Mugabe; Baba wa Taifa aliyemaliza vibaya

Rlechas_3a60

Member
Oct 4, 2018
12
27
Mwili wa aliyekuwa rais wa kwanza wa Zimbabwe, Robert Mugabe umehifadhiwa katika eneo ambalo alizaliwa, baada ya juzi kuagwa katika mji mkuu wa Harare, katika hafla iliyoshuhudiwa na watu kiduchu tofauti na mchango wake, ukongwe wake kwa taifa hilo.

Wakati wa kutoa heshima za mwisho, viongozi wa Afrika walitumia fursa hiyo kumsifu Mugabe, kama mpiganiaji wa Uhuru katika mazishi yake katika uwanja wa kitaifa mjini Harare.

Mrithi wake, Emmerson Mnagagwa alimtaja Mugabe kama kiongozi aliyekuwa na maono na kusema kwamba 'taifa letu linalia.

Hata hivyo, uwanja wa Taifa wenye uwezo wa kubeba watu 60,000, ulikuwa na idadi ndogo ya watu tofauti na ilivyotarajiwa na wengi.

Kwa upande mwingine, uchumi wa taifa hilo upo katika hali mbaya na raia wengi wa Zimbabwe waliamua kususia sherehe hiyo kutokana na ukandamizaji uliotekelezwa na uongozi wa Mugabe.

Kupanda kwa hali ya mfumuko na ukosefu wa ajira, ni baadhi ya masuala ambayo yamewafanya raia wa taifa hilo kumlaumu Mugabe.

''Tunafurahia, amefariki, kwa nini nihudhurie mazishi yake? sina mafuta,'' alisema mkazi mmoja wa Harare akizungumza na AFP.

''Hatutaki kusikia chochote kumuhusu tena. Yeye ndio sababu ya matatizo yetu''

Hata hivyo, mazishi yake yatafanyika baada ya mgogoro kati ya familia ya Mugabe na serikali kuhusu mahala atakapozikwa uliohitimishwa kwa makubaliano kuwa atazikwa katika makaburi ya mashujaa mjini Harare, familia yake imesema.

Jana, Msemaji wa familia na mpwa wake, alisema mwili wa Mugabe utazikwa baada ya kipindi cha mwezi mmoja wakati ambapo kaburi hilo litajengwa katika makaburi hayo ya mashujaa.

Mugabe ambaye alikuwa na umri wa miaka 95 alipofariki wiki iliopita alikuwa akitibiwa nchini Singapore.

Kulikuwa na jua na raia wachache walikwenda kutoa heshima za mwisho kwa kiongozi huyo.

Nje ya hayo, viongozi wa nchi za Afrika, wakiwo wastaafu waliingia katika uwanja huo kwa shangwe kubwa pamoja na viongozi waliopigania uhuru wa bara hili.

Rais Mnangagwa, kiongozi aliyempindua Mugabe miaka miwili iliopita, aliketi viti viwili karibu na mkewe Mugabe Grace.

Sifa za Mugabe kama mpiganiaji uhuru zilitolewa na kila kiongozi ambaye alisimamna kuhutubia akiwemo rais wa Kenya Uhuru Kenyatta.

Walitoautiana na maneno yaliotolewa na mwakilishi wa familia hiyo Walter Chidhakwa aliyesema ''Mugabe alikuwa na huzuni, huzuni mkubwa,' Ilikuwa safari ngumu na ya kuchukiza.''

Matamashi yake yalionyesha wazi wasiwasi uliopo kati ya serikali iliopo na familia ya Mugabe.

Zaidi ya viongozi kumi wakiwemo wale wa zamani wa mataifa ya Afrika, walihudhuria mazishi hayo, wakimsifu Mugabe kama kiongozi wa Afrika aliyeamua kutumikia maisha yake yote kwa raia wa Zimbabwe.

Kwa upande wake Rais Kenyatta, alisisitiza kwamba matatizo ya Kiafrika yanahitaji suluhu ya kiafrika.

Baadae raia wallimzomea rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa ikionekana kuwa jibu la ghasia dhidi ya wageni nchini kwake katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita.

Hata hivyo, alitambua kelele hizo kwa kusema: "Katika wiki mbili zilizopita, sisi Waafrika Kusini tumekuwa tukikabiliwa na wakati mgumu.

Tumekuwa na vitengo vya ghasia katika baadhi ya maeneo ya Afrika Kusini...hili limesababisha kama ninavyowasikia mukisema ... vifo na majeraha miongoni mwa idadi ya watu. lakini alisisitiza sisi Waafrika wa Kusini hatupendi ghasia dhidi ya wageni"

Mwaka 1980, Mugabe alishinda uchaguzi na kuwa waziri mkuu. Mwaka 1982 aliushutumu upinzani kwa kujaribu kupindua serikali.

