Mufti ataka Waislamu kuwekeza katika elimu zaidi

Status
Not open for further replies.
Mkuu kuna mambo na mipaka ya waziri, Rais, katibu kata. Unapodai MOU hii ilisainiwa na Waziri Lowassa, na Rais Muislamu, Mkuu wa Usalama wa Taifa Muislamu hebu tupatie evidence kama kweli wamesign. Au nawewe unakuwa kama jamaa mmoja anayejiita katibu TEC. We are anxious to know what realy went there!!!!.

Mkuu kuanzishwa tangia zamani hakumaanishi ndio zitolewe favourable terms from the government JK. Kumbuka hawa viongozi walitakiwa wawe na weledi wa kujua hii nchi ina waislamu, wakristo, wapagani, wahindu sasa tukisema tuwape favorable terms wakristo tu wahindi nao wasemeje? Unadhani zile shule za upanga, muhimbili na kisutu walijenga serikali? Wamejenga wahindi kipindi cha mkoloni sasa basi nao wapewe favourable terms kusaidia jamii.

Mkuu huwezi kuepuka kwani data zinaonyesha hizi seminari zilishamiri miaka ya 90 sasa kama MOU ilisaidia au la nakuachia wewe umalizie ila sidhani kama ni mada. Swala ni je huyu mufti anachokisema kina msingi.

Binafsi silaumu kila kitu serikali ni vema waislamu nao wakawa na moyo wa kusaidia. Kuna waislamu matajiri mno Tanzania ila utajiri wao unatumika katika siasa, kujionyesha, kuhonga akina dada, na ni wachache sana hutumia utajiri wao kuendeleza jamii. Vile vile jamii za kiislamu ni vema zikawa na mwamko wa kusoma kwa serikali haitaweza kufanya kila kitu. Sio lazima aje tajiri kuja kusaidia waislam, wenyewe kwa wenyewe wanaweza kuchangishana kufanya kitu cha msingi. Ila jambo moja waislamu linawarudisha nyuma nalo roho ya kutoa, yaani wengi wana roho ya kwanini nitoe mie sasa mioyo ya kutoa hawana.

Hivyo JK silaumu kila kitu serikali ila there is a share serikali lazima ibebe katika haya mambo kwani ile divide and rule iliyoanzia kipindi cha nyerere inaendelea mpaka sasa.
Mkuu hiyo MOU ina-apply kwa dini zoote hata kama Waislam leo hii wanataka kujenga hospitali, shule au chuo wanapata treatment sawa kama ndg zao Wakristo yaani kodi za vifaa vya ujenzi husamehewa na pia serikali huwajibika kusaidia katika uendeshaji yaani kuchangia kiasi cha budget na kulipa mishahara ya baadhi ya wafanyakazi haswa mahospitalini! Mfano Aga Khan institutions (Ismaili Islamic denomination) wanapata hizi benefits wanapowekeza katika vyuo vyao hata na kile wanachojenga sasa Arusha tukiacha mbali academies zao!
 
Mdondoaji said:
Mkuu kuna mambo na mipaka ya waziri, Rais, katibu kata. Unapodai MOU hii ilisainiwa na Waziri Lowassa, na Rais Muislamu, Mkuu wa Usalama wa Taifa Muislamu hebu tupatie evidence kama kweli wamesign. Au nawewe unakuwa kama jamaa mmoja anayejiita katibu TEC. We are anxious to know what realy went there!!!!.

Mkuu kuanzishwa tangia zamani hakumaanishi ndio zitolewe favourable terms from the government JK. Kumbuka hawa viongozi walitakiwa wawe na weledi wa kujua hii nchi ina waislamu, wakristo, wapagani, wahindu sasa tukisema tuwape favorable terms wakristo tu wahindi nao wasemeje? Unadhani zile shule za upanga, muhimbili na kisutu walijenga serikali? Wamejenga wahindi kipindi cha mkoloni sasa basi nao wapewe favourable terms kusaidia jamii.

Mdondoaji,

..off course kuna mipaka ya utendaji kati ya Raisi,Mawaziri, etc etc.

..lakini vilevile Mawaziri wanateuliwa na Raisi. sasa aliyemtuma Makinda na baadaye Lowassa kujadiliana na makanisa na maofisa wa ubalozi mpaka kufikia kusainiwa kwa hii MOU ni nani?

..kama Raisi Alhaji Mwinyi alikuwa hakubaliani na MOU basi alikuwa na mamlaka ya kumfukuza kazi Lowassa, pamoja na kusitisha utekelezwaji wa MOU hiyo.

..pia MOU ilikuwa inahusisha sekta zaidi ya moja, particularly AFYA na ELIMU. kwa msingi huo mchakato wa MOU ulihusisha watendaji wa serikali wa wizara za Afya na Elimu ambazo kwa wakati huo ama zilikuwa na Mawaziri Waislamu au Makatibu wakuu Waislamu.

..wizara ya Fedha ambako mnadai pesa zimekuwa zikichotwa pia ilikuwa chini ya Muislamu swaafi kabisa Alhaji Prof.Dr.Kighoma Ali Malima.

..the fact kwamba maofisa wa ubalozi wa nchi kama Ujerumani walishiriki ktk mchakato ina maanisha kwamba Wizara ya Mambo ya Nje ilikuwa na taarifa. sasa pale Foreign miaka ya 90 waziri alikuwa Ahmed Diria, na PS wake alikuwa Dr.Idris Msabaha.

..mwisho, Baraza Kuu la Waislamu Tanzania[BAKWATA] walishiriki kama OBSERVERS wakati wa mchakato uliopelekea kusainiwa kwa MOU.

..sasa ktk mazingira hayo kwanini umlaumu Lowassa peke yake badala ya serikali nzima ya wakati MOU inasainiwa iliyoongozwa na Alhaji Ali Hassan Mwinyi?

..naelewa kwamba kuna shule za madhehebu yasiyo ya Kikristo ambazo zilitaifishwa na Mwalimu Nyerere. lakini aliyechukua uamuzi wa kuzirejesha shule hizo ni Alhaji Ali Hassan Mwinyi? sasa kama ni lawama zielekezwe kwa Alhaji Mzee Mwinyi kwamba kwanini alirejesha hosteli za Agha Khan lakini akaendelea kushikilia shule[Tambaza,Zanaki,Muhimbili] ,au kwanini hakurejesha shule za Kisutu, Minaki[st.Andrew],Pugu[st.Francis],Mazengo[alliance boys], Ilboru etc etc??

..mwisho, Raisi Kikwete, Makamu Dr.Bilal, Mustapha Mkulo, Ramadhani Kijjah[wizara ya fedha], Prof.Jumanne Maghembe, Prof.Ramadhani Dihenga[wizara ya elimu], hawa wote wanashindwa nini kutenda haki kwa Waislamu na hao Mabohora na Mabaniani ambao shule zao bado zinashikiliwa na serikali? au nini kinawazuia kusitisha utekelezwaji wa MOU?

..binafsi nadhani Waislamu wangeacha kulaumu na kushutumu, badala yake wakajielekeza kwenye kutafuta suluhu ya matatizo yao, hali yao ingekuwa na unafuu, na huu mpasuko wa kidini usingekuwepo.

NB:

..moja ya ahadi za uchaguzi za JK ni kuzipandisha daraja baadhi ya hospitali kuwa za Rufaa. kati ya hospitali hizo zipo hospitali za mishen.
 
Mkuu hiyo MOU ina-apply kwa dini zoote hata kama Waislam leo hii wanataka kujenga hospitali, shule au chuo wanapata treatment sawa kama ndg zao Wakristo yaani kodi za vifaa vya ujenzi husamehewa na pia serikali huwajibika kusaidia katika uendeshaji yaani kuchangia kiasi cha budget na kulipa mishahara ya baadhi ya wafanyakazi haswa mahospitalini! Mfano Aga Khan institutions (Ismaili Islamic denomination) wanapata hizi benefits wanapowekeza katika vyuo vyao hata na kile wanachojenga sasa Arusha tukiacha mbali academies zao!

