Muhitimu wa kidato cha sita,nini nifanye kwa laki moja ndani ya hii miezi

Rabiel

Senior Member
Jul 20, 2013
197
40
Wakubwa habari,

mimi ni muhitimu wa kidato cha sita mwaka 2016, sijachaguliwa JKT, kwa sasa nipo Dar, nini nifanye kwa mtaji wa laki moja ndani ya hii miezi kabla ya kwenda chuo,

Msaada wenu tafadhali.
 
uza mapupu jitahidi uwe unawahi kila siku asubuhi vingunguti,ama sambusa za viazi,ama tembezi mihogo mibichi kwenye foleni.ukishindwa hivyo nunua dawa za panya na mende za30000 tafuta baskeli ya60000 na kipaza sauti pita mtaani tangaza unauza dawa za mende.nafkiri laki si ndogo huenda ikakutoa kwa staili hyo otherwise mengine hutoweza kalale uwe unakula mihogo tu,eti laki
 
nenda karume au ilala sokon okota mitumba ya watoto ya buku buku ingia mtaani kapige buku mbili mbil au buku jelo jelo,uta make mkwanja tu ila usione tabu kusaga nyayo.ukipata hata za wadada\wamama pia mzuka tu.
 
Back
Top Bottom