Napendekeza kuwe na JF classes; 1, 2. 3, 4 and 5, ili kila wahusika wa class fulani wachangie kwenye daraja lao. Vigezo viainishwe kutambua na ku-classify haya madaraja. Kuna watu humu, kwa mujibu wa argumentations katika mihango yao, ni dhahiri kuwa ni kiwango cha daraja la 5 lakini wanachangia katika hoja za daraja la kwanza, hivyo kufanya uchafuzi.
Pendekezo husika la Bunge linasema mamlaka ya uteuzi husika zishauriwe kuwajibisha wahusika..... wakati mamlaka hiyo bado hijashauriwa, ili ikubaliane au ikatae ushauri, wachangiaji JF daraja la 5 wanatangaza fulani amefukuzwa kazi ya uwaziri; amefukuzwa na nani?
JF daraja la 1 wanafahamu kuwa Prof. Muhongo bado ni Waziri wa Nishati na Madini kwa mujibu wa sheria za nchi.
Hata hivyo, sidhani iwapo mamlaka husika itakubaliana (soma give in) na shinikizo/ghiriba za akina Mengi & Co.