Muhimbili kuanza kupandikiza mimba mwaka 2020

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,403
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) nchini Tanzania itaanza kutoa huduma ya kupandikiza mimba kuanzia Januari mwaka 2020.​

Hayo yameelezwa leo Jumanne Novemba 19, 2019 na Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo, Profesa Lawrence Museru wakati akitoa taarifa ya mafanikio ya miaka minne ya MNH tangu Rais John Magufuli alipoapishwa kuwa kiongozi mkuu wa nchi.

“Tumeshapeleka wataalamu nchini India kuangalia namna ambavyo huduma ya upandikizaji mimba (IVF) inavyotolewa katika hospitali za umma, ni miundombinu na vifaa gani vinahitajika,” amesema Profesa Museru.

Amesema kwa sasa mainjinia wameanza kukarabati jengo katika hospitali hiyo litakaloanza kutumika kwa ajili ya kutoa huduma hiyo kabla ya jipya litakalojengwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili- Mloganzila.

“Ununuzi wa vifaa unafanyika na mipango imeanza, tayari wataalamu wameshatayarishwa, tunatarajia katika miezi miwili ijayo tutaanza rasmi kufanya upandikizaji,” amesema Profesa Museru.

Amesema huduma hiyo itakuwa ya kulipia, “tutataka watu wailipie hatujajua itagharimu kiasi gani, hiyo ni mpaka wataalamu watakapofanya maamuzi lakini asiyeweza kulipia pia tutaingia kwenye mfumo wa huduma za namna hiyo.”

Amesema katika kituo hicho zitatolewa huduma za kupandikiza figo, vifaa vya kusaidia kusikia, kupandikiza mimba, ini, uloto na maabara ya kujifunzia ujuzi.
 
Ni Jambo jema kwa wale wenye matatizo ya kutungisha mimba kiasili pia faida Ni nyingi hasa katika kuchagua mbegu (mapacha,jinsia nk), na uboreshaji wa mbegu za kiume.

Wasisahau haya mambo yanaenda mabadiliko ya Sheria hasa uraia, kuasili watoto na mirathi.
 
Hahaha...si mchezo
wanapoteza muda na hela bure..

Ajiri madume ya mbegu yasiyojulikana yakae pale iwe kazi kuwamwagia tu, ukimwagiwa unakwenda anaingia mwingine naye anamwagiwa kuna watu wanamatank ya mbegu..
 
Back
Top Bottom