Uchaguzi 2020 Muhsein Awadhi Said (Dkt. Cheni) achukua fomu ya kuwania Ubunge Ilala kupitia CCM

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,814
4,547
Muhsein Awadhi Said (Dkt. Cheni) Muigizaji Mkongwe na Mshereheshaji maarufu amechukua fomu ya kuwania Ubunge katika Jimbo la Ilala kupitia Chama cha Mapinduzi.

Baada ya zoezi la kuchukua fomu hiyo Dkt. Cheni aliongea kwa kifupi na Waandshi wa habari kuwa yeye ni mzaliwa wa Ilala kwa sasa amechukua fomu akiwa na nia ya kugombea Ubunge kwenye jimbo hilo lakini mambo mengine zaidi atayazungumza wakati sahihi ukifika.

Zaidi ya hayo, Viongozi mbalimbali kutoka Vyama tofauti wameonesha nia ya kutaka kuwania Ubunge katika Jimbo hilo la Ilala. Mathalani, Muigizaji mwingine Rashidi Mwinshehe Saidi maarufu kama (Kingwendu) ametangaza nia ya kutaka kugombea Ubunge katika jimbo hilo Kupitia chama cha CUF.

=> Uchaguzi 2020 - Rashid Mwinshehe(Kingwendu) achukua fomu ya kugombea Ubunge jimbo la Ilala

Hata hivyo, kwa sasa Jimbo hilo la Ilala linaongozwa na Mh. Mussa Azzan Zungu wa Chama cha Mapinduzi.

1594819085713.png
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom