Muhimbili hakuna umeme! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Muhimbili hakuna umeme!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Henge, Aug 26, 2011.

1. Henge

Henge JF-Expert Member

#1
Aug 26, 2011
Joined: May 14, 2009
Messages: 6,762
Likes Received: 78
Trophy Points: 145
Ndo natoka hapa muhimbili kumwona mgojwa huwezi kuamini hakuna umeme,
na generator yao ni mbovu, sijui inakuwaje ndo maana wakinamwandosya wanaenda India!
hii nchi watu wanaofikilia ni wachache sana inakuwaje umeme unakatwa na generator haifanyi kazi
tena sehemu muhimu kama hii ni bora ungekatika ikulu,

2. Viper

Viper JF-Expert Member

#2
Aug 26, 2011
Joined: Dec 21, 2007
Messages: 3,665
Likes Received: 44
Trophy Points: 145
hii hatari ! sasa wale wagonjwa wa ICU unakuwaje..?!

3. s

sweke34 JF-Expert Member

#3
Aug 26, 2011
Joined: Sep 28, 2010
Messages: 2,533
Likes Received: 10
Trophy Points: 135
yaani Ngeleja anapita hata muhimbili!!

4. M

Mrdash1 JF-Expert Member

#4
Aug 26, 2011
Joined: Sep 21, 2010
Messages: 1,379
Likes Received: 6
Trophy Points: 0
wewe kwa nini unasikitishwa na muhimbili tuu?? vipi hospitali za mikoa, wilaya, vituo vya afya vya kata, dispensary za vijiji????????? au unafikiri binadamu wanaishi dar es salaam peke yake? CCM na M kwere wao ni maafa ya taifa siyo ya muhimbili peke yake

5. Glue

Glue Senior Member

#5
Aug 26, 2011
Joined: Jan 14, 2011
Messages: 123
Likes Received: 10
Trophy Points: 35
Sio umeme tu, hata maji hakuna. Me nina jamaa yangu kalazwa takribam 3days now. Hakuna maji na wagonjwa hawaruhusiwi kuingia vyooni. Amakweli ukistahajabu ya Musa..!

6. Goheki

Goheki JF-Expert Member

#6
Aug 26, 2011
Joined: Aug 23, 2011
Messages: 270
Likes Received: 0
Trophy Points: 33
Ngeleja bado anesukuma gari la Jairo,hilo la mwimbili halimuhusu,kwani baada ya furaha masaa,sasa anamawazo ya jinsi ya kuadhibu idara ambazo hazikuchangia bajeti.

7. pangalashaba

pangalashaba JF-Expert Member

#7
Aug 26, 2011
Joined: Jan 10, 2011
Messages: 1,075
Likes Received: 855
Trophy Points: 280

so mkuu kwa sasa tunayaona ya firauni,ndo nani hapa nchini kwetu? tujuze tumjue huyo firauni wetu...

8. Kiby

Kiby JF-Expert Member

#8
Aug 26, 2011
Joined: Nov 16, 2009
Messages: 5,197
Likes Received: 1,003
Trophy Points: 280
Mimi nawaomba watanzania wote wachamungu Muombeni Mungu kwa bidii sana. Taifa letu limechafuliwa lugha tayairi, hakuna tena kuelewana. Serikali imenyanganywa ufahamu, utu umeondoka. Hebu fikiria kuna watu wanaoitwa waheshimiwa nyumbani kwao haijawahi ikitokea kukakatwa umeme. Lakini hospitali kuu ya taifa yenye nafsi nyingi za watoto, wamama na watu wa aina zote wanaopigania uhai wao wanakatiwa umeme na maji. Tuliwakataa wafanya biashara ya watumwa zamani zile. Sasa kuna tofauti gani ya utumwa huu tunaofanyiwa na ndugu zetu wenyewe na wale wakoloni weupe? Ni lini Tanzania tutapata uhuru? Na ni nini tunapaswa kikiondoa miongoni mwetu kuukaribisha uhuru wetu katika nchi yetu wenyewe? Waziri wa afya amepelekwa nje ya nchi kutibiwa, lakini chunguzeni kama hamtakuta pesa ile aliyokwishatumia mtwana huyu kama haizidi pesa ya kutengeneza genereta la pale Muhimbili.
HII NI LAANA, TAIFA HILI TUMEKABIZIWA KWA MUNGU MGENI, HEBU BASI TUUNGAME NA KUMREGELEA MUNGU MUUMBA MBINGU NA NCHI ILI ATUREJESHEE FAHAMU ZETU ZILIZOPORWA. SASA HIVI SISI SOTE TU MISUKULE NA HATA HATUJITAMBUI.

9. m

mikogo Senior Member

#9
Aug 27, 2011
Joined: Jul 24, 2011
Messages: 175
Likes Received: 4
Trophy Points: 35
hili la MNH kukosa umeme na generator kukosa mafuta au kuwa mbovu ni suala la menejimenti ya hapo MNH. ukweli wa nini kinachoendelea tuwadai wao na mamlaka za juu tuzidai hukumu ya wahusika wa kadhia hii na sisi hapa jamvini tusiwe wepesi wa ulalamishi. tushauri pasipo na jazba.

10. measkron

measkron JF-Expert Member

#10
Aug 27, 2011
Joined: Apr 11, 2011
Messages: 3,713
Likes Received: 365
Trophy Points: 180

Sio MNH tu mkuu! Mie nafanya kazi mkoani hapa hospitali mgao wa umeme kama kawaida, generator dogo, bovu. Pesa za mafuta na matengenezo ni zile zile za cost sharing! Kununua dawa hapo hapo kwani fedha ya MSD mara nyingi haitoshelezi. Swali linakuja, tuache kununua dawa tununue magenerator makubwa na mafuta? Serikali ilaumiwe na sio hospitali.

11. Desteo

Desteo JF-Expert Member

#11
Aug 27, 2011
Joined: Jul 27, 2011
Messages: 446
Likes Received: 7
Trophy Points: 35
Kuna taarifa ambazo huwa zinachacha. Kwani hadi muda huu hamna umeme?

12. Jackbauer

Jackbauer JF-Expert Member

#12
Aug 27, 2011
Joined: Oct 28, 2010
Messages: 5,920
Likes Received: 89
Trophy Points: 145
hayo ndiyo mazingira halisi ya hospitali za kitanzania

13. S

SALOS Member

#13
Aug 28, 2011
Joined: Aug 27, 2011
Messages: 26
Likes Received: 1
Trophy Points: 0
Mnalalamika sana watu, mkiambiwa mchange pesa ili wanunue majenereta makubwa ili kupunguza tatizo mtakubali? Chamsingi hao mafisadi watoe hayo madola walojaza kwenye account zao wanunue majenerata. Kuhusu maji,wachimbe hata visima kama dawasco wanazingua

14. Shine

Shine JF-Expert Member

#14
Aug 28, 2011
Joined: Feb 5, 2011
Messages: 11,514
Likes Received: 16
Trophy Points: 0

Kweli mkuu bora ikulu kwani wagonjwa bila umeme hawawezi kufanyiwa vipimo

15. Shine

Shine JF-Expert Member

#15
Aug 28, 2011
Joined: Feb 5, 2011
Messages: 11,514
Likes Received: 16
Trophy Points: 0

jamaa kasema muhimbili kwasababu ni tatizo aliloliona kwa macho yake huko kwingine ndo nyie mlioko huko mtujuze

16. Rweye

Rweye JF-Expert Member

#16
Aug 28, 2011
Joined: Mar 16, 2011
Messages: 15,029
Likes Received: 3,052
Trophy Points: 280
Nadhani bunge kuisha kinachofata tusubiri mgao mkuu wa karne,kwa kuanza tu leo mikoa ya kanda ya ziwa toka saa12 asubuhi hapakuwepo na umeme mpaka saa3 za usiku,tusubiri tuone

17. Mamndenyi

Mamndenyi JF-Expert Member

#17
Aug 29, 2011
Joined: Apr 11, 2011
Messages: 29,046
Likes Received: 6,492
Trophy Points: 280
Muhimbili last week hakukuwa na umeme, maiti zilishindikana kushushwa kutoka ghorofani ili zikahifaziwe, ukiwa na mgonjwa wodini jioni ni lazima uende na tochi ya kumtafuta, na kero nyingine za aibu zilijiri kwenye ile hosp. kuu ya taifa; je tz inakwenda wapi.

Loading...