Hebu tupatie basi MOU ya Jumuiya za Kiislamu na Serikali ya Tanzania. Hatutaki hekaya za kusadikika. Aga Khan unasema wanapata hizi benefits kwanza misamaha ya kodi kwa taasisi za kidini kwa sasa imefutwa huoni kama unatudanganya ndugu!!!! Au ndio yale maneno ya X-Paster alikwambia huna haja ya kulazimisha kuwa muislamu.
 
Mdondoaji,

..off course kuna mipaka ya utendaji kati ya Raisi,Mawaziri, etc etc.

..lakini vilevile Mawaziri wanateuliwa na Raisi. sasa aliyemtuma Makinda na baadaye Lowassa kujadiliana na makanisa na maofisa wa ubalozi mpaka kufikia kusainiwa kwa hii MOU ni nani?

..kama Raisi Alhaji Mwinyi alikuwa hakubaliani na MOU basi alikuwa na mamlaka ya kumfukuza kazi Lowassa, pamoja na kusitisha utekelezwaji wa MOU hiyo.

..pia MOU ilikuwa inahusisha sekta zaidi ya moja, particularly AFYA na ELIMU. kwa msingi huo mchakato wa MOU ulihusisha watendaji wa serikali wa wizara za Afya na Elimu ambazo kwa wakati huo ama zilikuwa na Mawaziri Waislamu au Makatibu wakuu Waislamu.

..wizara ya Fedha ambako mnadai pesa zimekuwa zikichotwa pia ilikuwa chini ya Muislamu swaafi kabisa Alhaji Prof.Dr.Kighoma Ali Malima.

..the fact kwamba maofisa wa ubalozi wa nchi kama Ujerumani walishiriki ktk mchakato ina maanisha kwamba Wizara ya Mambo ya Nje ilikuwa na taarifa. sasa pale Foreign miaka ya 90 waziri alikuwa Ahmed Diria, na PS wake alikuwa Dr.Idris Msabaha.

..mwisho, Baraza Kuu la Waislamu Tanzania[BAKWATA] walishiriki kama OBSERVERS wakati wa mchakato uliopelekea kusainiwa kwa MOU.

..sasa ktk mazingira hayo kwanini umlaumu Lowassa peke yake badala ya serikali nzima ya wakati MOU inasainiwa iliyoongozwa na Alhaji Ali Hassan Mwinyi?

..naelewa kwamba kuna shule za madhehebu yasiyo ya Kikristo ambazo zilitaifishwa na Mwalimu Nyerere. lakini aliyechukua uamuzi wa kuzirejesha shule hizo ni Alhaji Ali Hassan Mwinyi? sasa kama ni lawama zielekezwe kwa Alhaji Mzee Mwinyi kwamba kwanini alirejesha hosteli za Agha Khan lakini akaendelea kushikilia shule[Tambaza,Zanaki,Muhimbili] ,au kwanini hakurejesha shule za Kisutu, Minaki[st.Andrew],Pugu[st.Francis],Mazengo[alliance boys], Ilboru etc etc??

..mwisho, Raisi Kikwete, Makamu Dr.Bilal, Mustapha Mkulo, Ramadhani Kijjah[wizara ya fedha], Prof.Jumanne Maghembe, Prof.Ramadhani Dihenga[wizara ya elimu], hawa wote wanashindwa nini kutenda haki kwa Waislamu na hao Mabohora na Mabaniani ambao shule zao bado zinashikiliwa na serikali? au nini kinawazuia kusitisha utekelezwaji wa MOU?

..binafsi nadhani Waislamu wangeacha kulaumu na kushutumu, badala yake wakajielekeza kwenye kutafuta suluhu ya matatizo yao, hali yao ingekuwa na unafuu, na huu mpasuko wa kidini usingekuwepo.

NB:

..moja ya ahadi za uchaguzi za JK ni kuzipandisha daraja baadhi ya hospitali kuwa za Rufaa. kati ya hospitali hizo zipo hospitali za mishen.

Joka Kuu,

Kwa kweli hujanishawishi bado maneno unayozungumza kwasababu kwanza kwanini basi kama misamaha ya kodi navyofahamu mie ni wizara ya fedha inatoa basi asisign bwana Alhaj Professa Kighoma Ali Malima amekuja kusign mzee wa kanisa Mh Edward Lowassa? Pili unasema kuwa Mzee Mwinyi ndie aliyeruhusu nadhani mnamuonea wapi ameshiriki??? Na mzee mwinyi kutokumfukuza nadhani inategemea yeye alivyo ila ningelikuwa mie rais Mh Lowassa angelikuwa hana tena nafasi ya uwaziri maana serikali ya tanzania haina dini.

