Muhimbili wamethubutu na wameweza

Muhimbili wamethubutu na wameweza

Mkuu nikusahihishe kidogo. Cath Lab au catheterization laboratory kwa kitaalamu sio kifaa bari ni laboratory ndani yake ndo kuna kifaa au machine inayotumika kuingiza catheter huku ukiiona kwenye screen na hii machine ni x-ray, ina weza kua digital subtraction angiographic machine (d.s.a) kwahiyo mkuu, hiyo cath lab ni chumba na inavifaavingi kwa ujumla ndo inaita hivyo.

images
images
 
Huwezi kutenganisha ubovu wa huduma za afya na siasa, huwezi kutenganisha ubovu wa shule zetu na siasa, nk. Sijui una uelewa wa kiwango gani, lakini lazima ujiulize kwa nini urefu wa barabara za rami ndo mtaji wa kisiasa wa CCM? Mtoa mada anaandika kiusahihi kabisa kama CCM walivyozoea kwamba hata walipojenga bomba la maji shinyanga, waliamini ndo mtaji wao kisiasa. Waliponunua MRI machine, kila siku tulionyeshwa kuwa ndo mafanikio ya CCM! Of course tyhat is rubbish, lakini ndo walivyozoea!

Mimi nasema hivi bila kujali shida ya afya uliyonayo, haikustahili kusubiri miaka 54 ya uhuru bila kuwa na mashine ya moyo. Ni uzembe na upungufu wa akili za kupanga mambo ya maendeleo. Miaka 54 serikali haijajenga hospitali yoyote mpya, lakini serikali hiyo hiyo ina ofisi za CCM za magorofa kwa kila mkoa! Kila katibu na mwenyekiti ana gari la milioni 200.
Amua mwenyewe unachotetea.

Wewe akili yako imejaa siasa haaaaa!Uambiwe nini uelewe! hata suala la kukata Bima ya afya unasubiri mkutano wa siasa wakuambie!acha kujiharinia bwana kama huelewi usichangie nenda kaungane na wenzio Mwanza!
 
Ushauri tu!Afya haina siasa!ni vizuri kufuatilia kwa makini elimu ya Afya ili kuepuka kupata magonjwa ambayo kimsingi yanaepukika!ulevi kupindukia,uvutaji wa sigara, madawa ya kulevya, utumiaji na unywaji wa vitu vikali kwa afya, matumizi ya kemikali, vipodozi na mazingira hatarishi!! Haya mambo ndo yanafanya watu kuteseka na magonjwa makubwa!Pia tatizo la watu kutokujenga utamaduni wa kufanya mazoezi mara kwa mara kunafanya taifa lisiwe na watu wenye afya bali uwepo wa wingi wa watu wenye afya mgogoro!

Huduma za afya ni ghari hakuna asiyejua hilo ndo maana kuna baadhi ya mambo yanafanywa kwa awamu na sasa yamefanyika na hali iko tofauti na mchangiaji alivyosema!nimesema Siasa hazina nafasi kwenye afya, maaana afya ni uhai!Kama mchangiaji huna jipya bora ukae kimya tu na kupita kimyakimya kwenye uzi huu!

mkuu nani mwenye jukukmu la huhakikisha kuwa umma una taharifa sahihi juu ya elimu ya kinga?, kwa haraka ukiitazama jamii unatambua kuwa watu wanakosa taarifa sahihi juu ya afya zao, dalili ni kushamiri kwa waganga wa kienyeji, (rejea kikombe cha babu-hata wale tuliowatarajia kuwa wana elimu ya kutosha ya afya nao walienda! hapo ndo ujue tatizo lilivo kubwa.)
kuhusu kufanya mazoezi, ni proportion ya watanzania wachache sana wenye kuhitaji kufanya mazoezi kwani wengi wao shughuli zao za kila siku ni mazoezi tosha na pengine zaidi ya mazoezi.
 
Wewe akili yako imejaa siasa haaaaa!Uambiwe nini uelewe! hata suala la kukata Bima ya afya unasubiri mkutano wa siasa wakuambie!acha kujiharinia bwana kama huelewi usichangie nenda kaungane na wenzio Mwanza!

Huna la maana kwa kiwango nilichotegemea JF. hatutaweza kuelewana kwa sababu moja tu, nayo ni hiyo niliyoweka chini kwenye signature yangu.
 
