Kiabakari ni kijiji tu kama vijiji vingine ambavyo wananchi wake hawajui mambo yanavyondelea kwenye hii nchi ambako ndipo kimbilio la CCM. wana maisha magumu lakini hawajui kama wanaishi maisha magumu na wanaona ndiyo maisha wanayostahili kuishi. Lakini inawezekana pia (sina hakika) ikawa imetengenezwa; wamejuaje muhongo atapita wakajikusanya barabarani wakaanza kuimba na kupiga vigelegele kama hakukuwa na maandalizi mapema?
Tukumbuke kwamba suala la kufikisha umeme vijijini siyo suala la muhongo, ni suala la wizara na serikali kwa ujumla, kwa hiyo hata muhongo akitoka (ikitokea akatoka) bado mipango ipo na atakayeingia wizara hiyo ana wajibu wa kuliendeleza. Wananchi wasione kama ni fadhila za muhongo kuwapa umeme, wananchi wote wana haki ya kupata huduma hiyo bila kujali unaishi mjini au kijijini.
Lakini pia naomba unisadie kidogo, huo mchango alioutoa kwa wagombea ni mchango gani, wa fedha au wa mawazo? kama ni mchango wa fedha ni kwa ajili ya nini? Isijekuwa ni malipo ya kazi ya kuwa-mobilize kumsubiri na kuimba na kupiga vigelegele halafu tukaambiwa ni mchango.