Mukama ameikejeli Katiba!

Jibu hoja acha bla bla ! sio ya kweli hayo

Huyo mzee mkama anakulipa sh ngapi wewe? Halafu siasa mbaya kweli jamani, I used to think huyu mzee alikuwa smart lakini toka apewe kiti cha makamba nazidi kugundua kuwa hamnazo pia. Jana kaboa kweli kwenye taarifa ya habari, mshaurini asiwe anaweka mifano mingi ya kisayansi maana anazidi kulikoroga maskini. Ushauri mwingine labda unaweza kusaidia ni kuwa asitumie vitu alivyokuwa akitumia makamba kama meza, kiti n.k huenda ikasadia kdg otherwise tutakuwa tumebadlilishiwa mwimbaji tu taarabu zile zile.
 

Mtei alitofautiana na mwalimu kw usaliti wake ! si unajua tena wenzetu wa kaskazini pesa mbele mzee, maslahi ya wananchi baadae
 
Elewa maana ya kuanzishwa ilivyo andikwa kwenye thread yenyewe. Na hili liko wazi IMF ndio walioanzisha vyama vingi kwa shinikizo zao
Nikinukuu maelezo yako............... ............."Na hili liko wazi IMF ndio walioanzisha vyama vingi kwa shinikizo zao"............... mwisho wa kunukuu. ...................... Unasemaje kuhusu uwepo wa
1. CUF,
2. UDP
3. NCCR Mageuzi
4. etc........etc.............

Navyo vimeletwa na IMF .........???

Fafanua yafuatayo...............

1. Ungetubandikia ushahidi unaoonyesha kuwa CDM inafadhiliwa na watu wa nje............
2. Unasemaje juu ya BIBI TITI kukorofidhana na muasisi wa taifa hili............
 

Kwasababu unao ukweli nawe ni mwana jamvi umwage hapa tuudadavue, ila niijuavyo IMF hakuna shule bure, matibabu bure, makampuni makubwa kulipishwa kodi zote bila misamaha (Barick na wenzake) lakini kwa CDM hayo ndio ya msingi sasa sijui wanakula vipi meza moja na IMF.. Mhhh ipo kazi .. ngoja tuupate huo ushahidi ulionao
 
Na huu ufadhili wa maandamano kumbe pesa mwapata IMF , tunashukuru kwa kutujuza hivyo

For sure hapa sio mahala pako, nafikiri kwenye kijiwe cha kahawa ndo unakostahi. Unataka watu wachangie hoja isio na ushahidi..umechoka kufikiri.
 
Kama wamemuandika habari leo labda bado kivuli chake kinawatisha si ndo alikuwa (sijui sasa) mwenyekiti wa bodi ya magazeti ya serikali (TSN) kabla ya kukwapua kitumbua cha Mak/gamba.
 


KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilson Mukama, akifafanua jambo alipozungumza na wahariri wa vyombo vya habari wakati wa hafla ya chakula cha mchana alichowaandalia Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye. Kulia ni Katibu wa NEC, Uchumi na Fedha, Mwigulu Nchemba. (Na Mpigapicha Wetu).

Imeandikwa na Mwandishi Wetu - Habari Leo; Tarehe: 3rd May 2011

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilson Mukama amesema kinachofanyika sasa katika chama hicho ni mageuzi makubwa ya kukisafisha na kwamba si ajali.

Mukama amesisitiza kwamba, CCM itaendelea kupambana na ufisadi.

Amebeza kauli za baadhi ya wanasiasa hasa wa upinzani kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kitakufa, akisema "Chadema itakufa mara mia, CCM itabaki."

Mukama amewaambia watendaji na wahariri wa vyombo vya habari Dar es Salaam kuwa ilichofanya hivi karibuni CCM ni mabadiliko yenye utashi na si ajali, kwa maelekezo ya Mwenyekiti wa Taifa, Rais Jakaya Kikwete, ya haja ya kuwapo kwa mageuzi katika chama hicho tawala.

"Kilichofanyika ni kwa utashi, siyo ajali. Ulifanyika uchambuzi uliojengwa katika misingi ya kukifanya chama kiendelee kuongoza," alisema Mukama jana katika mkutano wake huo wa kwanza mkubwa na vyombo vya habari tangu ashike wadhifa huo mapema Aprili.

Alisema, vikao vya chama hicho havikukurupuka kufanya maamuzi ikiwemo kujiuzulu kwa Kamati Kuu na Sekretarieti, bali vilifanya hivyo kwa nia ya kuruhusu mageuzi hayo ambayo alisema maamuzi magumu zaidi yatarajiwe kuelekea mageuzi hayo.

"Tuko kwa utashi, msingi wa mabadiliko ni lazima uwe ndani ya chama chenyewe. Na mageuzi haya yana lengo la kukisafisha chama, siyo kukiua," alifafanua kada huyo wa miaka mingi katika CCM.

Alisema, kama kuna watu wanatilia shaka mageuzi hayo yaliyoendana na dhana ya kujivua gamba, wasubiri waone nini kitafanywa na chama hicho, kwa sababu kina dhamira ya dhati ya mageuzi hayo.

"Tuacheni, tupeni nafasi, subirini….kweli hili hatutafanya ajizi, alieleza Mukama na kuongeza:

"CCM imejivua gamba kwa kujaza safu upya za uongozi wake ndani ya Kamati Kuu na Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa. Hii ni hatua ya mwanzo katika mchakato wa mageuzi makubwa ndani ya chama."

