Kwa mtaji wa million 1 nifanye biashara gani?

Kwa mtaji wa million 1 nifanye biashara gani?

Sisa Og

JF-Expert Member
Joined
Apr 18, 2024
Posts
201
Reaction score
515
Habari zenu wana JF? Matumaini yangu hamjambo Kabisa.

Mimi naomba ushauri wenu. Nina mtaji wa millioni moja. Nipo Dar es Salaam. Ni biashara gani inafaa kwa mtaji huo.

Kichwani, nilikuwa nawaza kufungua movie library mtaani ila nikasema ngoja nisikie mawazo ya wengine.

Asanteni, nishaurini chochote ntazingatia.

Siku njema.
 
Chukua mia7 au 8 chukua roba za.mtumba nne au tano za viatu za kufungua mwenywewe, rudi nao magetoni uoshe uwe safi kabisa, kama kuna kiatu kina demage tafuta gundi au supa glue ziba, kama ni cha kushona shona.

Ukimaliza ndugu yangu nunua taa yako then kajichanganye kwenye yale masoko ya usiku, kuanzia saa 12 mpaka saa tatu mwaga mzigo wako chini, hakuna kodi hakuna tozo hakuna mgambo utakuja kunishukuru.
 
Nitumie hiyo hela niwe nakutumia mchele toka shinyanga maana huku kilo wanauza tsh 1300 sijui huko dar yenu ila naamini uko juu sana.
 
fungua kibanda cha mboga mboga_dagaa, furu,vituguu,nyanya,mafuta ya kula,maharage,mchele> ila sijui huko uliko kama mazingira yanaruhusu ungekuwa mkoani huku hiyo biashara ni mkombozi pia inafaida mno na hiyo pesa mkoani huku ni ndefu maana hatuna matumizi mengi ya kimaisha yaani frem tunakodi kwa elfu 5 kwa mwezi harafu mahitaji ya mboga ni makubwa sana me nipo shinyanga.
 
Asante kwa wazo
 
Mekj
Chukua mia7 au 8 chukua roba za.mtumba nne au tano za viatu za kufungua mwenywewe, rudi nao magetoni uoshe uwe safi kabisa, kama kuna kiatu kina demage tafuta gundi au supa glue ziba, kama ni cha kushona shona.

Ukimaliza ndugu yangu nunua taa yako then kajichanganye kwenye yale masoko ya usiku, kuanzia saa 12 mpaka saa tatu mwaga mzigo wako chini, hakuna kodi hakuna tozo hakuna mgambo utakuja kunishukuru.
Mekupata kiongozi. Asante sana
 
Habari zenu wana JF? Matumaini yangu hamjambo Kabisa.

Mimi naomba ushauri wenu. Nina mtaji wa millioni moja. Nipo Dar es Salaam. Ni biashara gani inafaa kwa mtaji huo.

Kichwani, nilikuwa nawaza kufungua movie library mtaani ila nikasema ngoja nisikie mawazo ya wengine.

Asanteni, nishaurini chochote ntazingatia.

Siku njema.
Kama unahitaji kufanikiwa kwa haraka kwakutengeneza faida kubwa ukiwa kama mjasiriamali mdogo jikite katika biashara za kutatua changamoto za watu tunaziita biashara za kitalaam (Expert Business)

Aina ya biashara hizi hazihitaji mtaji mkubwa wa pesa badala yake mtaji wake mkubwa ni suluhisho unalomiliki lenye kubeba majibu ya changamoto zinazo wasumbua watu

Mfano biashara nnayofanya mimi mtaji wake sio zaidi ya Tsh.100,000 lakini naweza kutengeneza faida Tsh.350,000 na zaidi kwa wiki tu

Lakini pia ili kufanya biashara hizi hauna ulazima wa kuwa na frem/physical office

Badala yake utatumia simu yako kama ofisi kwakuendesha biashara yako mtandaoni

Mfano unaweza kuwa una ujuzi wowote wa kiufundi mfano fundi ujenzi au mbunifu wa majengo

Hapo tayari unaweza kuanzisha biashara ya kitaalam ya kuwasaidia watu kuanza ujenzi kwa gharama ndogo na wakakulipa kama mtaalam

Majumbani watu wanasumbuka na uchafu sugu chooni,bafuni,jikoni n.k usiowezekana kutoka kwanjia za kawaida

Unaweza kujikita katika biashara ya kutengeneza dawa za usafi ambapo ukawa unatoa na huduma za usafi kwakusafisha sehemu zote zenye uchafu sugu

Kufanya usafi ukipewa tenda ya nyumba nzima unaweza kutengeneza kati ya Tsh.50,000 mpaka Tsh.250,000 huku mtaji wako utakao tumia ni kati ya Tsh.10,000 mpaka Tsh.30,000 kutokana na ukubwa wa kazi.

Hizo ni baadhi tu skills za Expert Business unazoweza kufanya na kujitengenezea kipato kikubwa

Unaweza kujiuliza wateja unapata wapi? Very simple utatumia simu yako kutangaza huduma zako mtandaoni na kujitengenezea soko kubwa mtandaoni

Yapo masoko mengi unayoweza kufanya mtandaoni ukiwa kama mtaalam na kutengeneza pesa nyingi ukiwa nyumbani kwako

Niko tayari kukusaidia mafunzo na muongozo ili uweze kutoka kiuchumi naamini utarudi hapa na mrejesho mzuri

Mafunzo ntakupatia bure mpaka pale utakapo weza kusimama mwenyewe nitafute WhatsApp kwa namba hii 0765949465.
 
Uzi wa muda sana, ningekupa ushuhuda wangu kuhusu huo mtaji wako.
 
Mimi nilikuwa na mtaji wa million 1, wazo langu ilikuwa kufungua duka la vyakula (haya maduka ya akina mengi) ila mtu mmoja akaniambia mtaji wako ni mdogo na hautaweza kushindana na hawa waha, nadhan unajua umahiri wa waha kwenye ishu ya duka. Nilipoangalia nikakiri mwenyewe kwa mtaji wangu sitaweza kutoboa.
Ushauri wake nifungue uwakala wa pesa. Hili wazo nikaona ni zuri. Kwahiyo nikaza kufuatilia TIN na lesen ili nipate laini zenye majina yangu. Nikafanikiwa kupata tin na lesen. TIN ilikuwa ni bure ila lesen kwa kipindi hicho iligharimu 83000.

Nilipopata hivyo vitu nikafanya mchakato wa lain. Nikatuma maombi kampun 4 za simu, na kila lain iligharimu 10000 kwa ajili ya muhuri wa mwanasheria. Baada ya hapo nikaza kutengeneza Banda la mbao. Kwenye banda vitu vingi nilitoa home kama mbao na bati. Ndani kama ya wiki Banda lilikuwa tayari. Nikawa nasubir laini, nakumbuka lain ya kwanza kutoka ilikuwa ya Airtel, huwa wako faster sana.
Muda ukawa unaenda na mkononi lain moja tu, nikamua kununua laini ya tigo. Mpaka hapo nikawa na lain za mitandao 2, Airtel na tigo.

Kazi ikaza na laini zangu 2, mpaka naza kaza mtaji ulisoma laki 7, laki 3 ilitumika kwenye lesen, kununua simu, Banda, gharama za lain na kununua lain ya tigo.
Baada muda nikapata lain ya halotel, lain ya voda ilichelewa sana. Ila nayo nilifanikiwa kuipata.

Changamoto ambazo nilikutana nazo ni float na cash. Mtaji wangu ulikuwa ni mdogo. Kuna muda mteja anataka kuweka elfu 50 au laki ila huna. Ukimkuta mteja si mstaarab anakujibu hovyo. Nakumbuka wateja km 3 waliniambia hapa unafanya nini sasa, bora tufunge ukalale tu. Ila nilikomaa.

Leo hii nimepiga hatua kubwa mtaji umekuwa, na ni mmoja wa mawakala ambao wananitegemea. Sikuchukua mkopo, kitu ambacho nilikifanya Yale malipo ya mwisho wa mwenzi nilikuwa nachukua elfu 50 kwa matumiz yangu inayobaki nilikuwa naiacha kwenye mtaji.
Zilipokuja hizi lain za lipa, ndo zilinisafishia njia. Zilinifanya nipige hatua kubwa sana.
Nilikuja kuongeza uwakala wa bank (NMB, CRDB, na NBC). Bank walikuwa hawatoi uwakala kwa mtu kwenye kinanda kama changu. Ila ilibidi wanipe kwasababu kuna doc waliomba wakakuta kazi inafanyika, miamala inasoma. Nakumbuka watu wa kwnza kunipa ni NMB kwahiyo bank zingine ilibidi wanipe tu. Watu walikuwa wakishanga kibanda kama changu halafu Nina huduma za kibank.

Kwahiyo kwa mtaji wako angalia biashara unayotaka kuifanya, eneo, washindan wako. Unaweza kuhisi mtaji wako ni mdogo ila kwa eneo ulilopo na mtaji wako ukikoma unatoboa. Mpaka washindan wanakuja wanakuta tayari una uzoefu.
 
Back
Top Bottom