Mukama anataka kamati nyeti ziongozwe na CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mukama anataka kamati nyeti ziongozwe na CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Luteni, Jun 27, 2011.

 1. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #1
  Jun 27, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Inasemekana kuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Willison Mukama anafanya kampeni ya kuzifanya kamati nyeti za bunge zinazoshikiliwa na wapinzani ziongozwe na wabunge wa CCM.

  “CCM ina wabunge wengi wasomi na wenye uwezo mkubwa sana kuliko hata wengine. Tunataka chama hiki kiwe wazi zaidi na kuisimamia karibu zaidi Serikali, sasa mimi nashangaa pamoja na kuwa na wabunge wengi hao kamati muhimu wanawapa wapinzani,”.

  Kauli ya Mrema:

  Mwenyekiti wa Kamati Hesabu za Serikali za Mitaa, Augustine Mrema, amesema kampeni inayofanywa na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Willison Mukama, ya kutaka kuwang’oa wapinzani katika kamati nyeti za Bunge, haina tija, alisema kamati hizo duniani kote zimekuwa zikiongozwa na vyama vya upinzani wala si chama tawala.

  “Mukama ajue hizi kamati zinaitwa over sight committee zinaongozwa na wapinzani na wala si chama tawala", alisema kisimgi, hata kama CCM wana wasomi lukuki ndani ya CCM hawaruhusiwi kuongoza kamati hizo.

  Kauli ya Zitto:

  Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma, Zitto Kabwe, alisema utaratibu huo wa kuchagua viongozi kutoka kambi ya upinzani unatumika katika nchi za Jumuiya Madola, aliongeza kuwa Mukama hajui kuwa ni utaratibu uliowekwa kikanuni. Alisema kuuondoa utaratibu huo ni kurudi nyuma kwa sababu chama chenye serikali hakiwezi kujikagua chenyewe, “Kamati hizi lazima zitazamwe na watu wengine,”.

  Kauli ya Kaimu Katibu wa Bunge

  Kaimu Katibu wa Bunge, John Joel, alisema utaratibu wa kuunda na kuchagua viongozi wa kamati hizo unatokana na kanuni za Bunge. Kwa mujibu wa Kanuni za Bunge, kifungu cha 113(11), wenyeviti wa kamati za bunge zinazosimamia matumizi ya fedha za umma ambazo ni Kamati ya Hesabu za Serikali kuu, Kamati za Hesabu za serikali za mitaa na Hesabu za Mashirika ya Umma, watachaguliwa miongoni mwa wajumbe ambao wanatoka katika kambi ya upinzani Bungeni.

  My take: Hii kampeni mpya ya Mukama ina tija gani kwa taifa.
   
 2. HISIA KALI

  HISIA KALI JF-Expert Member

  #2
  Jun 27, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 694
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ana nia nzuri tu ya kuficha madhambi ya serikali ya chama chake.
   
 3. Saharavoice

  Saharavoice JF-Expert Member

  #3
  Jun 27, 2011
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 2,644
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Mukama ni gamba gumu kuliko Makamba, time will tell
   
 4. Mawenzi

  Mawenzi JF-Expert Member

  #4
  Jun 27, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,261
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Jamani leo vp???? Mbona threads nyingi sana hazina sources???
   
 5. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #5
  Jun 27, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Home
   
 6. F

  FJM JF-Expert Member

  #6
  Jun 27, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Kama ni kweli Mukama anataka kufanya hivi basi CCM wakawa wanajikaanga kwa mafuta yao wenyewe. Ni hivi: Kamati zote zikiongozwa na chama Tawala ni wazi kuwa serikali itaweza kupitisha mambo mengi including miswaada yenye mapungufu kama ule wa mchakato wa katiba mpya. Na kwa sababu ndani ya bunge wabunge wa ccm ni wengi hakuna shaka hata kidogo serikali itapata ahueni. On the face of it Mukama anaweza akafikri kuwa hii itailtea umaarufu ccm. But the opposite is true.

  Kwanza, wapinzani watapata 'massive capital politically' kwa kusema kuwa ccm inatumia wingi wake kwenye chombo cha kutunga sheria yaani bunge kuziba jicho la kumulika uboronganji ndani ya serikali. Hivyo watasema (wapinzani) kuongozwa kwa hizi kamati nyeti na chama tawala ni kielelezo tosha kuwa wabunge wa ccm wapo kwa maslahi ya watu wachache ni sio watanzania wengi. (hii judge & jury approach on its own is enough to plummet ccm reputation even lower).

  CCM wanatakiwa wakubali kitu kimoja tu kwamba statistically, ndani ya bunge wana wafuasi wengi kwa maana ya wabunge wa ccm ni wengi. Lakini kwenye 'bunge la mtaani' yaani huku uraiani CHADEMA bila shaka wana wafuasi wengi zaidi, na kwa kadri siku zinavyokwenda bunge la mtaani linaonekana kuimarika na wafuasi wanakuwa wengi kuliko hata matarajio ya awali. Na ndio maana hata wakati mwingine serikali inaonekana kufuata ajenda za CHADEMA maana wanajuwa 'bunge la mtaani' halikubali vingenevyo e.g katiba mpya.

  Na hapa ndipo linakuja jambo la pili, ambalo ni muhimu zaidi kwa ccm kulitambua. Chini ya huu mfumo wa chama kushika hatamu toka kwa Mukama mambo mengi yatakayopitishwa bungeni yakiwemo bajeti, miswada ya sheria n.k yatakosa 'ownership' toka kwa wananchi ambao ni bunge la juu zaidi (upper house) na hivyo kutokuwa na 'legitimacy' kwa sababu tayari ccm na serikali yake watakuwa wamebambikizia hii reputation ya kuwa wapo kwa 'maslahi ya wachache'. Hivi ccm wanaweza kuwa mufilisi wa strategies kiasi hiki?

  Political suicide if you ask me!
   
 7. m

  mzee wa njaa JF-Expert Member

  #7
  Jun 27, 2011
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 1,368
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkama ana kichaa huyo we unajua hilo leo?
   
 8. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #8
  Jun 27, 2011
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Hivi Mukama ana wadhifa upi katika serikali na bunge zaidi ya kuwa Katibu Mkuu wa ccm? Nionavyo mimi hayo ni mawazo yake na hawezi kubadili utaratibu/kanuni zilizowekwa na bunge. Yeye ni katibu mkuu kama makatibu wakuu wengine wa vyama vingine, tofauti tu ni kuwa chama chake kinaongoza serikali kwa sasa.
   
 9. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #9
  Jun 27, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Ndo ameanza kazi.......taratibu atashika kasi kama MA-ROPE
   
 10. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #10
  Jun 27, 2011
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Utoke huko arudi kushughulikia magamaba, siku 90 alianza kuhesabu lini?
   
 11. Mwana va Mutwa

  Mwana va Mutwa JF-Expert Member

  #11
  Jun 27, 2011
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 429
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  kuna njia nyepesi sana kama anazitamani hizo kamati,
  kwakuwa zinashikwa na wapinzani,
  na kwakuwa ccm sasa si wapinzani,
  nashauri aboronge kwenye uchaguzi ujao,ccm kiwe cha upinzani,watashika hizo nafasi, smple like that
   
 12. h

  hans79 JF-Expert Member

  #12
  Jun 27, 2011
  Joined: May 4, 2011
  Messages: 3,802
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 145
  anajianda kugombea ubunge
   
Loading...