For your information aliyekuja kuigundua hiyo MOU ni huyo huyo mwislamu safiii!!! . Mmungu amrehemu. Sasa jiulize kwanini aliiilipua??? Tusidanganyane Joka Kuu kulalamika waislamu watalalamika mpaka ndugu zangu wakristo muache ubinafsi.
 
Sasa naanza kuelewa ni kwa nini mnagombana wenyewe, mnapingana wenyewe, mnagombania misikiti wakati ni nyumba za ibada............KUMBE KILA MTU NI KIONGOZI.

Yani kila mtu ni :msela::msela::msela::msela:TUUUUU!!!!
Wenyewe akina nani? Usidandie gari kwa mbele.
 
Hamasa iliyotolewa na Mufti Simba, ni njema na ya kuigwa na waungwana wote. Hamasa kama hii haijali aliyeitoa ana elimu gani au ana cheo gani! Wengi wetu tulihamasishwa kusoma na wazazi ambao ambao wao hawajaaenda shule, lakini walijuwa umuhimu wa elimu. Hivyo natowa hongera kwa Mufti Simba.
 
Ndugu inabidi ufafanue ni kwa jinsi gani kila mtu ni kiongozi. Bila hivo utafanya kosa kubwa la kimantiki. ABSOLUTES CANT CO-EXIST. Namuunga mkono Mufti.
 
Mkuu,
Unataka kuniambia kuwa huko vijijini, makanisa yanahali nzuri sana siyo?

Hata mie nilishaona makanisa na misikiti ikiwa na hali mbaya sana.

Msikiti kwa ndani sikuweza kuona ila kwa nje hata Kufuli halipo. Kuna mlango tu, basi.

Kanisa pia kulikuwa na mlango tu na vidawati kadhaa.........

Vijijini wote ni masikini sana sana. Huko hakuna haja ya kugawa mafungu.

Ila nashukuru kuwa unakubali kwamba kwa mjini, Waislaam wengi wanahela nzuri tu kuzidi Wakristo.

Hebu ona picha kadhaa za kanisa huku Sikonge.....

Msikiti.jpg Kanisa ndani 1.jpg Kanisa ndani.jpg
Mkuu nadhani unawazungumzia waislamu wa mijini. ukienda vijijini mkuu ni aibu hali ya maisha ni mbaya sana. Kuna msikiti mmoja nilienda vijijini huko nikakuta wameufunga na kufuli kwasababu wameshindwa kuuendesha. sasa uwingi wa waislamu unaosema wewe hebu fafanua zaidi.
 
DSC05754.JPG

Sheikh mkuu wa Tanzania, Sheikh issa Bin Shabani Simba, akiwahutubia waumini wa dini ya kiislam na wadau wa elimu, waliohudhuria harambee ya kuchangia fedha kwa ajili ya ujenzi wa bweni la wasichana na bwalo la kulia chakula katika shule ya sekondari Geita Islamic Seminary, wa tatu (shoto) ni mkuu wa wilaya ya Geita ndugu Mh. Philemoni Shelutete.
DSC05746.JPG

Baadhi ya wana madrasa katika harambee hiyo
DSC05755.JPG

Viongozi wa dini ya kiislam waliohudhuria harambee ya kuchangia fedha kwa ajili ya ujenzi wa Bweni la wasichana na Bwalo la chakula katika shule ya sekondari kiislam ya Geita kutoka kushoto wa tatu ni sheikh wa mkoa wa Mwanza Sheikh Salum fereji.
DSC05758.JPG

Wadau waliohudhuria harambee hiyo
DSC05761.JPG

Wadau wa elimu waliohudhuria harambee ya kuchangia fedha kwa ajili ya ujenzi wa bweni la wasichana na bwalo la chakula la shule ya sekondari ya kiislam Geita. harambee hiyo ilifanyika hapahapa wilayani Geita, amabo sasa ni Mkoa.

*Muft Simba, aongoza harambee Geita, achangia milioni tano taslim.
*Asema matokeo mabovu ya kidato cha nne yamesababishwa kwa kuajiri bora walimu na si walimu bora.
*Jumla ya milioni 17,321,300 zilikusanywa.

Picha zote na khabari
na Shabani Simba wa Globu ya Jamii, akiwa Geita.

Sheikh Mkuu wa Tanzania Sheikh Issa Bin Shabani Simba, amewataka waislam kuchangamka kuwekeza katika masuala ya elimu kwani elimu ndio mkombozi ma madhila yote yanayowakumba hapa nchini.

Na badala yake amewataka waislam waache kulalama na badala yake kupambana na vikwazo vyote vinavyowakabili.

Sheikh Simba, aliyasema hayo mjini hapa wakati akiendesha harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa Bweni la wasichana na bwalo la chakula kwenye shule ya sekondari ya kiislam Geita. Katika harambee hiyo sheikh Simba alichangia kiasi cha shilingi milioni tano, fedha taslim.

Sheikh Simba, aliwapongeza waislam wa wilaya ya Geita na vitongoji vyake kwa kujikamua kujenga shule ya sekondari kwa nguvu zao. Lakini aliwaasa viongozi wa shule hiyo kutafuta walimu bora na si bora walimu.

Alisema madhara ya kutafuta bora walimu kutufundishia watoto zetu matokeo yake ndio haya ya kupata matokeo mabovu ya kidato cha nne ya mwaka 2010.Alisema hivi juzi juzi matokeo ya kidato cha nne ya mwaka jana yametoka na kiwango cha ufaulu kiko chini hali hii imechangiwa kwa kiasi kikubwa kwa kuajiri bora walimu na si walimu bora.

Aliongeza uwezi kuwapata walimu wazuri kama huna mshahara wa kutosha unaokidhi magumu ya maisha ya sasa hivyo aliwataka viongozi wa shule hiyo kutafuta vyanzo mbalimbali vya mapato ili kupata fedha na hatimae kulipa mishahara minono itakayowafanya walimu wao wafikirie kazi yao tu ya kufundisha.

“Walimu hawasafiki nia kama hawajakirimiwa, maana yake walimu hawawezi kutufundishia vijana wetu kama hatuwajali” alisema sheikh Simba.

Aliongeza katika dini ya kiislam ukiwa na elimu ndio unakita katika uislam lakini kinyume chake ukiwa hauna elimu unakuwa kama kifaranga cha kuku anayeweza kupitiwa na mwewe wakati wowote.

“kama una elimu utakuwa unasikiliza la kila mtu bila ya kulichuAja kama linafaa au halifai na matokeo yake unayumba na kukosa msimamao muislam hatakiwi kuwa hivyo” alisema Sheikh Simbamba.

Aliwataka waislam kujitolea mali zao kwani kutoa ni sera ya uislam “ kutoa ni sera ya uislam na kutoa chochote ulichoruzukiwa kiwe kidogo au kikubwa” alisisitiza sheikh Simba.

Katika harambee hiyo jumla ya shilingi milioni17321300, zilikusanywa, fedha taslimu zikiw a milioni 4881300 na milioni 12,404,000. Vifaa vya ujenzi vilivyotewa saruji mifuko 87, mchanga maroli 6, bati 6.

Nae mkuu wa wilaya ya Geita ndugu Philemoni shelutete, akitoa salam za wilaya katika harambee hiyo alisema anaunga mkono jitihada za waislam wa Geita na kuhaidi kuwasaidia kwa hali na mali kwani kuanza kwa shule hiyo kutaleta manufaa kwa waislam na wasiokuwa waislam, na hatimaye kutoa ahadi ya kuchangia kiasi cha shilingi milioni moja.

Shule hiyo inayomilikiwa na Bakwata, wilaya ya Geita, ilianza ujenzi wake mwaka 2007katika eneo la Mwatulole, kijiji cha ihabuyaga kata ya kalangalala, mjini Geita.

Kukamilika kwa ujenzi wa Shule hiyo ya bweni inaweza kumaliza tatizo lililopo wilayani hapa la wanafunzi wanaomaliza darasa la saba na kufaulu baadhi yao wanakosa nafasi ya kujiunga na elimu ya sekondari na wasichana wanaochaguliwa katika shule za sekondari kukosa sehemu za kulala.

SOURCE: MICHUZI

Safi sana kwa kuwaeleza ukweli, maana kazi hawafanyi, shule hawaendi, kazi kukaa vijiweni kupiga umbea na majungu halafu malamiko kibao , oh wakristo wanatuonea. SOMENI! mwenzenu huyo kawapasulia. Bado mnalo?
 
Mkuu,
Unataka kuniambia kuwa huko vijijini, makanisa yanahali nzuri sana siyo?

Hata mie nilishaona makanisa na misikiti ikiwa na hali mbaya sana.

Msikiti kwa ndani sikuweza kuona ila kwa nje hata Kufuli halipo. Kuna mlango tu, basi.

Kanisa pia kulikuwa na mlango tu na vidawati kadhaa.........

Vijijini wote ni masikini sana sana. Huko hakuna haja ya kugawa mafungu.

Ila nashukuru kuwa unakubali kwamba kwa mjini, Waislaam wengi wanahela nzuri tu kuzidi Wakristo.

Hebu ona picha kadhaa za kanisa huku Sikonge.....

View attachment 21993View attachment 21994View attachment 21995

Kweli ni hali ya kusikitisha!!!! Inawezekana mijini waislamu wana pesa ila sina data za kutoa uwiano wa nani zaidi.
 
Salaam wanajamvi,
Shekh Mkuu wa Tanzania Mufti Issa bin Shaaban bin Simba amewahimiza waislam kujikita katika kujipatia elimu dunia badala ya kuweka nguvu kwenye elimu ahera pekee.

Mufti huyo aliyasema hayo akiwa wilayani Kondoa mkoani Dodoma wakati akifungua kituo cha elimu wilayani humo kinachojulikana kama "Mufti Issa bin Shaaban bin Simba Education Centre", kituo ambacho kinatarajiwa kuwa kitatoa elimu zote yaani ile ya dini na ile ya kawaida.

Akinukuliwa na shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Mufti alisema, "....Hakuna mtu au taifa lolote lililoendelea duniani bila kufanya jitihada katika Ilimu, bahati mbaya hapa katikati waislam tulilegalega kidogo.....,Nilimsimamisha hapa mtaalam wa kilimo, hata kulima huwezi kulima kama huna Ilimu, utachimba na jembe la mkono wee, utapanda bila utaratibu na hutafanikiwa...., hivyo kituo hiki kiwe changamoto kwa waislamu kujikita katika Ilimu dunia na Ilimu ahera".

Katika ufunguzi huo Mufti aliambatana na waziri wa mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa Mh. Bernard Membe ambaye aliwaahidi waislam kuwa Serikali itafanya kila liwezekanalo ili kituo hicho kiweze kutoa huduma bora.

Source:
Taarifa ya Habri TBC1 tarehe 09.05.2011 saa 2 usiku
 
Bernard Membe, ha jamaa anaanza kulenga mbali
 
Media Tanzania yale yaleeee

Huyu hana dhamana ya kuwasemea waislam wote Tanzania

huyu ni sheikh mkuu wa BAKWATA na constituency yake iko confined kwa hao hao

Kama angekuwa ni Sheikh Mkuu wa Tanzania mbona hajajibu kitu kuhusu WARAKA wa waislam ambao uko kwenye public domain?

Tatizo hapa ni kwa sababu the man has no meaningful education ya kuweza kusimama kwenye public domain na kujibu hoja. Infact Form 4 hakufika, na hicho Kiarabu inasemekana hajui...na media wanalijua hilo na wanazidi kumpandisha cheo kuwa ndio public face of Muslims in Tanzania. Its like claiming mtu kama vile KAKOBE ndio kiongozi mkuu wa waksristo Tanzania

This is pathetic.

Inasikitisha sana kuona kuwa hata katika jukwaa la heshma kama hili bado tuna members wasiopenda kujadiri hoja bali wanajadiri watu.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom