Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 280,550
- 729,429
Mwanadamu hutumia muda mchache sana kuwaza jinsi atakavyokwenda kwenye nyumba ya ibada na kumuomba Mola wake kwa roho na kwa kweli huku akitoa zaka na kuwasamehe waliomkosea huku akipanga kuwasaidia wenye shida mbalimbali za kiroho na za kimwili pia...kuwatembelea wagonjwa hospitalini na wafungwa gerezani bila kuwasahau yatima na watoto wa mitaani...hapa fikra zetu ni asilimia kumi tu
Mawazo yetu yamejikita kwenye mambo mabaya mambo machafu mambo ya kutisha visasi na starehe
-unapishana na binti, ushaona mbele halafu unataka kuona na nyuma, kishapo unajenga taswira ya ajabu kabisa nafsini mwako unamvua nguo zote na kumwacha uchi kabisa
-umeudhiwa na mtu kagusa hisia zako kwa nguvu hasi, amekuumiza unajenga taswira ya kufikirika ukipanga jinsi utakavyomuumiza na wewe! Kumuonyesha kwamba wewe ni kiboko na huchezewi....unajiapiza kumkomesha
- Nafsi pweke ni karakana ya shetani, uko pekeyako mahali unawaza jinsi utakavyopata hela nyingi za fasta bila kutoka jasho na jinsi utakavyotumbua starehe na kwenda viwanja vikali na watoto wakali huku ukiwa na usafiri wa nguvu nguo za gharama na vipodozi pia...unajenga picha nyiingi za kufikirika nafsini mwako
Cha kushangaza na cha kusikitisha mawazo haya mabaya hayana kikao yatapishana kama picha ndefu ya sinema za kihindi
Nafsi na ufahamu wa binadamu vina pande mbili hasi na chanya....hasi ina nguvu kwenye kutamba na kuwaza vitu vibaya na vya kufikirika hapa huchukua 90% ya mawazo yote LAKINI chanya ina nguvu kwenye kutoa maamuzi kwenye mambo mengi yaliyofikiriwa na kupangwa na hasi
Laiti kama mawazo yale ya nguvu hasi iliyopo nafsini mwetu yangeachwa tu mpaka kwenye matendo naamini dunia ingekuwa jehanam ya pili
Maisha yetu yamejazwa na makwazo kuanzia majumbani mitaani makazini mpaka kwenye mitandao ya kijamii. ..wengi waliokufa walioko mahospitalini na hata wafungwa magerezani ni matokeo ya nguvu chanya kushindwa kudhibiti mawazo mabaya ya kufikirika ya nguvu hasi ambayo yakikuja kutafsiriwa kwa vitendo na majanga yakayokea
Ulalapo kitandani mwako usiku huu...jitahidi kubadili mtazamo wako sasa yafukuzie mbali mawazo hasi na yakaribishe mawazo chanya..kwa kufanya hivyo hata ndoto za majinamizi hazitakuandama na wanga watakugwaya