Muingiliano wa mawazo ya kufikirika

Muingiliano wa mawazo ya kufikirika

Mkuu Mshana kuna kitu umekigusia kwa umbali sana lakini nafikri kinahitaji mjadala wake kabisa.

Nini nguvu ya mawazo chanya katika kumlinda mtu na wanga wa dunia hii??

Kwamba mtu mwenye mawazo chanya kuna uwezekano huwa anajijengea kaukuta fulani hivi kakiroho kanakomuwezesha kumkinga na watu wabaya wa dunia hii??
 
Umeiona reply ya Baba rai? Very very touching indeed
nimesoma asee. jamaa amegusa mule mule. ila kwa ulimwengu tulio nao sasa ulimwengu wa utandawazi na uhuru binafsi ninawaona binadamu wakienda mbali zaidi ya hapa. Asilimia kubwa ya wanadamu itazidi kuwa ya kuwaza mambo ya dunia kuliko Mungu kwasababu
1. ya ugumu wa maisha unavyozidi...kila ukiamka kuna jipya mara sukari imepanda, mara umetumbuliwa so hata muda na rasilimali za kusaidia yatima na wajane havipo. mara hakuna myanya ya udokoaji hivyo na vibaka wenye kuwaza mawazo ya wizi wanazidi na wengine kujikita zaidi kwenye utafutaji,
2. kukua kwa teknolojia (mfano kabla ya hizi social media ilikuwa mtu hana wa kujilinganisha naye lakini sasa hivi unaingia facebook IG unaona uliyemfolo yuko vaccation zanzibar, amevaa kichupi, anapiga shisha n.k n.k hivyo wengine wakitoka hapo nao wanaenda kuwaiga hao kwa kuona kama vile wao wako nyuma ya wakati. 3. unabii unatimia...ilitabiriwa siku za mwisho watu watajipenda wenyewe, hawatajali wenzao, hawatampenda Mungu, na mengine meeengi.
Na hapo watakapojikita ndani zaidi kwenye kuhangaika na ya dunia ndipoyule mwenye mamlaka na dunia hii atakaposema IMEKWISHAAAAAA na hapo ndipo utakumbuka hata usiome biblia , usaidie wenye shida, na mengineyo lakini hayatakuwa na maana tena.
 
Mkuu Mshana kuna kitu umekigusia kwa umbali sana lakini nafikri kinahitaji mjadala wake kabisa.

Nini nguvu ya mawazo chanya katika kumlinda mtu na wanga wa dunia hii??

Kwamba mtu mwenye mawazo chanya kuna uwezekano huwa anajijengea kaukuta fulani hivi kakiroho kanakomuwezesha kumkinga na watu wabaya wa dunia hii??
Ni kweli kabisa asigwa nipe muda kwenye hili ili tuweze kupata full version kitu kizima kilichoshiba
 
Ni kweli kabisa asigwa nipe muda kwenye hili ili tuweze kupata full version kitu kizima kilichoshiba
Ok mkuu nitashukuru sana aisee.

Usisahau kunitag nisije nikapitwa na hiyo kitu, maana JF ya siku hizi nyuzi nyingi mno, unaweza kupitwa na mjadala mzuri bila kujijua.
 
Ok mkuu nitashukuru sana aisee.

Usisahau kunitag nisije nikapitwa na hiyo kitu, maana JF ya siku hizi nyuzi nyingi mno, unaweza kupitwa na mjadala mzuri bila kujijua.
Pouwa
 
Kwanza nakupongeza kwa maada yako nzuri, pili nawapongeza wachangiaji wote humu, nimejifunza ati.

Hizo picha mbili juu hapo, zimenipa tafsiri ya mambo mengi sana, tena sana.

Ningependa kujua, hivi kuwa na mawazo hasi, mfano kuwaza kwenda beach, kuwaza kuwa na pesa nyingi, kuwaza mechi fulani hivi zilizopita iwe mpira ama michezo mengine kama ngumi, n.k n.k. Je ni dhambi? Kama ndiyo ni kwa muktadha upi!