Mkuu ni majanga, yahani taifa lenye
watu zaidi ya milioni 45 wanatumia ct-scan machines moja! huku mkiongeza idadi ya magari ya washa washa

washa washa muhimu kwa watu kama nyinyi msiopenda kutii sheria bila shuruti, we kweli poyoo hujui kuwa hata marekani na ulaya magari ya washawasha yapo, sembuse bongo yetu kuna mijitu kila siku inawaza vurugu na maandamano yasiyo na kichwa wala miguu
 
Takataka! Miaka 54 ya uhuru leo ndo haya yanatangazwa! Tena unatibu kwa kusaidiwa na wayahudi! Niliyeko mtwara nije Dar es salaam kupanga foleni ya tiba?

Mwaka 2005 Dr Masau alipotangaza haya, mbona tuliona hao hao wanafiki wa Muhimbili wakijitokeza na kusema ni kinyume cha maadili kujitangaza? Leo hii unaleta tangazo lile lile ili iweje?

Walioanza ni THI Tanzania Heart Institute ya marehemu Masau.
....exactly....mambo aliyokuwa anafanya dr. Masau (the late)miaka ya 2006 ndiyo wanatamba nayo sasa ccm....this is so sad....yaani kipindi kile walikua wanampiga zengwe Dr. Masau aliyekuwa anapambana kuyafanya haya wanayotamba nayo leo...alafu leo wanataka kuwapumbaza watanzania (kama kawaida yao)kwamba wanafanya mambo makuubwa...hii inashangaza sana....Ndio maana wanasema watanzania ni watu wa kusahau sana..maana watawala huwapumbaza kirahisi sana...Tena kipindi kile Dr. Masau alikua anafanya mpaka International conferences za Cardiac surgery (including tele conferences)...akiwahusisha mabingwa wa cardiology na cardio surgery kutoka pande mbalimbali za dunia....Alafu eti leo watawala wanawapumbaza wabongo eti wanafanya mambo haya ya ajabu!...kweli tuna safari ndefu....

...Hizi cardiac catheterization kwa wenzetu hufanywa routinely kama common procedures...Siasa za kibongo kweli zimeingilia taaluma....kila kitu kinahusishwa na siasa....
 
"...usibeze pasipobezeka."
 
washa washa muhimu kwa watu kama nyinyi msiopenda kutii sheria bila shuruti, we kweli poyoo hujui kuwa hata marekani na ulaya magari ya washawasha yapo, sembuse bongo yetu kuna mijitu kila siku inawaza vurugu na maandamano yasiyo na kichwa wala miguu
sitashangaa, ukiwa na fikra kama hizi lazima na vipaumbele vyako yawe majanga matupu.
 
Kumekuwa na mafanikio makubwa katika utoaji wa huduma za afya Hospitali ya Taifa Muhimbili. Kwamba sasa, wagonjwa wenye matatizo ya moyo wataweza kufanyiwa uchunguzi na kuweza kuhudumiwa kwa kuzibua mishipa inayopeleka damu kwenye moyo kwa mfumo wa kisasa zaidi.

Kwamba wagonjwa wenye matatizo hayo ya moyo, wataweza sasa kuzibuliwa matundu hayo kwenye moyo bila kufanyiwa upasuaji kifuani. Hii, kwa hakika ni habari njema, tena yenye kustahili kupongezwa.

Kwa mujibu wa taarifa kuhusu mafanikio haya, ni kwamba kufungwa kwa mtambo maalumu Hospitali ya Taifa Muhimbili, "Cath Lab" ndiko kutafanikisha huduma hizo muhimu katika maisha ya binadamu.

Kwa ufafanuzi tu ni kwamba, Cath Lab ni mtambo maalumu unaotumika kufanya uchunguzi, kuzibua mishipa inayopeleka damu kwenye moyo na kuziba matundu ya moyo bila kufanya upasuaji.

Kwa kuzingatia ukubwa wa magonjwa ya moyo nchini na gharama ambayo serikali na hata watu au taasisi binafsi zimekuwa zikiingia kusafirisha wagonjwa wa moyo kwa ajili ya kuokoa maisha yao kwa tiba za aina hii nje ya nchi, hakika, kwa kiasi kikubwa hatua hii itasaidia kuipa sura mpya sekta ya afya hapa nchini.

Tunajivunia wataalamu wetu nchini ambao tayari wameutumia mtambo huu kwa ufanisi mkubwa, kupitia Kitengo cha Tiba ya Moyo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, wakifanikiwa kufanya tiba ya moyo kwa kuziba matundu ya kwenye moyo bila kufanya upasuaji wa kifua.

