Taasisi ya Mifupa-MOI
Senior Member
- Apr 15, 2025
- 118
- 211
Kwa muda mrefu, tiba ya kiharusi hapa nchini ilikuwa changamoto kubwa kutokana na ukosefu wa teknolojia ya kisasa ya kuchunguza na kutibu mishipa ya damu ya ubongo kwa haraka na kwa ufasaha.
Hali hiyo ilisababisha wagonjwa wengi kupoteza maisha au kubaki na ulemavu wa kudumu. Ujio wa mtambo wa kisasa wa Cathlab uliopo MOI umeleta mageuzi makubwa katika huduma za kibobezi na kuanza zama mpya za matibabu ya kiharusi nchini.
Akizungumzia mapinduzi hayo, leo Alhamis Januari 22, 2026 Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Mhe. Balozi Dkt. Mpoki Ulisubisya amesema mtambo huo umeongeza kwa kiwango kikubwa uwezo wa hospitali kuokoa maisha ya wagonjwa katika Taasisi hiyo na kuongeza ufanisi wa huduma kwani mtambo huo unawasaidia wataalam kujua tatizo lilipo tofauti na hapo nyuma walikuwa wakifanya upasuaji kwa kubahatisha.
"Miaka ya hivi karibuni tulikuwa hatuna namna ya kujua ni sehemu hasa ambazo zimepata matatizo... Lakini katika taasisi yetu (MOI), tuna wataalam ambao wamesoma na kubobea katika kutekeleza majukumu yao ya kutumia vifaa hivi vya kisasa mashine inayoitwa Cath Lab (Angio Suite)" amesema Dkt. Mpoki
Aidha, Dkt. Mpoki ametoa rai kwa Watanzania na watu wote wenye dalili za kiharusi kuwahi katika Taasisi hiyo kwa ajili ya kuchunguzwa ili kama kuna maeneo ya kurekebishwa yarekebishwe kabla ya kupata ulemavu wa kudumu.
Kwa upande wake, mtaalam kutoka Pennsylvania nchini Marekani, Prof. David Sacks amesema wameshirikiana na wataalam wa MOI katika kubadilishana uzoefu katika matumizi ya mtambo wa CathLab (Angio Suite) kwa kutumia mbinu za Kisasa kubaini kwa usahihi sehemu yenye tatizo kwenye mishipa ya damu ya ubongo.
Ameongeza kuwa ushirikiano huo umeongeza ufanisi wa uchunguzi na matibabu, kupunguza hatari ya ulemavu na vifo vitokanavyo na kiharusi, pamoja na kuwezesha wataalam wa ndani kufanya tiba hizo kwa viwango vya kimataifa.
Aidha, amesisitiza kuwa ushirikiano huo wa kitaalamu utaendelea ili kuhakikisha wagonjwa wengi zaidi wanapata huduma bora na za kisasa hapa nchini bila kulazimika kwenda nje ya nchi.