Ahsante!
 
Binafsi huwa najisemea, laiti Mungu, huyu angetupa vitu vitatu vikubwa vikafanya kazi ndani yetu, hakika labda peponi tungeenda wote ama motoni tungeenda wote. Vitu hivyo ni MACHO YA KIROHO, KUTOKUSAHAU, VISASI / KUTOKUSAMEHE. Japo wapo walio navyo hivyo juu hapo, ila wengi wetu hatuna na labda tunahangaika kuvitafuta.

MACHO YA KIROHO, tungefahamu kabla mleta maada hajaleta mchanganuo wake humu, labda tungemuwahi asiulete ama tungemjibu humu kwa kumueleza ukweli, mbona nawe upo vile na hivi.

KUTOKUSAHAU, kuna matukio mengi sana yametokea na yanaendelea kutokea maishani mwetu, laiti tusingeumbiwa kusahau, hakika tungeuwana sana na hata kufa wenyewe endapo waliotusababishia maumivu hatuwawezi kwa namna yoyote ile.

VISASI / KUTOKUSAMEHE, hakika kwa haya, tumshukuru Mungu, sana maana ametuumbia kutua mizigo yetu na kusamehe, vikichagizwa na mafundisho yake tokea ktk vitabu vyake vitakatifu. Maana binafsi narudia tena binafsi, dhambi zitzkazotupeleka Jehanamu, wala siyo hizi pendwa kama uasherati sijui na uzinzi, hizo huwa naziona ni nyepesi tu, ila hii ya KUTOKUSAMEHE kwa maana ya VISASI, wengi tutaangamia nazo.

Naweza kama nisieleweke na mkahisi nimetoka nje ya maada, hapana ila ukinisoma vema utaelewa na utajua tu bado nipo ndani ya maada.

Ahsante!
 
Unajua binadamu siku zote tumeumbiwa kupenda na kutamanai yaliyo mazuri, na bahati nzuri mchangiaji mmoja hapo alieleza ya kuwa, mwisho wa nyakati, watu watapenda ya kuupendezesha mwili, kujipamba, n.k. Na bahati nzuri nyengine, hata mleta maada ameeleza hapo juu ya kuwa, hata viongozi wa dini mawazo hasi yanawatawala sana. Na huo ni ubinadamu.

Unajua mawazo hasi ni kutojiamini kimwili, kiakili (fikra), na kiroho. Ndiyo maana kuna mifano mingi ndani ya Biblia, watu walipenda kuona miujiza tu, isipofanyika wanadai ya kuwa Mungu, hayupo. Hata wale wanafunzi wake Yesu, baada ya Yesu kuuwawa walitawanyika na kurudi katika shughuli zao wakijisahau ya kuwa wapo walioambiwa watawavua watu, na huo ni ubinadamu hakuna wa kuwalaumu.

Kuna mahala kwenye Biblia, Yaani siku chache baada ya Yesu, kulisha maelfu ya watu, bado wanafunzi wake walikuwa na mawazo yale yale ya kibinadamu, wanaulizana na kulaumiana mbona hawakuchuka mikate na wapo safarini tena kwa njia ya maji, Yesu, yeye akawa akiwafundisha ila wao wanawaza kula na kulaumiana, Marko 8:14-21 narudia tena na huo ni ubinadamu.

Mkuu wa anga hili, tangu asababishe wanadamu wa awali kuitenda dhambi ya asili, anatusumbua sana hadi leo hii, Hawa na Adamu, walitaka vitu vizuri, kufanana na Mungu, na huo ni ubinadamu.

Ila kwa kumuamini Mungu, pekee yote hayo maovu na maasi, tutayashinda hakika. Mazingira ndiyo yanatusababishia tuwe na mawazo hasi, ila daima tuyafuate mausia na mafundisho ya Mungu.