Maelfu ya watu waliuawa alipolituma jeshi lake lililopata mafunzo Korea Kaskizini, kuwakandamiza maadui zake.

Mwaka 1987,alibadilisha katiba ili imruhusu kuwa rais na kuongeza mamlaka yake huku uchumi wa nchi hiyo ulianza kudorora baada ya mwaka 2000,
Wakati Mugabe aliagiza kunyakua mashamba yaliomilikiwa na watu weupe yaliyokuwa kinara katika uchumi.

Mfumuko wa bei ulipelekea sarufi ya taifa kuwa bila thamani na hali nchini humo ikazidi kudororeka.

Baada ya uchaguzi wa mwaka 2008, Mugabe alilazimika kugawanya mamlaka na kiongozi wa upinzani Morgan Tsvangirai.

Japo kulikuwa na ghasia dhidi ya wafuasi wa Tsvangirai katika kampeni za uchaguzi.

Ndoa yake na Grace Mugabe anayemzidi kwa maika 40, inahisiwa ndio ilimponza kwani wengi walikasirishwa kuandaliwa kuwa mrithi wake.
Wakati akiwa madarakani, Mugabe aliwahi kuapa ya kuwa Mungu pekee ndio angeweza kumtoa madarakani.
 
1568613090104.jpeg

1568615032172.jpeg

Hizi ndiyo siku nilizompenda Mugabe
 
Toa akili za kibeberu hapa

Hao wazimbabwe hawana shukran mzee aliwapokonya wazungu ardhi akawapa wazawa bado wanamdhihaki hawajui matatizo yalianza baada ya mugabe kuchukua ardhi?
 
Umeshafika Zimbabwe Mkuu kwa hakika kule hali ya maisha ni ngumu sana na Wazimbabwe wengi hawampendi wanaona kama yeye ndio amewasababishia hali hiyo
 
Toa akili za kibeberu hapa

Hao wazimbabwe hawana shukran mzee aliwapokonya wazungu ardhi akawapa wazawa bado wanamdhihaki hawajui matatizo yalianza baada ya mugabe kuchukua ardhi?
Dhuluma mbaya kwani hao wazungu ni raia wa wapi?hawana tofauti na makaburu waSA
Walikaa karne nyingi mpaka wakapoteza uasili angekaa nao wangesalimisha portion tu
 
Sorry you know nothing about land aquistion in Zimbabwe
Google it at least you can learn something
Dhuluma mbaya kwani hao wazungu ni raia wa wapi?hawana tofauti na makaburu waSA
Walikaa karne nyingi mpaka wakapoteza uasili angekaa nao wangesalimisha portion tu
 
Mwili wa aliyekuwa rais wa kwanza wa Zimbabwe, Robert Mugabe umehifadhiwa katika eneo ambalo alizaliwa, baada ya juzi kuagwa katika mji mkuu wa Harare, katika hafla iliyoshuhudiwa na watu kiduchu tofauti na mchango wake, ukongwe wake kwa taifa hilo.

Wakati wa kutoa heshima za mwisho, viongozi wa Afrika walitumia fursa hiyo kumsifu Mugabe, kama mpiganiaji wa Uhuru katika mazishi yake katika uwanja wa kitaifa mjini Harare.

Mrithi wake, Emmerson Mnagagwa alimtaja Mugabe kama kiongozi aliyekuwa na maono na kusema kwamba 'taifa letu linalia.

Hata hivyo, uwanja wa Taifa wenye uwezo wa kubeba watu 60,000, ulikuwa na idadi ndogo ya watu tofauti na ilivyotarajiwa na wengi.

Kwa upande mwingine, uchumi wa taifa hilo upo katika hali mbaya na raia wengi wa Zimbabwe waliamua kususia sherehe hiyo kutokana na ukandamizaji uliotekelezwa na uongozi wa Mugabe.

Kupanda kwa hali ya mfumuko na ukosefu wa ajira, ni baadhi ya masuala ambayo yamewafanya raia wa taifa hilo kumlaumu Mugabe.

''Tunafurahia, amefariki, kwa nini nihudhurie mazishi yake? sina mafuta,'' alisema mkazi mmoja wa Harare akizungumza na AFP.

''Hatutaki kusikia chochote kumuhusu tena. Yeye ndio sababu ya matatizo yetu''

Hata hivyo, mazishi yake yatafanyika baada ya mgogoro kati ya familia ya Mugabe na serikali kuhusu mahala atakapozikwa uliohitimishwa kwa makubaliano kuwa atazikwa katika makaburi ya mashujaa mjini Harare, familia yake imesema.

