Mufti ataka Waislamu kuwekeza katika elimu zaidi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mufti ataka Waislamu kuwekeza katika elimu zaidi

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Mzito Kabwela, Jan 30, 2011.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #1
  Jan 30, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,523
  Likes Received: 1,702
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Sheikh mkuu wa Tanzania, Sheikh issa Bin Shabani Simba, akiwahutubia waumini wa dini ya kiislam na wadau wa elimu, waliohudhuria harambee ya kuchangia fedha kwa ajili ya ujenzi wa bweni la wasichana na bwalo la kulia chakula katika shule ya sekondari Geita Islamic Seminary, wa tatu (shoto) ni mkuu wa wilaya ya Geita ndugu Mh. Philemoni Shelutete.[​IMG]

  Baadhi ya wana madrasa katika harambee hiyo
  [​IMG]

  Viongozi wa dini ya kiislam waliohudhuria harambee ya kuchangia fedha kwa ajili ya ujenzi wa Bweni la wasichana na Bwalo la chakula katika shule ya sekondari kiislam ya Geita kutoka kushoto wa tatu ni sheikh wa mkoa wa Mwanza Sheikh Salum fereji.
  [​IMG]
  Wadau waliohudhuria harambee hiyo
  [​IMG]

  Wadau wa elimu waliohudhuria harambee ya kuchangia fedha kwa ajili ya ujenzi wa bweni la wasichana na bwalo la chakula la shule ya sekondari ya kiislam Geita. harambee hiyo ilifanyika hapahapa wilayani Geita, amabo sasa ni Mkoa.


  *Muft Simba, aongoza harambee Geita, achangia milioni tano taslim.
  *Asema matokeo mabovu ya kidato cha nne yamesababishwa kwa kuajiri bora walimu na si walimu bora.
  *Jumla ya milioni 17,321,300 zilikusanywa.


  Picha zote na khabari
  na Shabani Simba wa Globu ya Jamii, akiwa Geita.


  Sheikh Mkuu wa Tanzania Sheikh Issa Bin Shabani Simba, amewataka waislam kuchangamka kuwekeza katika masuala ya elimu kwani elimu ndio mkombozi ma madhila yote yanayowakumba hapa nchini.


  Na badala yake amewataka waislam waache kulalama na badala yake kupambana na vikwazo vyote vinavyowakabili.


  Sheikh Simba, aliyasema hayo mjini hapa wakati akiendesha harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa Bweni la wasichana na bwalo la chakula kwenye shule ya sekondari ya kiislam Geita. Katika harambee hiyo sheikh Simba alichangia kiasi cha shilingi milioni tano, fedha taslim.

  Sheikh Simba, aliwapongeza waislam wa wilaya ya Geita na vitongoji vyake kwa kujikamua kujenga shule ya sekondari kwa nguvu zao. Lakini aliwaasa viongozi wa shule hiyo kutafuta walimu bora na si bora walimu.

  Alisema madhara ya kutafuta bora walimu kutufundishia watoto zetu matokeo yake ndio haya ya kupata matokeo mabovu ya kidato cha nne ya mwaka 2010.Alisema hivi juzi juzi matokeo ya kidato cha nne ya mwaka jana yametoka na kiwango cha ufaulu kiko chini hali hii imechangiwa kwa kiasi kikubwa kwa kuajiri bora walimu na si walimu bora.

  Aliongeza uwezi kuwapata walimu wazuri kama huna mshahara wa kutosha unaokidhi magumu ya maisha ya sasa hivyo aliwataka viongozi wa shule hiyo kutafuta vyanzo mbalimbali vya mapato ili kupata fedha na hatimae kulipa mishahara minono itakayowafanya walimu wao wafikirie kazi yao tu ya kufundisha.

  “Walimu hawasafiki nia kama hawajakirimiwa, maana yake walimu hawawezi kutufundishia vijana wetu kama hatuwajali” alisema sheikh Simba.

  Aliongeza katika dini ya kiislam ukiwa na elimu ndio unakita katika uislam lakini kinyume chake ukiwa hauna elimu unakuwa kama kifaranga cha kuku anayeweza kupitiwa na mwewe wakati wowote.

  “kama una elimu utakuwa unasikiliza la kila mtu bila ya kulichuAja kama linafaa au halifai na matokeo yake unayumba na kukosa msimamao muislam hatakiwi kuwa hivyo” alisema Sheikh Simbamba.

  Aliwataka waislam kujitolea mali zao kwani kutoa ni sera ya uislam “ kutoa ni sera ya uislam na kutoa chochote ulichoruzukiwa kiwe kidogo au kikubwa” alisisitiza sheikh Simba.

