Muelekeo wa Uwekezaji nchini chini ya uongozi wa Prof. Mkumbo, Tunatokaje tulipo?

Azizi Mussa

Verified Member
May 9, 2012
8,789
2,000
Kuna msemo kuwa ili kupata matokeo yasiyo ya kawaida, ni lazima kwanza kufanya kitu kisichokuwa cha kawaida .

Sote tunakubaliana kuwa ili kukuza uchumi wetu, kwa vyovyote vile ni lazima tukuze uwekezaji wa kutoka nje lakini pia wa ndani ya nchi.

Hata hiyo sio tu kwamba kasi ya uwekezaji kwa ujumla wake hairidhishi sana bali pia kuna hoja ya kwamba mazingira ya uwekezaji hayavutii vya kutosha. Aidha, kuna hoja kuwa, biashara nyingi zinazoanzishwa huishia kufa na watanzania wengi wanashindwa kuwekeza kwa kukosa mitaji.

Pamoja na uwezo mkubwa ambao Prof. Mkumbo anao na hivyo kuleta matumaini kuwa kuna hatua tunaweza kupiga chini ya uongozi wake, vile vile yanahitajika mabadiliko makubwa ya kimifumo ili kupata mafanikio makubwa. Kwa leo nitagusia eneo moja kwa ufupi sana, maeneo mawili tutayagusia wakati mwingine.

Kwanza, kuhusu hoja ya kwamba hakuna mazingira rafiki ya uwekezaji. Hoja hii inajiekemeza kwenye suala la kwamba, kumekuwa na tozo na kodi nyingi bila kujali biashara zinatengeneza faida au laa jambo ambalo ni sawa na kumkamua ng'ombe bila kujali anakula au la! mwishowe anakufa.

Ni nini cha kufanya? Kwa kuwa TRA ni chombo cha serikali cha kukusanya kodi, kwa muundo wake hamna namna kinaweza kujikita sana kukuza biashara za wadau badala ya kukusanya kodi.

Hivyo ni vyema kuwa na mfumo mwingine ambao kazi yake itakuwa ni kufuatilia biashara 'interprises' mpyaa na zile za zamani ili kubaini changamoto zinazokabili biashara husika na kuzifikisha kwa wafanya maamuzi haraka bila urasimu ili zitatuliwe. Aidha, kutambua kama biashara husika zinaenda kwa hasara na kushauri wafanya maamuzi juu ya ' interventions' muhimu za kufanya ili kuokoa biashara husika ikiwemo pengine kupunguziwa kodi kwa kipindi maalum na na kutambua biashara ambazo zishatengemaa na kuongeza kodi kidogo kidogo kwa namna ambayo italeta 'win win situation'.k

Kwa maoni yangu, kulingana na mazingira ya kisiasa nchini, kazi hii inaweza kuwa na ufanisi ikiwa kitengo/ mfumi huu utaundwa ndani ya chama kinachoongoza dola, na humo wakawekwa watu wenye uwezo mkubwa wa kufikiri, kuchanganua mambo na kubuni solutions za matatizo mbalimbali ya kiuwekezaji.

Mfumo juu utaweka mazingira ya kuhakikisha kuwa, hakuna biashara 'interprises' inayokufa, na kuchukulia kuwa kufa kwa biashara hata moja tu bila kujali ukubwa wake ni kosa kubwa sana.

Mbinu hii imetunika China na ndio moja ya sababu moja ya sababu kubwa zilizosaidia kuibuka kwa biashara na kampuni nyingi kubwa na ndogo ndogo kuanzia miaka ya 90's hadi sasa ambazo zinaendeshwa kwa faida na kuiweka China kwenye kilele cha mafanikio ya kiuchumi kwa kutengeneza na kukuza wawekezaji wa ndani ya china na nje ya china waliowekeza China.

Mfumo huu utakuwa ni complement kwa mifumo iliyopo ya ukusanyaji kodi ambapo wakati wakusanya kodi watakuwa wanakamua maziwa, mfumo huu utakuwa unamlisha ng'ombe ili kwanza aweze kuwepo na kisha atoe maziwa.

Swali ni je? Kama watakaopewa kazi hiyo wataamua kuwa corrupt pengine wakawa wanafanya manipulation na wasitoe taarifa za kweli? Jibu ni kwamba mfumo huo utatakiwa kuwa na checks and balances ndani yake wenyewe na nje pia.

Nitaendelea sehemu ya pili itakayoeleza ni kwa vipi tunaweza kutengeneza wawekezaji wa ndani kwa wingi, kwa muda mfupi na kwa mafanikio makubwa na Sehemu ya tatu ambayo itaelezea ni nini Tufanye ili wawekezaji wa nje waje Tanzania na sio kwenda nchi nyingine duniani? Wakati dunia ina mamia ya nchi.
 

dudus

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
14,467
2,000
Covid-19 imeathiri uwekezaji duniani kote sio Tanzania peke yake japo Tanzania haina Corona kwa mujibu wa wataalamu wetu. Pili sheria za kodi nazo ni tatizo; Wizara ya Prof. Mkumbo ni mwathirika wa hayo.
 

ngorokolo

Senior Member
Mar 3, 2021
132
250
Unamzungumzia mkumbo huyu aliehojiwa juzi na ITV?sina hakika sana kama kuna la maana atakaloliibua mkumbo ndani ya muda atakao kuwepo katika hiyo wizara mfano mzuli ni majuzi anaacha kuzungumzia changamoto za wizara na namna mpango kazi wa namna ya kuzitatua anapoteza muda kuwashambulia chadema yaani unawaza huyu nae ni professor?
 

Azizi Mussa

Verified Member
May 9, 2012
8,789
2,000
Uko sahihi sana mkuu. Katika mazingira hayo sasa, ndio unapoonekana zaidi umuhimu wa kutengeneza wawekezaji wa ndani kwa wingi, ambapo mbele ni tutajadili ni kwa vipi hilo linawezekana kwa kwa kufanya mabadiliko flani flani kwenye mfumo wa elimu na kujenga uwezo kwenye maeneo flani flani.
... Covid-19 imeathiri uwekezaji duniani kote sio Tanzania peke yake japo Tanzania haina Corona kwa mujibu wa wataalamu wetu. Pili sheria za kodi nazo ni tatizo; Wizara ya Prof. Mkumbo ni mwathirika wa hayo.
.
 

Azizi Mussa

Verified Member
May 9, 2012
8,789
2,000
Tatizo la kukosa ubunifu ni Tatizo pana kidogo linalotusumbua waafrika wengi. Kwa hiyo kabla ya kunyoshea wengine vidole kuwa sio wabunifu, ni vyema kuonesha sample ya ubunifu kwa sababu kumlaumu mwingine ni rahisi kazi kufanya!
Huyu mzee hana ubuni wowote yeye anachowaza ni CHADEMA unaitwa kwenye kipindi kwenye TV badala ya kuongelea mipango wewe unakomaa na CHADEMA mwanzo mwisho, Wizara haina Waziri ina kivuli pekee
 

Azizi Mussa

Verified Member
May 9, 2012
8,789
2,000
Hana uwezo hajawahi kufanya biashara ya aina yoyote maishani mwake eti unampa Wizara ya uwekezaji!
Mkuu, ili kuwezesha vitu flani vitokeee, sio lazima muwezeshaji awe ashafanya vitu hivyo. Mfano, mwalimu wa shule ya msingi anawezesha watu kuwa madaktari, ma ingeneer ni.k ila yeye hajawahi kuwa.

Au waganga wa kienyeji huwezesha watu kupata pesa za majini na kuwa matajiri, wakati wao hawajawahi kuwa matajiri. Hahaahahaa (jocking)
 

Azizi Mussa

Verified Member
May 9, 2012
8,789
2,000
Kibongo bongo ni moja ya watu smart sana, kulingana na samples zilizopo. Kwa hiyo akipata support anaweza kuleta mafanikio makubwa kwenye eneo la uwekezaji.

Tatizo ni pale tunapojilinganisha na kina Musk, bila kukumbuka wabongo tunajijua tu wenyewe hahahahah
Kitila Mkumbo ana uwezo mkubwa? 😂😂😂😂tangu lini?
 

Babati

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
44,574
2,000
Tatizo la kukosa ubunifu ni Tatizo pana kidogo linalotusumbua waafrika wengi. Kwa hiyo kabla ya kunyoshea wengine vidole kuwa sio wabunifu, ni vyema kuonesha sample ya ubunifu kwa sababu kumlaumu mwingine ni rahisi kazi kufanya!
Wewe utakuwa na shida kichwani, unaitwa kwenye kipindi ajili ya kuongelea mafanikio ya Wizara yako, changamoto na mikakati lakini unaishia kuisema CHADEMA, kwani bado tupo kwenye kampeni? JK alikuwa Rais akitaka kwenda nje anaondoka na wafanyabiashara hata 50 kwenda kuwakutanisha na wafanyabiashara wakubwa duniani na kupata uzoefu, huko angani ni kushauriana namna ya kukuza uchumi na mengine.
 

Econometrician

JF-Expert Member
Oct 25, 2013
11,596
2,000
Kibongo bongo ni moja ya watu smart sana, kulingana na samples zilizopo. Kwa hiyo akipata support anaweza kuleta mafanikio makubwa kwenye eneo la uwekezaji.

Tatizo ni pale tunapojilinganisha na kina Musk, bila kukumbuka wabongo tunajijua tu wenyewe hahahahah
Kwa hiyo kwako Kitila ni mtu smart?
 

Econometrician

JF-Expert Member
Oct 25, 2013
11,596
2,000
By the way as long as Magufuli ana exist kwenye kile kiti hakuna chochote kipya kwenye uwekezaji kitakachofanyika na hata kikifanyika hakita kuwa na umuhimu sababu uwekezaji Tanzania umerudishwa nyuma na Sera zake za miaka 47 za kutaka serikali kuhodhi kila kitu.

Ukiachana na huo,kuna kuna uwekezaji wa MTU moja moja ambapo Watanzania wengi walikuwa wamisha anza kupiga hatua Kibiashara hence maisha binafsi ya watu kustawi hapa napo katurudisha hatua 1000 nyuma.Mchawi wa maendeleo ya Watanzania kila Siku mnampamba na kumsifia bado tunasubiri miujiza-poor Tanzanians.
 

G4N

JF-Expert Member
Apr 6, 2014
314
1,000
Mkumbo hahisiki na chochote hapa. Lawama zote ziende kwa jiwe
 

Bramo

JF-Expert Member
Oct 21, 2009
12,043
2,000
Uko sahihi sana mkuu. Katika mazingira hayo sasa, ndio unapoonekana zaidi umuhimu wa kutengeneza wawekezaji wa ndani kwa wingi, ambapo mbele ni tutajadili ni kwa vipi hilo linawezekana kwa kwa kufanya mabadiliko flani flani kwenye mfumo wa elimu na kujenga uwezo kwenye maeneo flani flani.

.
Azizi,

Kuna Mabadiliko Makubwa sana yamefanywa kwenye mfumo wa Elimu tena kwa hati ya dharura kwa kuanzisha Somo la Historia ya Tanzania kuanzia Darasa la Kwanza Mpaka Form six.
Au Nasema Uongo Ndugu Zangu ?
 

denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
5,648
2,000
Kitila angekuwa na uwezo angeanzisha chama chake akijenge tukione badala ya kukimbilia CCM kama alivyofanya, he is nobody to me; hapo ulipotaka kuundwe chombo kitachojihusisha na masuala ya kodi kitakachokuwa nje ya TRA na kitatokana na watu toka ndani ya "chama dola", hapo ndipo sijakuelewa kabisa.

Hili neno "chama dola" kwanza mtambue sio sifa ndugu zanguni, mamlaka na nguvu ya chama chochote cha siasa siku zote lazima yatoke kwa wanachama na wapenzi wake, kutegemea nguvu toka nje ya hapo ni udhaifu, hicho chama hakifai kuongoza nchi.

Hali hii ndio husababisha CHADEMA waonekane wanaharakati, kwasababu kwa hali ya kawaida hawashindani na wanasiasa wenzao bali wanashindana na "chama cha siasa" jina tu kinachotegemea support ya kina Mambosasa.

Hiki ndicho husababisha Chadema wajivike uanaharakati ili kujaribu kwenda sawa na hiki chama kinachotegemea nguvu ya dola/polisi ili kupigania haki zao, mfano pale wanapotaka kuandamana kisheria inaruhusiwa, lakini Mambosasa anakataa maandamano yao ili kuilinda CCM, hapa lazima Chadema wapiganie hali yao, ila wajinga huwaita wanaharakati bila kujua their motive behind.

Sasa ukishakuwa na chama dhaifu kama hicho kinachotegemea dola, hao watu "ma-genious" unaowataka wapewe hiyo task ya kufuatilia mambo ya biashara za watu watakuwa na nguvu gani kutekeleza majukumu yao kwa uhuru bila kupendelea maslahi ya chama chao, na/au kujipendekeza kwa kiongozi wao kwa kuwakandamiza wale wasio wa chama chao ili kumfurahisha bosi wao? hapa utaona hapatakuwepo na tofauti yoyote na haya tunayoshuhudia siku hizi.

Kwa mtazamo wangu mengi ya hayo uliyoandika hapo juu yanahitaji mtazamo na fikra mpya katika taifa letu ili kutekelezeka, na fikra hizo lazima ziongozwe na katiba mpya itakayompa kila mmoja wetu uwanja wake wa kutimiza majukumu yake kisheria zaidi (kwa uhuru), badala ya kusubiri fulani akupe kazi halafu uanze kufanya hiyo kazi kwa hofu bila weledi wowote ili umridhishe bosi wako.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom