Muhongo amfuata Jakaya Kikwete Uswisi

Muhongo amfuata Jakaya Kikwete Uswisi

RUCCI

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2011
Posts
1,702
Reaction score
1,716
IMG_1899-300x225.jpg


WAKATI Watanzania wakisubiri kujua hatima ya Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, aliyewekwa kiporo na Rais Jakaya Kikwete baada ya kuhusishwa na kashfa ya uchotwaji wa zaidi ya Sh bilioni 300 kwenye Akaunti ya Tegeta Escrow, waziri huyo amesafiri kwenda Davos nchini Uswisi kuungana na rais katika Mkutano wa Jukwaa la Uchumi Duniani maarufu kama World Economic Forum.

Kwa mujibu wa chanzo cha habari kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Muhongo ameondoka nchini jana. "Profesa ameondoka leo (jana) kwenda Switzerland (Uswisi) ambako ataungana na rais kwenye mkutano huo utakaoanza Januari 21 hadi 24," kilipasha chanzo hicho.

MTANZANIA ilipomtafuta Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Salva Rweyemamu, ili kuthibitisha taarifa hiyo, hakuweza kutoa jibu na badala yake kumporomoshea mwandishi matusi huku akimwambia aachane na habari hiyo.

"Acha habari zenu za kipumbavu hizo," alisema Salva.

Alipoulizwa habari za kipumbavu ni zipi na kwanini anatukana badala ya kutoa majibu alisema: "Nimekwambia acha upumbavu, kama unataka habari nipigie na kama hutaki usinipigie, siyo kila kitu mnachoandika tu lazima nizungumzie," alisema na kukata simu.

Akizungumza na wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam Desemba 22 mwaka jana, Rais Kikwete alitangaza kumuweka kiporo Profesa Muhongo akisubiri kupata ufafanuzi kuhusu mambo kadha wa kadha ili kujiridhisha kabla kuujulisha umma juu ya hatua atakazochukua dhidi ya waziri huyo.

Wakati akimuweka kiporo Muhongo, Rais Kikwete alitangaza kutengua uteuzi wa aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka baada ya vyombo vya Serikali kubaini na kujiridhisha amekiuka maadili ya utumishi wa umma kwa kuingiziwa Sh bilioni 1.65 kwenye akaunti yake binafsi.

Rais Kikwete alifikia hatua hiyo akitekeleza moja ya maazimio manane ya Bunge kuhusu sakata la uchotwaji wa fedha kwenye akaunti ya Tegeta Escrow yaliyofikishwa serikalini lililopendekeza kuwajibishwa kwa Bodi ya Shirika la Umeme (Tanesco), Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Eliakim Maswi ambaye amesimamishwa kazi kupisha uchunguzi, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Tibaijuka, pamoja na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Muhongo.

Source:
Mtanzania
 


MTANZANIA ilipomtafuta Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Salva Rweyemamu, ili kuthibitisha taarifa hiyo, hakuweza kutoa jibu na badala yake kumporomoshea mwandishi matusi huku akimwambia aachane na habari hiyo.

"Acha habari zenu za kipumbavu hizo," alisema Salva.

Alipoulizwa habari za kipumbavu ni zipi na kwanini anatukana badala ya kutoa majibu alisema: "Nimekwambia acha upumbavu, kama unataka habari nipigie na kama hutaki usinipigie, siyo kila kitu mnachoandika tu lazima nizungumzie," alisema na kukata simu.

Source:Mtanzania

Kama ni kweli alisema hivyo anastahili kupelekwa hospitali akapimwe akili. Anasahau kwamba akiwa katika ofisi ya serikali anawajibika kwa wananchi, ikiwa ni pamoja na kupitia waandishi wa habari?

Hawa maofisa wengine sijui wameingiliwa na mdudu gani kichwani anaewafanya wafikiri wao ni wao katika nchi hii, na wengine wote ni wapumbavu wasiostahili hata kuwafunulia midomo. Arrogance ya namna hii haistahili kabisa toka kwa mtu aliye ofisi ya serikali.

Kama ni upumbavu basi upumbavu uko kwake asiyejua jinsi ya ku-handle waandishi wa habari huku akijua yuko katika ofisi itakayomkutanisha na waandishi wa habari karibu kila siku. Kama kazi inamshinda si aombe tu kubadilishwa au kujiuzulu?
 
RUCCI
Ameenda kuhamisha ela za ESCROW huyo, hakuna chochote alichoenda kufanya huko
 
Last edited by a moderator:
Jambazi la ESCROW laendelea kula kodi za Wananchi ... RUCCI
 
Last edited by a moderator:
Si inaeleweka kuwa nyingi ya pesa za ufisadi 'zinazopigwa' na viongozi wa nchi barani Afrika, huwa zinawekwa kwenye mabenki nchini Uswisi?

İnawezekana mkulu, pamoja na 'kiporo' chake, wameorganize trip hiyo, ili waende huko uswisi, kwenda 'kuzichungulia' hizo account zao, ili kujiridhisha kuwa hazijawa frozen na nchi 'wanoko' za wafadhili, waliokata misaada yao kuja nchini kwetu, kutokana na skandali hiyo ya Escrow!
 
Mleta mada shida iko wapi hapo,nyie mnadhani kila mnaepiga makelele aondolewe anaondolewa,acheni ulofa na ukanjenje.

Mkuu mbona mimi sijaona shida ya mleta mada?Alichofanya ni kuleta habari wala hajawa biased upande wowote dont rush to post anything soma na uelewe then ndo ujibu.
 
Wasiwasi wangu si hatma Prof Muhongo, bali ni hatma ya legacy atakaoiacha Mkuu baada ya kuhitimisha ng'we yake!!!!!
Asishangae kama ataishia kuzomewa mitaani kutokana na umaliziaji wake usiokuwa na mvuto kwa wapigakura waliomwingiza madarakani wakiwa na matumaini makubwa!
 
Jamani upotoshaji huu hadi lini? Leo asubuhi muhongo alikuwa mara,kaenda mda gani uswisi?
 
No wonder umevimbiwa fedha za ESCROW! Pamoja na Uongo wote wa kulidanganya Bunge na wananchi pale Mjengoni! Pamoja na Kuhusika kwake kwenda kumleta Sethi kwaajili ya kufanikisha deal la ESCROW! Pamoja na kukataa Ushauri wa Mwanasheria Ngwilimi aliekwenda kufanikisha Due Diligence kule Malaysia na kasha kumlazimisha ajiuzulu na baadae kutengeneza Uongo ambao hata m.toto wa darasa la kwanza anaugundua BADO unaendelea kumsafisha huyu Kuwadi wa Rasilimali zetu? Tambua kuwa Cheo ni Dhamana na kama kweli angekuwa msafi asingeng'ang'ania madaraka bali angachia ngazi kasha wananchi wamsafishe kama kweli hakuhusika ... Kuendelea kukumbatia Uwaziri ni UFISADI mwingine wa kuendelea kutafuna fedha za walipa kodi ... Soon ataburuzwa mahakamani ....
Huyu ni kiongozi mzalendo katika serikali hii' fitina zenu hazina mashiko ndugu yangu! Tafuten.zengwe jingine
 
Back
Top Bottom