenyeviti wa kamati za bunge zinazosimamia matumizi ya fedha za umma ambazo ni Kamati ya Hesabu za Serikali kuu, Kamati za Hesabu za serikali za mitaa na Hesabu za Mashirika ya Umma, watachaguliwa miongoni mwa wajumbe ambao wanatoka katika kambi ya upinzani Bungeni.
My take: Hii kampeni mpya ya Mukama ina tija gani kwa taifa.