Ahsante!
 
Kwanza nakupongeza kwa maada yako nzuri, pili nawapongeza wachangiaji wote humu, nimejifunza ati.

Hizo picha mbili juu hapo, zimenipa tafsiri ya mambo mengi sana, tena sana.

Ningependa kujua, hivi kuwa na mawazo hasi, mfano kuwaza kwenda beach, kuwaza kuwa na pesa nyingi, kuwaza mechi fulani hivi zilizopita iwe mpira ama michezo mengine kama ngumi, n.k n.k. Je ni dhambi? Kama ndiyo ni kwa muktadha upi!

Ahsante!
Hizo si dhambi bali ni matendo ya kufurahisha mwili uozao mwili wenye kutamani kila kitu kizuri
 
Binafsi huwa najisemea, laiti Mungu, huyu angetupa vitu vitatu vikubwa vikafanya kazi ndani yetu, hakika labda peponi tungeenda wote ama motoni tungeenda wote. Vitu hivyo ni MACHO YA KIROHO, KUTOKUSAHAU, VISASI / KUTOKUSAMEHE. Japo wapo walio navyo hivyo juu hapo, ila wengi wetu hatuna na labda tunahangaika kuvitafuta.

MACHO YA KIROHO, tungefahamu kabla mleta maada hajaleta mchanganuo wake humu, labda tungemuwahi asiulete ama tungemjibu humu kwa kumueleza ukweli, mbona nawe upo vile na hivi.

KUTOKUSAHAU, kuna matukio mengi sana yametokea na yanaendelea kutokea maishani mwetu, laiti tusingeumbiwa kusahau, hakika tungeuwana sana na hata kufa wenyewe endapo waliotusababishia maumivu hatuwawezi kwa namna yoyote ile.

VISASI / KUTOKUSAMEHE, hakika kwa haya, tumshukuru Mungu, sana maana ametuumbia kutua mizigo yetu na kusamehe, vikichagizwa na mafundisho yake tokea ktk vitabu vyake vitakatifu. Maana binafsi narudia tena binafsi, dhambi zitzkazotupeleka Jehanamu, wala siyo hizi pendwa kama uasherati sijui na uzinzi, hizo huwa naziona ni nyepesi tu, ila hii ya KUTOKUSAMEHE kwa maana ya VISASI, wengi tutaangamia nazo.

Naweza kama nisieleweke na mkahisi nimetoka nje ya maada, hapana ila ukinisoma vema utaelewa na utajua tu bado nipo ndani ya maada.

Ahsante!
Mimi nakuelewa vizuri sana..kwanza ni muhimu kupata tafsiri sahihi ya dhambi
Dhambi ni jambo la kiimani , nje ya hapo hakuna dhambi
Lakini vile vile dhambi ni matendo yote ya kuwaza kunena na kutenda yenye madhara kwako na kwa wengine...nje ya hapo hakuna dhambi
 
Yaan usile nyama ukianza kupratice meditation je naweza kuja kula tena kwa baadaye au ivyo vitu vya kutokula moja kwa moja n.k kwann embu nipe sababu
 
Yaan usile nyama ukianza kupratice meditation je naweza kuja kula tena kwa baadaye au ivyo vitu vya kutokula moja kwa moja n.k kwann embu nipe sababu
Nyama ukishaacha acha kula na ukazoea hiyo hali ni vigumu mno kuirudia si kwamba kuna masharti la hasha lakini kule kuiona tu utajisikia vibaya
Vile vile nyama inaleta hasira kuongeza uzito na kukamaza misuli
 
Nyama tamu asee mi vigezo vingine sawa lakin nyama[emoji24] [emoji24] [emoji24]
 
Sex naweza kuicontrol vizuri, kula kwa muda sawa [emoji2] [emoji2] [emoji2]
 
Back
Top Bottom