Alisema, lengo la hatua hiyo ya mwanzo ni kupata viongozi wenye mtazamano, msimamo na vitendo vinavyooana na mwelekeo wa mageuzi yanayotarajiwa kufanywa na CCM.

"Ni kwa sababu hiyo CCM katika mchakato wake wa kufanya mageuzi makubwa imeanza na suala la aina ya viongozi wa kufanikisha mchakato huo," alieleza.

Mbali na Mukama, Sekretarieti mpya inaundwa na Naibu Katibu Mkuu Bara, John Chiligati, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Ali Vuai Ali, Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, Katibu wa Uchumi na Fedha, Mwigulu Nchemba, Katibu wa Oganaizesheni na Mipango Asha Abdallah Juma na Katibu wa Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, January Makamba.

Nape, Nchemba na Makamba walihudhuria katika mkutano huo wa jana na wanahabari ambao Mukama alisema ni muhimu kwa sababu CCM kama taasisi ya kisiasa na taasisi za vyombo vya habari, wote wana nafasi muhimu katika ujenzi wa mustakabali wa nchi.

Akizungumzia vita dhidi ya ufisadi, Mukama alisema, Chama Cha Mapinduzi kitaendeleza mapambano dhidi ya tatizo hilo na kwamba itachukua hatua stahili kwa wanachama wake wanaotuhumiwa kwa ufisadi kwa kufuata taratibu za maadili za chama hicho.

"Tutaendeleza mapambano dhidi ya ufisadi, na hilo limeelezwa vyema katika azimio letu la 15 la NEC mjini Dodoma, likiwataka wanachama wote wanaotuhumiwa kwa ufisadi watafakari, wapime na wachukue hatua dhidi ya tuhuma hizo.

"Lakini pia Mwenyekiti wa Taifa katika kufunga mkutano wa NEC alieleza kuwa chama hakitakuwa na ajizi katika kupambana na ufisadi na kuwataka wanachama hao wanaotuhumiwa kwa ufisadi watafakari, wapime na wachukue hatua wenyewe, lakini kama hawatafanya hivyo, chama kitawawajibisha," alieleza Mukama.

Alifafanua zaidi suala hilo la ufisadi kwa baadhi ya wanachama wao baada ya kuulizwa kuwa haoni kwa nini watuhumiwa wasipelekwe kwenye vyombo kama Takukuru, alisema wanachofanya wanachama hao ni kuwajibika kisiasa kama taratibu za chama zilivyo.

Aidha, alisema kwa rekodi zilizopo hakuna mahali ambako CCM ilieleza kuwa watuhumiwa hao wa ufisadi wamepewa siku 90 wajipime wenyewe, kama chama hicho hakifanya maamuzi juu yao.

"Hizi siku 90 sijui zimetoka wapi…rekodi ni hizo nilizowasomea (azimio la 15 na hotuba ya Mwenyekiti ya kufunga kikao cha NEC). Na kawaida NEC inakutana baada ya miezi minne, sasa siku 90 za wapi," Alihoji Mukama.

Akijibu hoja kuwa CCM inakufa, Mukama alisema chama hicho ni taasisi iliyojengwa kwa misingi imara na yenye utajiri na rasilimali, hivyo haoni kifo chake.

"Chadema itakufa mara mia, lakini CCM haiwezi kufa, imejengwa kwa misingi imara," alieleza Mukama.

Kwa upande wake, Nape alisisitiza kuwa usafi wa wanachama wa chama hicho hauwezi kupangiwa na mtu na kusisitiza kuwa "CCM ni taasisi kubwa. Chadema ni fotokopi tu."
 
Hakuna ubaya wa kuanzishwa kwa shinikizo ili mradi ni shinikizo la kuwakomboa wananchi walalahoi ambao CCM imewafanya watumwa ndani ya ardhi ya mababu zao. Mashinikizo mengine ni muhimu sana, Angalia shinikizo la kumng'oa Gbagbo wa Ivory Cost lilivyokuwa zuri. Hata CCM hawana tofauti na Gbagbo, ni lazima ang'olewe madarakani ili watu wa Tanzania wapate mtawala anayewajali. Mimi siku natamani nihame Tz lakini hata nikihama watoto wangu na ndugu zangu watabaki TZ na hivyo ni bora niungane tu wapambanaji wa ukweli ili tuiokoe nchi yetu kutoka kwa nduli mwingine (CCM).
 
CDM itazidi kusonga mbele mtajitahdi kugundua mbinu za kukidhoofisha lakini mtaishia kupewa majibu na ma great thinkers.

Na ww umo kwani ? mbona tuliomo humu hatuzidi 5, na jina lako halipo
 
Nilifikiri baada ya kuondoka makamba basi ngojera na taarabu zitakwisha kumbe na huyu naye bado tu? Kweli kobe hawezi kuvua gamba lake!
Hivi akilivua bado utamwita kobe au marehemu kobe? CCM watawezaje kuvua gamba? Wakivua tu ujue hakuna atakayebakia kwenye chama na hicyo kitakufa automatically. Wao wasubiri tu wananchi watakapoliponda nyundo gamba lao lisambaratike kabisa.
 
Na ww umo kwani ? mbona tuliomo humu hatuzidi 5, na jina lako halipo
Uwiiiiiiiiiiiii! Kumbe siku hizi Great Thinkers wamekuwa akina yakhe, wewe nawe ni Great thinker? mimi kuanzia leo nimejiondoa kwenye kundi hilo maana limevamiwa na popo
 

mod haya sio matusi
uitampaje mgongo ama kiswahli kigumu??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…