Benny
JF-Expert Member
- Jun 6, 2014
- 3,275
- 5,416
Kuusoma umeusoma,
ila hujautafakari,
we ni kama dabo,
anajigamba hana akili,
watu wangu mnakera,
mnaposhndwa mwaga sera,
na ndo kama ticha,
nawatia tu bakora,
magnii mi ndo namba,
hao wengne ni washamba,
kipande we si kaka,
we ni dogoflan amaizn,
kama hunipati,
we nicheki kwenye phone,
nawakil mi vesi,
kwenye koti sina kesi,
vesi zangu past tense,
flow future tense yes,
kaka kipande
magnifico na dabo
Mkibaki hapa lazima mtatoka kapa
Ama mtachapa lapa
Kwa stanza ninazowapa
Kwa vina nawachapa
Nawakaba mtasepa
Nawachora nawapora kila mtindo mnadorora
Mim ndo chongo mwenye usongo wa kuona kwenye giza bila visa bila hongo mnazama kwenye udongo
Choko kwenye soko nawakomba kama ukoko
Mnapata wasi hamna nafasi mpo chini kama viatu vya farasi
Acha niwafuze niwajuze ushairi mnitukuze niwakimbize niwabeze niwakaze kama waya kwenye zeze
Najua mpo poa hii salamu kwenu ninatoa
Anzeni kujibu kwa kubeepu niwakamue kama jipu
Last edited by a moderator: