SoC04 Muda uwe ni dira kuu katika ujenzi wa uchumi wa taifa

Tanzania Tuitakayo competition threads

MDAU TZ

Member
Jun 9, 2023
9
41
MUDA ni sehemu muhimu sana katika mpangilio wa mambo mengi duniani, na hii ni tangu kwa kuumbwa kwake, kutokana na maandiko ya vitabu vya dini, vimeandikwa kwamba hata Mungu aliutumia muda katika kuumba ulimwengu, na kuongeza kuwa Dunia iliumbwa kwa siku sita na ya saba ikawa ni mapumziko yake.

Hii inaonesha kuwa katika kutengeneza kitu chochote na kutaka kufanikiwa, ni muhimu basi kuutumia muda katika kukamilisha kwake, hata kama ikiwa ni sekunde dakika, saa, siku, mwezi au mwaka, lakini itasidia kuonesha kwamba uko katika hatua gani, na umebakisha nini na nini unapaswa ukifanye ili kutimiza lengo unalolikusudia.

Na tukirejea katika uumbwaji wa Dunia, tutagundua kwamba Mungu hakutumia muda tu katika uumbaji bali aliuutumia kwa ufasaha, kwamaana katika zile siku sita, alihakikisha anamaliza kila kitu na ndio maana hakuna sehemu ya maandiko inayosema aliwahi kurudia kufanya marekebisho kwasababu hiyo alipata nafasi ya kupumzika ile siku ya saba.

Najua sisi sio kama Mungu, ni wanadamu na kamwe hatuna uwezo kama wake, hivyo hatuwezi kufanya kama yeye, bali nimetumia Mandiko na kugusia kazi alioifanya Mungu, Muumba mbingu na Ardhi kama sehemu ya utangulizi wangu, katika kuujulisha uma kwamba namna gani muda ulivyo nyenzo kuu katika maisha yetu.

Hata mataifa yalioendeleaq mfano Marekani kwa zaidi ya miaka 200 tangu wapate uhuru, wametumia vizuri Muda katika kujenga Uchumi wao hadi leo kuwa namba moja duniani, na bado wanapambana kuendelea kuwa imara kwakujua kwamba wasipofanya hivyo ipo siku Muda utakuja kuwageuka.

China walitumia muda katika kufanya mageuzi ya kiuchumi na kufikia hatua hii walionayo sasa, Urusi wakati wa mabadiliko ya kiuongozi miaka 99, katika vyanzo mbalimbali vya historia vinaeleza kuwa Boris Yeltsin aliyekuwa Rais wa shirikisho la urusi wakati huo, alitumia muda katika kumtafuta mrithi wake na hatimae kumpata Vladimir Putin na kufanya Taifa hilo kuwa imara mpaka sasa.

Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Baba wa taifa hili, licha ya kutumia muda katika kupambania Uhuru na kuupata miaka ya 60, lakini bado aliona sio Muda sahihi wa kutumia rasilimali zilizokuwepo wakati ule yakiwemo madini, hakuwa tayari kufanya hivyo kwasababu alijua utafika wakati wa kuzitumia kwa faida ya Watanzania wote.

KIVIPI MUDA HAUTUMIKI VIZURI NA WAPI UTUMIKE?

UJENZI WA MIUNDO MBINU, mfano barabara nyingi hujengwa bila ya kuzingatia viwango hari inayopelekea kudumu kwa muda mfupi, pengine husababishwa na wakandarasi wasio na ubora au ufinyu wa bajeti, kitendo hiki hufanya kutumika kwa pato kubwa la taifa katika tatizo moja na hivyo Nchi kudumaa kiuchumi, wakati kama zitajengwa barabara zenye ubora na kudumu kwa muda mrefu, Kama Taifa itafika Muda litakuwa limemaliza Tatizo la barabara kabisa, na kuelekeza nguvu katika matatizo mengine.

UTEKELEZAJI WA MIRADI YA KIMKAKATI, mfano ujenzi wa bwawa la umeme la mwalimu Nyerere, lililokadiriwa kukamilika 21/22, lakini mpaka leo bado hakieleweki, Reli ya kisasa ya mwendo kasi, hii yote ni kutokana na kutokuuthamini Muda, Miradi hii kama ingekamilika kwa wakati ingeleta tija kwa taifa kwa kuanza kurudisha mapato katika mzuunguko, na kusaidia Nchi kupiga hatua za haraka katika Maendeleo.

UWAJIBIKAJI MAKAZINI, inatokea kuna mtumishi ameleta uzembe na kulisababishia Taifa hasara na bado yupo kazini, huu muda wa huyu mtu kuendelea kuwa ofisini kwake ni sawa na kuusimamisha uchumi wa Nchi kwa kuufunga kamba, kwasababu mtumishi huyu ataendelea kukwamisha maendeleo yasisonge mbele kwa uzembe au masilahi yake binafsi, Mtu huyu anapswa atolewe na kuwekwa mwengine atakaetambua thamani ya Muda.

MAAMUZI YA KITAIFA, Mamlaka zenye dhamana ya kutoa maamuzi kwaajili ya Taifa hili, linapaswa kutafakari kwa kina juu ya upokeaji wa wawekezaji, wapo wawekezaji wenye nia ya kunyanyua uchumi wetu, na wapo wanyonyaji, amabao watachangia kudumaza uchumi wetu, Maamuzi haya yapimwe kwa viwango tofauti kutokana na ukubwa wake.

Kuundwe vyombo huru mbali na vilivyopo vitakavyotathimini maamuzi hayo kabla ya kupitishwa na hata baada ya kupitishwa na kuanza kufanya kazi, na iwe na nguvu ya kisheria ya kutengua baazi ya maamuzi yenye viashiria vya kuliletea Taifa Hasara, kwakuwa kupitishwa kwa maamuzi yasiofaa ni sawa na kulipotezea Taifa Muda.

MFUMO WA USAFIRISHAJI MIJINI, Kumekuwa na upotezaji wa muda mwingi barabarani wakati wa kwenda kazini au kurudi Nyumbani kwa wafanyakazi wa taasisi binafsi na watumishi wa uma, na hii ni kutokana na asilimia kubwa ya vyombo vya usafiri kumilikiwa na watu binafsi wanaojali maslahi yao kuliko muda, uzembe wa madereva barabarani, uchakavu wa vyombo venyewe na ubovu wa miundombinu imekuwa chanzo cha watu kutofika kazini kwa wakati na hivyo kufanya maendeleo ya Nchi kusuasua.

Ni wakati sasa wa serikali kufikiria kuwekeza katika usafirishaji hasa katika mij yote mikubwa, ukamilishaji wa miradi kama barabara za mwendo kasi, uboreshaji wa usafiri wa relini, kama uanzishwaji wa treni za umeme mijini, kuanzishwa kwa chombo cha udhibiti ubora ambacho kitasimamia na kuhakikisha shughuli za usafiri mijini zinakuwa safi na salaama.

Mambo ni mengi lakini niaminini mimi, nasema muda ukithaminiwa na kufuatwa vizuri, kila kitu kitakwenda katika mpangilio, na uchumi wa taifa letu utanyanyuka kwa haraka sana, mfano tuliuona wakati wa serikali ya awamu ya tano, zile zilukuwa ni dalili ya kuujali muda, punde nchi ikapaa mpaka uchumi wa chini wa kati, ingawa sasa sijui tuko wapi, lakini ninachotaka kusisitiza katika kumalizia ni kwamba ingawa hatuwezi kuijenga kwa Tanzania kwa siku sita, na ya saba tukapumzika, ila muda ukizingatiwa ipasavyo tutafika nchi ya ahadi.
 
Mungu aliutumia muda katika kuumba ulimwengu
Mmh! Angetumia muda isingewezekanika maana muda haukuwepo kabla ya kuumbwa kwa ulimwengu. Labda mchakato wa kukamilika kwake ndio unatumia muda ila kuumbwa aaaaah! Ni paaap dakika sifuri ulimwengu huu hapa🤩🤯🤯🤯.

Hii inaonesha kuwa katika kutengeneza kitu chochote na kutaka kufanikiwa, ni muhimu basi kuutumia muda katika kukamilisha kwake, hata kama ikiwa ni sekunde dakika, saa, siku, mwezi au mwaka, lakini itasidia kuonesha kwamba uko katika hatua gani, na umebakisha nini na nini unapaswa ukifanye ili kutimiza lengo unalolikusudia.
Hakika, kwetu sisi, muda ni kanuni yetu na ni lazima tuutumie vizuri kukamilisha mambo.

UTEKELEZAJI WA MIRADI YA KIMKAKATI, mfano ujenzi wa bwawa la umeme la mwalimu Nyerere, lililokadiriwa kukamilika 21/22, lakini mpaka leo bado hakieleweki,
Inasikitisha sana, tunajicheleweahea mambo mazuri sana.

Mambo ni mengi lakini niaminini mimi, nasema muda ukithaminiwa na kufuatwa vizuri, kila kitu kitakwenda katika mpangilio, na uchumi wa taifa letu utanyanyuka kwa haraka sana, mfano tuliuona wakati wa serikali ya awamu ya tano, zile zilukuwa ni dalili ya kuujali muda, punde nchi ikapaa mpaka uchumi wa chini wa kati, ingawa sasa sijui tuko wapi,
Naamini broh, muda usipotezwe kizembe.
 
Back
Top Bottom