Muhongo amfuata Jakaya Kikwete Uswisi

Muhongo amfuata Jakaya Kikwete Uswisi

IMG_1899-300x225.jpg

WAKATI Watanzania wakisubiri kujua hatima ya Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, aliyewekwa kiporo na Rais Jakaya Kikwete baada ya kuhusishwa na kashfa ya uchotwaji wa zaidi ya Sh bilioni 300 kwenye Akaunti ya Tegeta Escrow, waziri huyo amesafiri kwenda Davos nchini Uswisi kuungana na rais katika Mkutano wa Jukwaa la Uchumi Duniani maarufu kama World Economic Forum.

Kwa mujibu wa chanzo cha habari kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Muhongo ameondoka nchini jana. “Profesa ameondoka leo (jana) kwenda Switzerland (Uswisi) ambako ataungana na rais kwenye mkutano huo utakaoanza Januari 21 hadi 24,” kilipasha chanzo hicho.

MTANZANIA ilipomtafuta Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Salva Rweyemamu, ili kuthibitisha taarifa hiyo, hakuweza kutoa jibu na badala yake kumporomoshea mwandishi matusi huku akimwambia aachane na habari hiyo.

“Acha habari zenu za kipumbavu hizo,” alisema Salva.

Alipoulizwa habari za kipumbavu ni zipi na kwanini anatukana badala ya kutoa majibu alisema: “Nimekwambia acha upumbavu, kama unataka habari nipigie na kama hutaki usinipigie, siyo kila kitu mnachoandika tu lazima nizungumzie,” alisema na kukata simu.

Akizungumza na wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam Desemba 22 mwaka jana, Rais Kikwete alitangaza kumuweka kiporo Profesa Muhongo akisubiri kupata ufafanuzi kuhusu mambo kadha wa kadha ili kujiridhisha kabla kuujulisha umma juu ya hatua atakazochukua dhidi ya waziri huyo.

Wakati akimuweka kiporo Muhongo, Rais Kikwete alitangaza kutengua uteuzi wa aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka baada ya vyombo vya Serikali kubaini na kujiridhisha amekiuka maadili ya utumishi wa umma kwa kuingiziwa Sh bilioni 1.65 kwenye akaunti yake binafsi.

Rais Kikwete alifikia hatua hiyo akitekeleza moja ya maazimio manane ya Bunge kuhusu sakata la uchotwaji wa fedha kwenye akaunti ya Tegeta Escrow yaliyofikishwa serikalini lililopendekeza kuwajibishwa kwa Bodi ya Shirika la Umeme (Tanesco), Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Eliakim Maswi ambaye amesimamishwa kazi kupisha uchunguzi, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Tibaijuka, pamoja na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Muhongo.

Source:
Mtanzania

Yaan ninyi mnataka kila mtu aondolewe tu!
JK hayuko tayari kubembeleza urafiki na kaizari. Wayahudi walipiga kelele Yesu asulibiwe (hata kama hakuwa na kosa). Sasa Herode akatoa hukumu akikwepa kumwaga unga.

Hivyo, jambo hilo halitatokea kwa Muhongo. Hana makosa zaid ya #Khusda za wattu
 
Mnaemwita mzalendo sijui akili zenu mmeziacha wapi???Kama ndivyo,kwanini alimkana mwanasheria wa Tanesco aliyeleta ukweli???kwanin walimshinikiza kuachia ngazi na kumbambikizia kesi???hivi mnatetea nini hapa??acheni ujinga
 
ivi tanzania davos inaenda kufanya nn kama si kupoteza tu pesa za walipa kodi, ile ni club ya big boys makampun makubwa duniani na nchi tajiri zenye viwanda sie inatuhusu nn!!!! ujinga wa mwafrika hautaisha milele!!!
 
Wakati baadhi ya wapinga maendeleo nchini wakipuuza uwezo wa Prof. Sospeter Muhongo ktk utendaji kazi wake, wanaotambua uwezo wake wanatumia mawazo na taaluma yake kuendeleza nchi zao kwenye sekta ya Nishati na Madini. Prof. Muhongo amealikwa Davos nchini Uswisi kuhudhuria kwenye World Economy Forum, mkutano huo mkubwa unashirikisha viongozi na wataalamu kutoka mataifa mbalimbali.

Pia waziri Muhongo amealikwa na serikali ya Marekani kwenye mkutano mkubwa unaojadili masuala ya Nishati ambapo atakuwa mmoja wa wazungumzaji kwenye mkutano huo. Aidha, Prof. Muhongo akitoka Marekani, atakwenda nchini Italia kwa mwaliko wa nchi hiyo kwa ajili ya kutoa mada kwenye mkutano unaojadili masuala ya Madini. Huyo ndo waziri mchapakazi Prof. Sospeter Muhongo ambaye hatuoni thamani yake lakini wenzetu wanaiona na kuitumia, ipo siku tutamkumbuka!!
 
cc,mengi
 
Hata kama kwenye macho hawataki lakini watamsoma kimoyo.
 
Mbona kuna taarifa kwamba JK amewaita mawaziri wake wote warudi Dar, na ambao tayari wako Dar wasitoke.

Vipi hiyo taarifa ni ya uongo au haimuhusu Prof Muhongo.
 
Anakwenda kuwafundisha nini huko? Davos, Marekani, Italia etc. wanahangaikia miradi ya REA na wao? Ngoja akawapige lecture njia rahisi ya kupeleka umeme vijijini Marekani na Italy. Pia atawafumbua macho kuhusu miradi ya umeme wa gesi nchini mwao wapunguze gharama za walaji. Tena ikibidi wamchukue moja kwa moja awe mtaalamu wao.

Sifa za kijinga!!!!
 
Mbona kuna taarifa kwamba JK amewaita mawaziri wake wote warudi Dar, na ambao tayari wako Dar wasitoke.

Vipi hiyo taarifa ni ya uongo au haimuhusu Prof Muhongo.
Taarifa ya uongo hiyo
 
Hili litoa mada nalo sijui leo limeamkia wapi, limeshanichefua kabisa!
 
Wakati baadhi ya wapinga maendeleo nchini wakipuuza uwezo wa Prof. Sospeter Muhongo ktk utendaji kazi wake, wanaotambua uwezo wake wanatumia mawazo na taaluma yake kuendeleza nchi zao kwenye sekta ya Nishati na Madini. Prof. Muhongo amealikwa Davos nchini Uswisi kuhudhuria kwenye World Economy Forum, mkutano huo mkubwa unashirikisha viongozi na wataalamu kutoka mataifa mbalimbali.

Pia waziri Muhongo amealikwa na serikali ya Marekani kwenye mkutano mkubwa unaojadili masuala ya Nishati ambapo atakuwa mmoja wa wazungumzaji kwenye mkutano huo. Aidha, Prof. Muhongo akitoka Marekani, atakwenda nchini Italia kwa mwaliko wa nchi hiyo kwa ajili ya kutoa mada kwenye mkutano unaojadili masuala ya Madini. Huyo ndo waziri mchapakazi Prof. Sospeter Muhongo ambaye hatuoni thamani yake lakini wenzetu wanaiona na kuitumia, ipo siku tutamkumbuka!!

Hata shemeji yetu Faraja huwa anaalikwa Davos mara nyingi tu!
 
IMG_1899-300x225.jpg

WAKATI Watanzania wakisubiri kujua hatima ya Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, aliyewekwa kiporo na Rais Jakaya Kikwete baada ya kuhusishwa na kashfa ya uchotwaji wa zaidi ya Sh bilioni 300 kwenye Akaunti ya Tegeta Escrow, waziri huyo amesafiri kwenda Davos nchini Uswisi kuungana na rais katika Mkutano wa Jukwaa la Uchumi Duniani maarufu kama World Economic Forum.

Kwa mujibu wa chanzo cha habari kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Muhongo ameondoka nchini jana. “Profesa ameondoka leo (jana) kwenda Switzerland (Uswisi) ambako ataungana na rais kwenye mkutano huo utakaoanza Januari 21 hadi 24,” kilipasha chanzo hicho.

MTANZANIA ilipomtafuta Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Salva Rweyemamu, ili kuthibitisha taarifa hiyo, hakuweza kutoa jibu na badala yake kumporomoshea mwandishi matusi huku akimwambia aachane na habari hiyo.

“Acha habari zenu za kipumbavu hizo,” alisema Salva.

Alipoulizwa habari za kipumbavu ni zipi na kwanini anatukana badala ya kutoa majibu alisema: “Nimekwambia acha upumbavu, kama unataka habari nipigie na kama hutaki usinipigie, siyo kila kitu mnachoandika tu lazima nizungumzie,” alisema na kukata simu.

Akizungumza na wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam Desemba 22 mwaka jana, Rais Kikwete alitangaza kumuweka kiporo Profesa Muhongo akisubiri kupata ufafanuzi kuhusu mambo kadha wa kadha ili kujiridhisha kabla kuujulisha umma juu ya hatua atakazochukua dhidi ya waziri huyo.

Wakati akimuweka kiporo Muhongo, Rais Kikwete alitangaza kutengua uteuzi wa aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka baada ya vyombo vya Serikali kubaini na kujiridhisha amekiuka maadili ya utumishi wa umma kwa kuingiziwa Sh bilioni 1.65 kwenye akaunti yake binafsi.

Rais Kikwete alifikia hatua hiyo akitekeleza moja ya maazimio manane ya Bunge kuhusu sakata la uchotwaji wa fedha kwenye akaunti ya Tegeta Escrow yaliyofikishwa serikalini lililopendekeza kuwajibishwa kwa Bodi ya Shirika la Umeme (Tanesco), Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Eliakim Maswi ambaye amesimamishwa kazi kupisha uchunguzi, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Tibaijuka, pamoja na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Muhongo.

Source:
Mtanzania

Ukoo wa panya
 
Udhaifu wa serikali shuruti uwe udhaifu wa wananchi, kama sio kweli lazima kungechimbika ardhi ya TZ
 
Profesa Muhongo aalikwa Uswisi, Marekani
Atahutubia mikutano ya wasomi duniani

Na mwandishi wetu,

W
aziri wa Nishati wa Tanzania Profesa Sospeter Muhongo amealikwa kuhudhuria mkutano unaoshirikisha viongozi na wataalamu kutoka mataifa mbali mbali nchini Uswisi.

Mkutano huo ujulikanao kama World Economic Forum unafanyika jijini Davos nchini humo. Aidha kutoka nchini Uswisi, Profesa Muhongo ataelekea nchini Marekani alikoalikwa na Serikali ya nchi hiyo kwenye mkutano mkubwa unaojadili masuala ya nishati ambapo yeye atakuwa mmoja wa watoa mada.
Akitoka nchini Marekani, Profesa Muhongo ataelekea nchini Italia ambako pia amealikwa kama mmoja wa wataalamu duniani. Wakati mataifa makubwa yakipigana vikumbo kuwasilisha mialiko kwa Profesa Sospeter kwa kuthamini na kuheshimu utalaamu wake, wanasiasa na wafanyabiashara hapa nchini wameendelea kupuuza utaalamu huo na kuwalaghai watanzania.
Kikundi hicho cha watu wenye kusaka madaraka wanaotafuta fursa ya kuiweka mkononi serikali ijayo, wamekuwa wakitumia vyombo vya habari kuchafua wataalamu na wasomi mahiri wanaoheshimika duniani kama Profesa Muhongo.
“Inasikitisha wapinga maendeleo hawa wanaotumiwa na mataifa yale yale yanayothamini utaalamu wa akina Muhongo, wameendelea kuwafanya watanzania wajinga wao wanaoweza kuwaburuza kwa propaganda na kuwchafua watu wema na wazalendo”, ameeleza kwa masikitiko Bwana Swedi Mfanyabishara jijini Dar es salaam.
Aidha ameelezea kushangazwa na watu waliojipatia uheshimiwa ambao awali amedai walikuwa wezi na majambazi, wanavyoweza kuwa na ujasiri wa kuwatukana wataalamu kama Profesa Muhongo. “Umefika wakati sasa kwa wazalendo wa nchi hii kusimama imara kupambana na watu hawa ili kuwaokoa watanzania wasiangukie mikononi mwa mabepari na wezi wa rasilimali zao”, amedai.
Wakati huo huo, Waziri Muhongo ameiagiza Bodi ya TANESCO ifuatilie miradi ya umeme ya makaa ya mawe ili kumaliza kabisa tatizo la upatikanaji wa umeme nchini.
Aidha mradi wa umeme vijijini(REA) unatarajiwa kupeleka umeme kwenye vijiji 1,500 nchini kote na kwamba Waziri Muhongo ameagiza mikoa na wilaya kuhakikisha mradi huo unakamilika kabla ya Aprili 30 mwaka huu. ( Source; ALHUDA)
 
Back
Top Bottom