Lakini si tu wataalamu wetu hapa nchini bali hata wenzao kutoka nje ya nchi ambao, kwa pamoja, wamefanikisha tiba hiyo, hao ni pamoja na madaktari bingwa kutoka Hospitali ya Prince Sultan Cardiac Centre ya Riyadh Saudi Arabia.

Tunaungana na Watanzania wengi katika kuamini kwamba hi ni hatua nyingine kubwa katika nyanja ya tiba na afya nchini baada ya kushuhudia ushirikiano wa aina hii na hospitali nyingine kadhaa za kimataifa kwa kutumia mifumo ya habari kama Video Conference ambayo huwawezesha madaktari kufanya upasuaji nchini kwa kushirikiana na madaktari bingwa wenzao walioko nje ya nchi.

Umetumwa Au umerogwa na Kama siyo basi upeo wako wa elimu juu ya heart surgery ni mdogo Au hujui mbaya zaidi huna uwezo wa kufanya cardiovascular surgical analysis ndo maana unaongea pumba zaidi ktk muktadha wa jambo usilolielewa.

Umeendika habari Kama za chereko chereko.
 
Kwa hela ipi? Ukinijibu hapo nitakuunga mkono kwamba Muhimbili mmeweza....hamjachangishana ni pesa ya kodi ya kila mtanzania. Naomba ubadili useme watanzania tumeweza, tumethubutu ....usijipachike gauni la taifa na kujifanya umelinunua wewe KARIAKOO. Nguo ya kuazima....malizia kama unajua kiswahili
 
Afya ni ghari ndugu yangu, pole sana ndio maana Serikali inawahamasisha wananchi kuwa na bima ya afya katika maeneo yao maana tiba ni gharama! Maana hata machinga na wajasiriamali wanahimizwa kila leo kuwekeza kwenye Bima ya afya kwa sababu hiyo hiyo maana ugonjwa hauna taarifa!Nakushauri kama na wewe hauna bima ya Afya kata ili baadaye usiilaumu Serikali yako kwa mambo ambayo yako ndani ya uwezo wako kwa manufaa yako! Juhudi unayoitumia kukomaa kupata mil. 2 nakuomba uitumie hivyo hivyo kukata Bima ya Afya!Uguza salama ndugu!

Mkuu sio kila mwananchi anabima na wala sijazungumzia bima hapo nimezunguza tushwa iliupate hudima laiti ungejua pia hao madaktari hapendi watu wanao tumia bima sababu tu hawapati chochote kitu.

Huduma ya afya kwa tanzania ni anasa.
 
washa washa muhimu kwa watu kama nyinyi msiopenda kutii sheria bila shuruti, we kweli poyoo hujui kuwa hata marekani na ulaya magari ya washawasha yapo, sembuse bongo yetu kuna mijitu kila siku inawaza vurugu na maandamano yasiyo na kichwa wala miguu
Mkulimawakiteto magari ya washawasha Ulaya no machache kuliko hospital na vifaa tiba kwa ajili ya afya za with wake. Huyo jamaa yuko sahihi viongozi wetu wanajali sana kusalia madarakani kwa vitisho kuliko kuimarisha huduma muhimu za afya name elimu. Wananchi wakipatiwa huduma sahihi kwa wakati hutakuja sikia mgomo wala maandamano na mwisho hakutakuwa na haja ya washawasha ..iletwe ya niini. Mataifa ya huko kwingine wananunua na kuboresha miundombinu ya kujilinda na maadui was nje ya nchi sio kutengeneza uadui na watu wake kama sisi.
 
Kumekuwa na mafanikio makubwa katika utoaji wa huduma za afya Hospitali ya Taifa Muhimbili. Kwamba sasa, wagonjwa wenye matatizo ya moyo wataweza kufanyiwa uchunguzi na kuweza kuhudumiwa kwa kuzibua mishipa inayopeleka damu kwenye moyo kwa mfumo wa kisasa zaidi.

Kwamba wagonjwa wenye matatizo hayo ya moyo, wataweza sasa kuzibuliwa matundu hayo kwenye moyo bila kufanyiwa upasuaji kifuani. Hii, kwa hakika ni habari njema, tena yenye kustahili kupongezwa.

Kwa mujibu wa taarifa kuhusu mafanikio haya, ni kwamba kufungwa kwa mtambo maalumu Hospitali ya Taifa Muhimbili, "Cath Lab" ndiko kutafanikisha huduma hizo muhimu katika maisha ya binadamu.

Kwa ufafanuzi tu ni kwamba, Cath Lab ni mtambo maalumu unaotumika kufanya uchunguzi, kuzibua mishipa inayopeleka damu kwenye moyo na kuziba matundu ya moyo bila kufanya upasuaji.

Kwa kuzingatia ukubwa wa magonjwa ya moyo nchini na gharama ambayo serikali na hata watu au taasisi binafsi zimekuwa zikiingia kusafirisha wagonjwa wa moyo kwa ajili ya kuokoa maisha yao kwa tiba za aina hii nje ya nchi, hakika, kwa kiasi kikubwa hatua hii itasaidia kuipa sura mpya sekta ya afya hapa nchini.

Tunajivunia wataalamu wetu nchini ambao tayari wameutumia mtambo huu kwa ufanisi mkubwa, kupitia Kitengo cha Tiba ya Moyo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, wakifanikiwa kufanya tiba ya moyo kwa kuziba matundu ya kwenye moyo bila kufanya upasuaji wa kifua.

Lakini si tu wataalamu wetu hapa nchini bali hata wenzao kutoka nje ya nchi ambao, kwa pamoja, wamefanikisha tiba hiyo, hao ni pamoja na madaktari bingwa kutoka Hospitali ya Prince Sultan Cardiac Centre ya Riyadh Saudi Arabia.

Tunaungana na Watanzania wengi katika kuamini kwamba hi ni hatua nyingine kubwa katika nyanja ya tiba na afya nchini baada ya kushuhudia ushirikiano wa aina hii na hospitali nyingine kadhaa za kimataifa kwa kutumia mifumo ya habari kama Video Conference ambayo huwawezesha madaktari kufanya upasuaji nchini kwa kushirikiana na madaktari bingwa wenzao walioko nje ya nchi.

Kuna madaktari wa ngapi wa kitanzania wanafanya upasuaji wa moyo? Inawezekana ikawa ile joint venture ya madaktari wa nje niliosikia kwenye radio, which would mean ni jambo la mda na limetokana na fadhila za hao madaktari siyo jitihada za serikali ya ccm.
 
Kuna ukiritimba wa hali ya juu sana MNH.. Hakuna fairness, rushwa ya vitu vidogo vidogo, fikiria kufata file tu toka block moja kwenda lingine mtu bado anatoa kidogo. Then unakuja kusema eti huduma zimeimarishwa..
 
Kuna vitu ambavyi huletwa na wakati,mambo haya ya technology ni gobal issue si ya ccm au chama fulan,...ni sawa na mtu atokee aseme ameleta simu za mkonon wakat hata ama kungekuwa na kilaza madarakani zingeingia tu maana ni upepo wa dunia nzima....kuna vitu ambavyo vikifanyika twaweza kumpa credit mhusika,mfano itokee tren zite ziwe za umeme bongo,kuwe na fly over kama 10 au 20 hiv dar nk,lkn vingine hivi mnaleta siasa tu! Hayo matibabu ya moyo mnayosifia yanafaa nini wakati watu wanateseka mawodini kwa ukosefu wa dawa tena zile za msingi? Imagine hospitali inakosa hata zile dawa za dhalura hslafu watu mnasifia tu
 
....exactly....mambo aliyokuwa anafanya dr. Masau (the late)miaka ya 2006 ndiyo wanatamba nayo sasa ccm....this is so sad....yaani kipindi kile walikua wanampiga zengwe Dr. Masau aliyekuwa anapambana kuyafanya haya wanayotamba nayo leo...alafu leo wanataka kuwapumbaza watanzania (kama kawaida yao)kwamba wanafanya mambo makuubwa...hii inashangaza sana....Ndio maana wanasema watanzania ni watu wa kusahau sana..maana watawala huwapumbaza kirahisi sana...Tena kipindi kile Dr. Masau alikua anafanya mpaka International conferences za Cardiac surgery (including tele conferences)...akiwahusisha mabingwa wa cardiology na cardio surgery kutoka pande mbalimbali za dunia....Alafu eti leo watawala wanawapumbaza wabongo eti wanafanya mambo haya ya ajabu!...kweli tuna safari ndefu....

...Hizi cardiac catheterization kwa wenzetu hufanywa routinely kama common procedures...Siasa za kibongo kweli zimeingilia taaluma....kila kitu kinahusishwa na siasa....

Good observations. Uelewa wetu umeshuka kiasi kwamba sasa unawanyima watu haki yao kwa kipindi kirefu, siku ukiwapa wanashukuru na kupiga magoti kama hawa.

Sasa hivi wanashukuru kwa mashine hospitali, barabara za rami na wengine hata kwa kupewa T-shirt na kofia.
 
Back
Top Bottom