Azizi Mussa
JF-Expert Member
- May 9, 2012
- 9,172
- 7,428
Kuna msemo kuwa ili kupata matokeo yasiyo ya kawaida, ni lazima kwanza kufanya kitu kisichokuwa cha kawaida .
Sote tunakubaliana kuwa ili kukuza uchumi wetu, kwa vyovyote vile ni lazima tukuze uwekezaji wa kutoka nje lakini pia wa ndani ya nchi.
Hata hiyo sio tu kwamba kasi ya uwekezaji kwa ujumla wake hairidhishi sana bali pia kuna hoja ya kwamba mazingira ya uwekezaji hayavutii vya kutosha. Aidha, kuna hoja kuwa, biashara nyingi zinazoanzishwa huishia kufa na watanzania wengi wanashindwa kuwekeza kwa kukosa mitaji.
Pamoja na uwezo mkubwa ambao Prof. Mkumbo anao na hivyo kuleta matumaini kuwa kuna hatua tunaweza kupiga chini ya uongozi wake, vile vile yanahitajika mabadiliko makubwa ya kimifumo ili kupata mafanikio makubwa. Kwa leo nitagusia eneo moja kwa ufupi sana, maeneo mawili tutayagusia wakati mwingine.
Kwanza, kuhusu hoja ya kwamba hakuna mazingira rafiki ya uwekezaji. Hoja hii inajiekemeza kwenye suala la kwamba, kumekuwa na tozo na kodi nyingi bila kujali biashara zinatengeneza faida au laa jambo ambalo ni sawa na kumkamua ng'ombe bila kujali anakula au la! mwishowe anakufa.
Ni nini cha kufanya? Kwa kuwa TRA ni chombo cha serikali cha kukusanya kodi, kwa muundo wake hamna namna kinaweza kujikita sana kukuza biashara za wadau badala ya kukusanya kodi.
Hivyo ni vyema kuwa na mfumo mwingine ambao kazi yake itakuwa ni kufuatilia biashara 'interprises' mpyaa na zile za zamani ili kubaini changamoto zinazokabili biashara husika na kuzifikisha kwa wafanya maamuzi haraka bila urasimu ili zitatuliwe. Aidha, kutambua kama biashara husika zinaenda kwa hasara na kushauri wafanya maamuzi juu ya ' interventions' muhimu za kufanya ili kuokoa biashara husika ikiwemo pengine kupunguziwa kodi kwa kipindi maalum na na kutambua biashara ambazo zishatengemaa na kuongeza kodi kidogo kidogo kwa namna ambayo italeta 'win win situation'.k
Kwa maoni yangu, kulingana na mazingira ya kisiasa nchini, kazi hii inaweza kuwa na ufanisi ikiwa kitengo/ mfumi huu utaundwa ndani ya chama kinachoongoza dola, na humo wakawekwa watu wenye uwezo mkubwa wa kufikiri, kuchanganua mambo na kubuni solutions za matatizo mbalimbali ya kiuwekezaji.
Mfumo juu utaweka mazingira ya kuhakikisha kuwa, hakuna biashara 'interprises' inayokufa, na kuchukulia kuwa kufa kwa biashara hata moja tu bila kujali ukubwa wake ni kosa kubwa sana.
Mbinu hii imetunika China na ndio moja ya sababu moja ya sababu kubwa zilizosaidia kuibuka kwa biashara na kampuni nyingi kubwa na ndogo ndogo kuanzia miaka ya 90's hadi sasa ambazo zinaendeshwa kwa faida na kuiweka China kwenye kilele cha mafanikio ya kiuchumi kwa kutengeneza na kukuza wawekezaji wa ndani ya china na nje ya china waliowekeza China.
Mfumo huu utakuwa ni complement kwa mifumo iliyopo ya ukusanyaji kodi ambapo wakati wakusanya kodi watakuwa wanakamua maziwa, mfumo huu utakuwa unamlisha ng'ombe ili kwanza aweze kuwepo na kisha atoe maziwa.
Swali ni je? Kama watakaopewa kazi hiyo wataamua kuwa corrupt pengine wakawa wanafanya manipulation na wasitoe taarifa za kweli? Jibu ni kwamba mfumo huo utatakiwa kuwa na checks and balances ndani yake wenyewe na nje pia.
Nitaendelea sehemu ya pili itakayoeleza ni kwa vipi tunaweza kutengeneza wawekezaji wa ndani kwa wingi, kwa muda mfupi na kwa mafanikio makubwa na Sehemu ya tatu ambayo itaelezea ni nini Tufanye ili wawekezaji wa nje waje Tanzania na sio kwenda nchi nyingine duniani? Wakati dunia ina mamia ya nchi.