  Katika harambee hiyo jumla ya shilingi milioni17321300, zilikusanywa, fedha taslimu zikiw a milioni 4881300 na milioni 12,404,000. Vifaa vya ujenzi vilivyotewa saruji mifuko 87, mchanga maroli 6, bati 6.

  Nae mkuu wa wilaya ya Geita ndugu Philemoni shelutete, akitoa salam za wilaya katika harambee hiyo alisema anaunga mkono jitihada za waislam wa Geita na kuhaidi kuwasaidia kwa hali na mali kwani kuanza kwa shule hiyo kutaleta manufaa kwa waislam na wasiokuwa waislam, na hatimaye kutoa ahadi ya kuchangia kiasi cha shilingi milioni moja.

  Shule hiyo inayomilikiwa na Bakwata, wilaya ya Geita, ilianza ujenzi wake mwaka 2007katika eneo la Mwatulole, kijiji cha ihabuyaga kata ya kalangalala, mjini Geita.

  Kukamilika kwa ujenzi wa Shule hiyo ya bweni inaweza kumaliza tatizo lililopo wilayani hapa la wanafunzi wanaomaliza darasa la saba na kufaulu baadhi yao wanakosa nafasi ya kujiunga na elimu ya sekondari na wasichana wanaochaguliwa katika shule za sekondari kukosa sehemu za kulala.


  SOURCE: MICHUZI
   
 2. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #2
  Jan 31, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  hapa nawaunga mkono!
   
 3. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #3
  Jan 31, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Hapo sheikh mkuu umenena!!!!:clap2:
   
 4. P

  Paul S.S Verified User

  #4
  Jan 31, 2011
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Hii imetulia,i like it
   
 5. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #5
  Jan 31, 2011
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  Media Tanzania yale yaleeee

  Huyu hana dhamana ya kuwasemea waislam wote Tanzania

  huyu ni sheikh mkuu wa BAKWATA na constituency yake iko confined kwa hao hao

  Kama angekuwa ni Sheikh Mkuu wa Tanzania mbona hajajibu kitu kuhusu WARAKA wa waislam ambao uko kwenye public domain?

  Tatizo hapa ni kwa sababu the man has no meaningful education ya kuweza kusimama kwenye public domain na kujibu hoja. Infact Form 4 hakufika, na hicho Kiarabu inasemekana hajui...na media wanalijua hilo na wanazidi kumpandisha cheo kuwa ndio public face of Muslims in Tanzania. Its like claiming mtu kama vile KAKOBE ndio kiongozi mkuu wa waksristo Tanzania

  This is pathetic.
   
 6. P

  Paul S.S Verified User

  #6
  Jan 31, 2011
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Mkuu punguza jazba, tatizo lako ni nini hasa? mimi sioni kwanini unamponda kiasi hicho.
  Hapa issue ni kuwa amefanya uchangishaji wa pesa kwaajili ya jambo jema la elimu, na akatoa wito jambo hilo liendelee.
  Nawachangiaji wanapongeza kitendo hicho, sasa sijui wewe ulitaka aseme wailamu wa bakwata tu ndio wajali elimu au vipi?
  Maana naona unatoka nje ya mada sasa na kuanza kuhoji uhalali wake badala ya wito wake kama muislam
   
 7. P

  Paul S.S Verified User

  #7
  Jan 31, 2011
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Mkuu punguza jazba, tatizo lako ni nini hasa? mimi sioni kwanini unamponda kiasi hicho.
  Hapa issue ni kuwa amefanya uchangishaji wa pesa kwaajili ya jambo jema la elimu, na akatoa wito jambo hilo liendelee.
  Nawachangiaji wanapongeza kitendo hicho, sasa sijui wewe ulitaka aseme wailamu wa bakwata tu ndio wajali elimu au vipi?
  Maana naona unatoka nje ya mada sasa na kuanza kuhoji uhalali wake badala ya wito wake
   
 8. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #8
  Jan 31, 2011
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  [​IMG]
   
 9. mwanamara

  mwanamara Member

  #9
  Jan 31, 2011
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 53
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 15
  For sure that is the right and best statement muslims desperately need to hear and work on by all the right means regardless it protrudes from the educated or uneducated muslim or non-muslim. Hamasa katika kuunga mkono juhudi za kuwekeza kwenye elimu inaunganisha zaidi kuliko hamasa katika kuunga mkono juhudi za kulaumu inavyogawa zaidi. Ni bora kuchagua hamasa bora mapema na kuifanyia kazi.
   
 10. V

  Vumbi Senior Member

  #10
  Jan 31, 2011
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 191
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Sioni sababu ya kumdhihari mufti mkuu wa TZ, ni kiongozi aliyechaguliwa kihalali na anaongoza taasisi inayotambuliwa kihalali. Kama wewe humuhitaji au humtambui kwa matakwa yako sioni sababu ya kumrushia maneno hayo. Suala linalozungumziwa ni elimu amekosea nini kusema waislamu wachangie na kuwekeza kwenye elimu?. Mimi nadhani ametoa mawazo mazuri na anatakiwa kuungwa mkono na mtu yeyote mpenda maendeleo.

   
 11. P

  Paul S.S Verified User

  #11
  Jan 31, 2011
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Mkuu umenena hasa kigreat thinker, lakini chaajabu mtu anakuja from no where anaanza kulaumu tuuuu, hizi lawama wakati mwingine hazisaidii sana
   
 12. m

  mtemiwao JF-Expert Member

  #12
  Jan 31, 2011
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 384
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyu anaelaumu labda ni mmoja wa wale mbumbumbu waliokaa pale mwz wakafanya kakongamano ka kitoto na kutoa tamko la kichekechea
   
 13. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #13
  Jan 31, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Mimi namuunga mkono Shekhe Mkuu na in fact ndiye ninayemtambua kuwa ni kiongozi rasmi wa waislam nchini. Waislam lazima wabadilike. Waanze kuthamini elimu na ndiyo itakuwa ukombozi wao.

  Hao mashekhe ubwabwa wa Mwanza waliotoa tamko tuwapuuze. Njaa ya pilau ndiyo inawasumbua.
   
 14. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #14
  Jan 31, 2011
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,856
  Likes Received: 2,432
  Trophy Points: 280
  Ndugu zetu Waislamu inabidi sasa watuambie Kiongozi wao Mkuu Tanzania Ni nani??

  sijaona ubaya wa alichoongea Sheikh Mkuu Mussa bin Shaabaan Simba.......

  Nadhani hawa na wengine dizaini ya Mdondoaji ...wangependa Sheikh Mmoja wa Msikiti Wa Al Idrissa.........BASALAH Ndie awe sheikh mkuu au mtu wa aina hiyo .....hawanyimwi kumchagua kwa taratibu zao ..ili basi tujuwe nani anaongea kwa niaba yao ....
   
 15. Z

  Zero One Two JF-Expert Member

  #15
  Jan 31, 2011
  Joined: Sep 16, 2007
  Messages: 9,390
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  Huwa sielewi wakisema kiongozi fulani au Mufti amechangia shilingi milioni tano. Ni hela zake binafsi au mfuko fulani wa ofisi ya Mufti?

  Mufti ana mshahara wa kutoa milioni tano just like that, au ndio anataka watu waseme BAKWATA wezi?

  Na kama sio zake, kwa nini wasiseme wazi kwamba zimechangiwa na BAKWATA?


   
 16. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #16
  Jan 31, 2011
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Saafi sana Shekh Simba:clap2::clap2::clap2:
   
 17. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #17
  Jan 31, 2011
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Hii ndio kauli ya Waislamu. Sio zile za vibaraka wachache wanaotumiwa na mafisadi alafu wanajifanya ni waislamu. Waislamu inabidi waungane kuwapiga vita watu wachache wanaotumiwa kuwachafua katika jamii.
   
 18. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #18
  Jan 31, 2011
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Kiongozi kwa mujibu upi? Kwa wasilamu kila mtu ni kiongozi!
   
 19. T

  Tata JF-Expert Member

  #19
  Jan 31, 2011
  Joined: Dec 3, 2009
  Messages: 4,737
  Likes Received: 657
  Trophy Points: 280
  Suala ni kama alichosema kuhusu umuhimu wa waislamu kusomesha watoto kina mantiki au la. Mambo ya elimu yake na kama anajua kiarabu au hayana uhusiano wowote na harambee ya kujenga mabweni ya wasichana Geita.
   
 20. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #20
  Jan 31, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  mh. umemuelewa philemon ktk mchango wake, kaweka maneno "kiongozi Mkuu' jamani hata kama kila mtu ktk jumuiya ni kiongozi huwa kuna Mkuu wa viongozi. Kwa ili nawaomba waislam wote wawe na hofu ya Mungu,wamtambue kiongozi mkuu. Uislamu si siasa, tujaribu kujua kuwa lazima kuna mtu ambaye amechaguliwa kuwaongoza wenzie Tanzania,uyo ndo mkuu. Kama nakosea nielekeze mkuu.
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...