Muhimbili wamethubutu na wameweza

Muhimbili wamethubutu na wameweza

singidadodoma

JF-Expert Member
Joined
Nov 11, 2013
Posts
4,394
Reaction score
1,538
Kumekuwa na mafanikio makubwa katika utoaji wa huduma za afya Hospitali ya Taifa Muhimbili. Kwamba sasa, wagonjwa wenye matatizo ya moyo wataweza kufanyiwa uchunguzi na kuweza kuhudumiwa kwa kuzibua mishipa inayopeleka damu kwenye moyo kwa mfumo wa kisasa zaidi.

Kwamba wagonjwa wenye matatizo hayo ya moyo, wataweza sasa kuzibuliwa matundu hayo kwenye moyo bila kufanyiwa upasuaji kifuani. Hii, kwa hakika ni habari njema, tena yenye kustahili kupongezwa.

Kwa mujibu wa taarifa kuhusu mafanikio haya, ni kwamba kufungwa kwa mtambo maalumu Hospitali ya Taifa Muhimbili, "Cath Lab" ndiko kutafanikisha huduma hizo muhimu katika maisha ya binadamu.

Kwa ufafanuzi tu ni kwamba, Cath Lab ni mtambo maalumu unaotumika kufanya uchunguzi, kuzibua mishipa inayopeleka damu kwenye moyo na kuziba matundu ya moyo bila kufanya upasuaji.

Kwa kuzingatia ukubwa wa magonjwa ya moyo nchini na gharama ambayo serikali na hata watu au taasisi binafsi zimekuwa zikiingia kusafirisha wagonjwa wa moyo kwa ajili ya kuokoa maisha yao kwa tiba za aina hii nje ya nchi, hakika, kwa kiasi kikubwa hatua hii itasaidia kuipa sura mpya sekta ya afya hapa nchini.

Tunajivunia wataalamu wetu nchini ambao tayari wameutumia mtambo huu kwa ufanisi mkubwa, kupitia Kitengo cha Tiba ya Moyo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, wakifanikiwa kufanya tiba ya moyo kwa kuziba matundu ya kwenye moyo bila kufanya upasuaji wa kifua.

Lakini si tu wataalamu wetu hapa nchini bali hata wenzao kutoka nje ya nchi ambao, kwa pamoja, wamefanikisha tiba hiyo, hao ni pamoja na madaktari bingwa kutoka Hospitali ya Prince Sultan Cardiac Centre ya Riyadh Saudi Arabia.

Tunaungana na Watanzania wengi katika kuamini kwamba hi ni hatua nyingine kubwa katika nyanja ya tiba na afya nchini baada ya kushuhudia ushirikiano wa aina hii na hospitali nyingine kadhaa za kimataifa kwa kutumia mifumo ya habari kama Video Conference ambayo huwawezesha madaktari kufanya upasuaji nchini kwa kushirikiana na madaktari bingwa wenzao walioko nje ya nchi.
 
Tunashukuru kwa kutujuza na kila mwenye macho haambiwi tazama,
 
Aisee Wapinzani wamebeza nini sasa. Ungeelezea vizuri. Hilo ni jambo jema japo limechelewa sana kufikia nchi yetu. Ila vipi tathmini ya hali ya huduma za afya kwa Tanzania nzima? Maana naona serikali imefanikiwa sana kupandisha hadhi hospitali na sio kuongezea ufanisi majengo, vifaa tiba ni vile vile kasoro majina tu. Muhimbili bado sana katika moyo. Wataalam wachache mnoo. Ila tutafika kaka..
 
ndio wamethubutu wameweza je hiyo cath lab itamsaidia vip mwananchi wa kawaida? tunaona ni watanzania wangapi wenye hali za chini wanaoweza kumudu gharama za muhimbili? unadhani wote waliopo mwananyamala wanapenda kwenda kulundikana pale? ni pongezi kwa kuweza kufanikisha hilo ila usibeze upinzani kwa kuwa hilo bado halina manufaa ya moja kwa moja kwa watu wa kipato cha chini.
 
Na hizo bei mwazijua?? Kwa mtu wa hali ya chini ni mtihani
 
Haya waambie wale wananchi wa Lupeta, Mpwapwa(Dodoma) wanaotibiwa chini ya mti walioonyeshwa na ITV habari jana.
 
.............Kwamba sasa, wagonjwa wenye matatizo ya moyo wataweza kufanyiwa uchunguzi na kuweza kuhudumiwa kwa kuzibua mishipa inayopeleka damu kwenye moyo kwa mfumo wa kisasa zaidi.
..........................

Takataka! Miaka 54 ya uhuru leo ndo haya yanatangazwa! Tena unatibu kwa kusaidiwa na wayahudi! Niliyeko mtwara nije Dar es salaam kupanga foleni ya tiba?

Mwaka 2005 Dr Masau alipotangaza haya, mbona tuliona hao hao wanafiki wa Muhimbili wakijitokeza na kusema ni kinyume cha maadili kujitangaza? Leo hii unaleta tangazo lile lile ili iweje?

Walioanza ni THI Tanzania Heart Institute ya marehemu Masau.
 
ndio wamethubutu wameweza je hiyo cath lab itamsaidia vip mwananchi wa kawaida? tunaona ni watanzania wangapi wenye hali za chini wanaoweza kumudu gharama za muhimbili? unadhani wote waliopo mwananyamala wanapenda kwenda kulundikana pale? ni pongezi kwa kuweza kufanikisha hilo ila usibeze upinzani kwa kuwa hilo bado halina manufaa ya moja kwa moja kwa watu wa kipato cha chini.

Siku ukiugua utajua umuhimu wake
 
Siku ukiugua utajua umuhimu wake
ni wangapi wanashidwa kuhudumiwa muhimbili kwasababu hawana hela? kama hujjashuhudia mtu anarudishwa hom kisa hawezi kuaford cost za muhimbili sio mbaya ila kwa wale walioexperience hata kwa kuona tuu kwa jirani wanaelewa unachomaanisha
 
Aisee Wapinzani wamebeza nini sasa. Ungeelezea vizuri. Hilo ni jambo jema japo limechelewa sana kufikia nchi yetu. Ila vipi tathmini ya hali ya huduma za afya kwa Tanzania nzima? Maana naona serikali imefanikiwa sana kupandisha hadhi hospitali na sio kuongezea ufanisi majengo, vifaa tiba ni vile vile kasoro majina tu. Muhimbili bado sana katika moyo. Wataalam wachache mnoo. Ila tutafika kaka..

Hata kama iliyoletwa ni huduma nzuri umesahau kuwa serikali imetimiza wajibu wake sio hisani kwa watanzania. Na huenda imeweza kufanya hivyo kwa pressure toka opposition.
 
Naona kichwa cha habari na habari haviendani, Wapinzani ndio waliokuwa wanapiga kelele viongozi kwenda kutibiwa nje, madaktari kupiga dili kupitia tiba za nje, iweje leo wabeze,

Ha ha ha ha kwani Wapinzani ndo wamekarabati,kujenga na kuboresha hali hiyo au ni serikali ya CCM ndo imefanya vitu vyake?
 
ni wangapi wanashidwa kuhudumiwa muhimbili kwasababu hawana hela? kama hujjashuhudia mtu anarudishwa hom kisa hawezi kuaford cost za muhimbili sio mbaya ila kwa wale walioexperience hata kwa kuona tuu kwa jirani wanaelewa unachomaanisha

Wabunge wenu nyongeza ya posho hawakatai wewe unasema nini!kuboresha huduma ni jambo moja, kuchangia huduma ni jambo la pili! asiyefanya kazi asile, hakuna vitu vya bure siku hizi! Tusijenge taifa la mazezeta, huko CDM kwenyewe mnachangishwa fedha za kuendesha chama au unataka utibiwe bure?
 
Takataka! Miaka 54 ya uhuru leo ndo haya yanatangazwa! Tena unatibu kwa kusaidiwa na wayahudi! Niliyeko mtwara nije Dar es salaam kupanga foleni ya tiba?

Mwaka 2005 Dr Masau alipotangaza haya, mbona tuliona hao hao wanafiki wa Muhimbili wakijitokeza na kusema ni kinyume cha maadili kujitangaza? Leo hii unaleta tangazo lile lile ili iweje?

Walioanza ni THI Tanzania Heart Institute ya marehemu Masau.
Mkuu ni majanga, yahani taifa lenye
watu zaidi ya milioni 45 wanatumia ct-scan machines moja! huku mkiongeza idadi ya magari ya washa washa
 
Kwa kweli usimamizi wa rasilimali zetu ni duni sana kupitia serikali yetu. Kila mwenye udhubutu hushikwa mikono asisogee. Matumizi sahihi ya kodi zetu serikali haisimamii ipasavyo ndio maana tunakopa maendeleo tunatumia maingizo ya kodi. Hatutafika. Hakuna namna wananchi watahamasika kuchangia mpaka wa vitisho manyanyaso na bado michango yao hutumiwa vibaya na wanaosimamia...Hospital ya Taifa haina ubora hata wa hospital ya kufundishia katika nchi za asia..bado sana na kama tungekuwa makini sasa tungekuwa mbali ktk tasnia ya afya. Kinjekitile Junior..CCM haiwezi kusimamia mali asili zetu tukaboresha afya au hata miundombinu mingine.
 
Muhimbili operates on 66 heart patients in 7days.

Saves Sh1.3bn, Emerges strongest among EA public hospitals.
JK-Mtoto-16May2015%281%29.jpg

President Jakaya Kikwete visits six year-old Habiba Khalfan Lipande at Muhimbili National Hospital after surgeons successfully treated her by plugging a vent in her heart using the new technology which needs no open surgery. Habiba comes from Mavumba village in Morogoro Region. (Photo: Freddy Maro of State House)

The Cardiac Centre at the Muhimbili National Hospital (MNH) has succeeded in filling holes in patients' hearts by using a special device without opening up the chest as is usually done, medical reports at the MNH have confirmed.

Dr Hussein Kidanto, acting director general of the hospital, said that the use of special devices to treat heart ailments started last months, with 18 patients put to scanning on heart blood vessels and four being treated of blocked vessels.

A major treatment was to fill up a hole in the heart to allow blood vessels to reach a hole, which some infants are born with such a condition, he said.

In conducting those operations, specialist doctors at MNH worked with visiting heart specialists from the Prince Sultan Cardiac Centre in Riyadh, kingdom of Saudi Arabia, who paid a medical visit at the national facility from May 8 to 16, invited via the good offices of Muntanda Islamic Trust of Britain.

Soma zaidi: Home

Sasa sema uliyaona hayo kabla ya Kikwete? unajuwa ni nini hicho?

DSC03097.jpg

Back
Top Bottom