toka bara, visiwani tanzania inapendeza/
tanzania namba one.. duniani twapoteZA/
milima, mito, maziwa kila kona... vivutio vya asili tanzania yetu noma/
lake tanganyika.. hasara usipofika, wegeni njooni bongo hainahaja ya kusita/
ngorongoro crater, naitazama nakesha... inapendezesha bongo, tanzania neemeka/
mlima kilimanjaro/simba, nyati na wao....
ziwa victoria, nyasa ... wengine hakuna nchini kwao/
Najivunia utanzania
Uasili kwa kila njia/
Mwenyezi ametushushia wanyama miti ya kila asilia/
Tuna mibuyu mpaka tukuyu Warembo wanapata ubuyu/
Ngorongoro na manyamara Kilimanjaro Mlima wa bara /
Tumejaliwa vivutio Mnachofanya majangili sio/
Daily magendo ya tembo
Ona wengi hawana magego /
Uasili wa asili umasaini so masihara /
Tunadumisha asili vichwani ona vipara /
Wanyama mwituni Tanzanite mbuguni/
Serikali huni Wamembinfsishia mkoloni/
Licha ya Uasili bado watu duni /
Dawa EDO mr2 na babu Duni ..........
tuna misitu, wanyama tele kwa tele/
watanzania halisi kwanza piga kelele/
misele kila kanda, vivutio tele.. tanzania inapendezea, yani bongo mbele kwa mbele /
hakuna haja ya kwenda U. S, mana bongo inanibamba/
rock city mwanza, mjanja tafta kiwanja/
serengeti, ngorongoro zote zinatupa mikwanja/
aaah! mbuga mikumi naiota kwa kitanda/
ukitaka kupanda mt. kilimanjaro funga mkanda/
bahari ya hindi, upepo pata mawimbi/
nitabaki hapa bongo nchi nyengine SITIMBI/
washindani hao hapo..Nani zaidi. sumbaiArusha ndo kituo /
Utalii kwa mkupuo /
Mawio mpaka machweo/
weupe Huvutiwa na vivutio /
Tuna madini almasi na dhahabu/
Tunao mbuni tausi pia Nyumbu/
ajabu Utalii wa ndani bubu /
Sio Kaboom wala Munkari wanaenda kuona Nyumbu /
Watanzania Tuamke /
Kulinda uasili waume kwa wake/
Asili yetu tuweusi /
Anaeiasi wote tumtusi /
Ona kuna wambulu na waluguru/
Wanyaturu wote tumemulikwa na nuru /
Tu wamoja wote/
Dumisheni asili tz hapafanani na popote /
Haina shaka. Ila hivyohivyo naona bw. radiation hayupo on air. Basi mshindi kati ya worldboss na dabo apambane na magnifico kwa vile yupo. Then radiation akija baadae aendelee na bingwa. Huku nikimsii gwijimimi asikimbie
Piga kura
nawashukuru wote mlionipigia na msionipigia kura maana bila nyinyi mpambano huu usingekuwepo.... dabo hongera zako nakutakia mashindano mema.