Jana, Msemaji wa familia na mpwa wake, alisema mwili wa Mugabe utazikwa baada ya kipindi cha mwezi mmoja wakati ambapo kaburi hilo litajengwa katika makaburi hayo ya mashujaa.

Mugabe ambaye alikuwa na umri wa miaka 95 alipofariki wiki iliopita alikuwa akitibiwa nchini Singapore.

Kulikuwa na jua na raia wachache walikwenda kutoa heshima za mwisho kwa kiongozi huyo.

Nje ya hayo, viongozi wa nchi za Afrika, wakiwo wastaafu waliingia katika uwanja huo kwa shangwe kubwa pamoja na viongozi waliopigania uhuru wa bara hili.

Rais Mnangagwa, kiongozi aliyempindua Mugabe miaka miwili iliopita, aliketi viti viwili karibu na mkewe Mugabe Grace.

Sifa za Mugabe kama mpiganiaji uhuru zilitolewa na kila kiongozi ambaye alisimamna kuhutubia akiwemo rais wa Kenya Uhuru Kenyatta.

Walitoautiana na maneno yaliotolewa na mwakilishi wa familia hiyo Walter Chidhakwa aliyesema ''Mugabe alikuwa na huzuni, huzuni mkubwa,' Ilikuwa safari ngumu na ya kuchukiza.''

Matamashi yake yalionyesha wazi wasiwasi uliopo kati ya serikali iliopo na familia ya Mugabe.

Zaidi ya viongozi kumi wakiwemo wale wa zamani wa mataifa ya Afrika, walihudhuria mazishi hayo, wakimsifu Mugabe kama kiongozi wa Afrika aliyeamua kutumikia maisha yake yote kwa raia wa Zimbabwe.

Kwa upande wake Rais Kenyatta, alisisitiza kwamba matatizo ya Kiafrika yanahitaji suluhu ya kiafrika.

Baadae raia wallimzomea rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa ikionekana kuwa jibu la ghasia dhidi ya wageni nchini kwake katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita.

Hata hivyo, alitambua kelele hizo kwa kusema: "Katika wiki mbili zilizopita, sisi Waafrika Kusini tumekuwa tukikabiliwa na wakati mgumu.

Tumekuwa na vitengo vya ghasia katika baadhi ya maeneo ya Afrika Kusini...hili limesababisha kama ninavyowasikia mukisema ... vifo na majeraha miongoni mwa idadi ya watu. lakini alisisitiza sisi Waafrika wa Kusini hatupendi ghasia dhidi ya wageni"

Mwaka 1980, Mugabe alishinda uchaguzi na kuwa waziri mkuu. Mwaka 1982 aliushutumu upinzani kwa kujaribu kupindua serikali.

Maelfu ya watu waliuawa alipolituma jeshi lake lililopata mafunzo Korea Kaskizini, kuwakandamiza maadui zake.

Mwaka 1987,alibadilisha katiba ili imruhusu kuwa rais na kuongeza mamlaka yake huku uchumi wa nchi hiyo ulianza kudorora baada ya mwaka 2000,
Wakati Mugabe aliagiza kunyakua mashamba yaliomilikiwa na watu weupe yaliyokuwa kinara katika uchumi.

Mfumuko wa bei ulipelekea sarufi ya taifa kuwa bila thamani na hali nchini humo ikazidi kudororeka.

Baada ya uchaguzi wa mwaka 2008, Mugabe alilazimika kugawanya mamlaka na kiongozi wa upinzani Morgan Tsvangirai.

Japo kulikuwa na ghasia dhidi ya wafuasi wa Tsvangirai katika kampeni za uchaguzi.

Ndoa yake na Grace Mugabe anayemzidi kwa maika 40, inahisiwa ndio ilimponza kwani wengi walikasirishwa kuandaliwa kuwa mrithi wake.
Wakati akiwa madarakani, Mugabe aliwahi kuapa ya kuwa Mungu pekee ndio angeweza kumtoa madarakani.
Msaada Mkuu hivi nani au nini tafsir ya Baba wa Taifa?

Kama inamaanisha Rais wa Kwanza wa nchi toka ukolone KICHWA CHA HABARI KIBADILISHWE kwa kuwa Rais wa Kwanza wa Zimbabwe huru April 1980.

Rais wao wa Kwanza alikua Basha mmoja mchungaji wa dhehebu la Methodist Minister Prof. Canaan Sodindo Banana 1980-1987.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom