Muda wa Urais ni Miaka kumi, ikitokea akazidisha mtafanyaje wananchi

Katiba imetungwa na Watanzania kuelekeza kwamba Rais atatawala kwa kipindi cha miaka 5 baada ya hapo kama atachaguliwa tena kwa muhula wa pili basi itakuwa ni miaka5 baada ya hapo hapaswi kugombea tena lakini ni watanzania hao hao tunaoweza kuamua kwamba Rais atawale mihula mitatu maana nchi ni ya kwetu tuna haki ya kujiamulia mambo yetu.
 
Hahaha kaka unarudia mule mule HAIWEZEKANI, Nakubaliana nawe utaratibu ni miaka 5, lakini haijawahi kuwa 5, na hata inapotokea kutaka kuwa 5 wanakataa, rejea Zanzibar 2015. Hili linaeleweka hata juhudi za sasa za kukataliwa katiba mpya, kuleta muswaada wa vyama vya siasa, kuzuia mikutano ya siasa inaweza kuwa na sura mbaya lakini tunayaona yanatokea. Na inaweza kuwa mikakati yao lakini hoja hapa lipo. Miaka 5 iko kikatiba, na 5x2=10 na imekuwa hivyo awamu 5 sasa.Kwa kuongezea nyie mnafuata katiba wao wanafuata ILANI. Hapo ndipo mnapopishana, wanaenda nyie mnarudi.
Turudi kwenye mada hili la kuongeza muda pia halipo kikatiba, swali ni ikiwa litatokea tutafanya nini wananchi?
Mtafanya kile mlichofanya baada ya kupigwa mkwara na RPC wa makao makuu kule!
 
Akiongeza tutawaomba alshabab sasa waingilie kati,kakatiba kenyewe kabovu(in Nyerere's voice)haka halafu tena kakanyagwe hatuwezi kuwa taifa lenye amani tena hatuwezi.Kama mjenga nchi ni mwananchi halikadhalika mbomoa nchi atakuwa mwananchi mwenyewe.Mchezo wa kuchezea katiba si mzuri,hatutaheshimiana hapa,matokeo ni kukosa uvumilivu na uvumilivu ukitoweka sote tunajua kifuatacho

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nyerere alitawala tangu 1961 mpaka 1985, sijui ni kwanini ilikuwa hivyo. Ila marais waliofuatia wamekuwa na utaratibu wao wa kukaa miaka 10 kila mmoja. Kunadhana kwamba hiwezekani akazidisha muda, eti katiba inamkataza, sawa. lakini ikitokea aka kaa zaidi ya miaka kumi kwa kisingizio chochote, mtafanya nini wananchi. Kua haijawahi kutokea Tanzania sio hoja hapa, kwasababu hata huko ilikotokea hawakuomba, bali mazingira yalitengenezwa na ikawa hivyo. Huwa wansema nitaondoka nikiona mambo yako sawa lakini hayo mambo hawayasemi.

Ikiwa hujaambukizwa ukimwi, huwa unasema mimi siwezi kuupata, haiwezekani. Lakini ukimwi huwa unapata wateja wapya kila siku na kila dakika, na hata wale waliowahi kusema mimi haiwezekani nao wamekumbwa na gharika hilo. Sasa assume inatokea kwetu Tanzania Magufuli naongeza muda, anasema aliyoyapanga kuyafanya hayajaisha ataondoka atakapo jiridhisha yeye kwamba yamefanyika.

Kabla hajazuia Bunge live ilianza minong'ono na wapo wale waliosema HAIWEZEKANI, na hata kabla hajazuia mikutano ya siasa wapo wale waliosema HIWEZEKANI mengine mengi walisema hayawezekani lakini yamewezekana na kila mtu yuko kimyaaaaa. Sasa kuna muswaada wa vyama vya siasa, ilianza minong'ono ,hadi sasa tunauona muswaada na watu wanapeleka maoni yao na maoni yanakusanywa kwa mtindo huohuo tusioufahamu lakini mambo yanakwenda na mwisho utapitishwa. Muswaada wa katiba mpya uliisha tupwa, kuna waliobisha wakasema imetumika pesa nyingi sana na muda HAIWEZEKANI tukauacha na haitawezekana, lakini sasa ni historia, na maisha yanasonga mbele.

Je hili la kuongeza muda baada ya miaka kumi kuisha bado wapo wanosema HAIWEZEKANI? na ikiwa LITAWEZEKANA wao watafanya nini? au tutalialia humu basi tunazoea siku zinaenda.
wadau karibuni tujadiri.

ITAWEZEKANA vizuri sana kwa sababu watanzania ni watu wapole sana, hatutaki vurugu na hatutaki kuvunja amani. tutamuchia atwale mpaka aseme pooo. Mambo mengi makubwa ya kutia hasira na kuhuzunuisha yametokea kwenye taifa hili watanzania tuliishia kulalamika kidogo baadae tukapotezea tukasonga mbele.

Raia always tunaishia kusema "mambo ya siasa ni magumu tuwaachie wenywe, mimi naangalia kupata ugali na kutunza familia yangu wacha wauwane wenyewe sisimu na upinani"
 
Hahaha haya maswali ni kwa ajili ya watu wazima, wewe ulipaswa uwe umelala kesho uwahi shule. Wazazi wa siku hizi hawaangalii watoto wana kesha jamiiforums, halafu wanalalamikia elimu kuwa duni.

nimekupa evidence kuwa hautawezs fanya lolote

pia swali lako ni irrelevant maana ni utopia

utopia majibu ni utopia
 
Wengi wa wapiga kura wana elimu ndogo sana ya Uraia,hawajui nini maana halisi ya kupiga kura. Hawajui nguvu ya kura zao,kwao kupiga kura ni jambo la mazoea tu...
Elimu ndogo ya Uraia itawafanya Watanganyika wasifanye jambo lolote lile tofauti na maelekezo watakayopewa na serikali ya chama dola..!
 
Back
Top Bottom