Muasisi wa CHADEMA atofautiana na Wabunge wa CHADEMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Muasisi wa CHADEMA atofautiana na Wabunge wa CHADEMA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mashayo, Nov 20, 2010.

 1. M

  Mashayo Member

  #1
  Nov 20, 2010
  Joined: May 29, 2007
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Soma hizi habari tatu kwa makini, kisha naomba maoni yako:-

  "Wabunge wa Chadema walikataa bungeni Pinda asiwe Waziri Mkuu na pia chama hicho hakimtambui Jakaya Kikwete kuwa ni Rais halali wa Tanzania. "
  (Source: HABARI LEO HabariLeo | Wabunge Chadema wasusa

  "SIKU mbili baada ya Mbunge wa Jimbo la Katavi, Mizengo Pinda, kuteuliwa na Rais Jakaya Kikwete na kupitishwa na Bunge, kushika wadhifa wa uwaziri mkuu, Muasisi wa Chadema, Edwin Mtei, amepongeza uteuzi huo.."
  (Source: MWANANCHI:Muasisi wa Chadema ampongeza Pinda)

  "Katika hali isiyokuwa ya kawaida, Wabunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), wameamua kutoka nje ya Bunge mara baada ya Rais wa nchi, Jakaya Kikwete kuanza kuhutubia Bungeni. Wabunge hao wametimiza adhima yao ya kutoka nje ya Bunge kama walivyoahidi hapo mwanzo kwa kile kinachodaiwa kuwa hawamtambui Dkt Kikwete kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania." (Source: Global Publishers, BREAKING NEWS: WABUNGE WA CHADEMA WATOKA BUNGENI! - Global Publishers)

  Je hii habari ya pili kama ilivyotolewa na gazeti la MWANANCHI ni ya kweli? Na kama ni ya kweli, Je Mzee wetu Edwin Mtei alitamka pongezi hizi kama yeye (at personal level) au kama chama? Na kama alitamka kama chama, je kuna haja ya chama kubatilisha tamko hili?

  NB: Ninavyofahamu, Uteuzi wa Waziri Mkuu ni moja ya shughuli ya Raisi. Waziri Mkuu ni Kiongozi Mkuu wa shughuli za serikali bungeni. Kupongeza uteuzi huo ni kumpongeza Raisi kwa kufanya shughuli yake kwa ufanisi. Ukipongeza shughuli za Raisi kwa lugha nyingine ni kusema unamtambua Raisi. Kama nimeelewa tofauti naomba nieleweshwe tafadhali.
   
 2. Kiherehere

  Kiherehere JF-Expert Member

  #2
  Nov 20, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,804
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 160
  Tatizo liko wapi?? Umeambiwa mzee Mtei ni kiongozi wa CHADEMA?? Mbona CCM huwa hawasikilizi ushauli wa kina BUTIKU,WARIOBA nk, hiyo haimaanishi utashi wao ndio maamuzi ya CHAMA,chama kina viongozi.
   
 3. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #3
  Nov 20, 2010
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Sio Mtei tu, hata viongozi na wabunge wengine wa chadema hawatambui. Kutokumtambua Rais ni utashi binafsi wa Mbowe uliopokelewa kwa "ndio" na Dr. Slaa na sasa wameushinikiza kwa other Chadema juniors. Zitto na Ndesamburo hawaungi hili.
   
 4. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #4
  Nov 20, 2010
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  kamati kuu ya Chadema hii hapa:
  1.Freeman Aikael Mbowe -Mwenyekiti
  2.Said Amour Arfi (MB)- M/Mwenyekiti Bara
  3.Said Issa Mohamed- M/mwenyekiti Zanzibar
  4.Dr Wilbrod Peter Slaa- Katibu Mkuu
  5. Zitto Zuberi Kabwe- Naibu Katibu Mkuu Bara
  6.Hamad Mussa Yusuph-Naibu Katibu Mkuu Zanzibar
  6. Edwin Mtei- Mwenyekiti Mstaafu
  7.Bob N Makani- Mwenyekiti Mstaafu
  8.Philemon Ndessamburo(MB)
  9.Mhonga Said Ruhanywa (MB)
  10.Shaban Mambo-Mwenyekiti Umoja wa Madiwani
  11.Lazaro Massai-Mwenyekiti wa Halmashauri Karatu
  12.Philip Shelembi
  13.Susan Lyimo(MB)
  14.Mwanamrisho Abama-Zanzibar
  15.Prof Mwesiga Baregu
  16.Dk Kitilla Mkumbo
  17.Nassor Ally Salim -Zanzibar
  18.Regia Estelatus Mtema- Mjumbe mdogo kuliko wote kwa kuchaguliwa
  19.Shida Salum Bitaliho
  20.Leticia G Mosore-Mwenyekiti -Baraza la Wanawake CHADEMA(BAWACHA)
  21.Susan H Kiwanga
  22.Grace Kiwelu(MB)
  23.Paul Herman Sule- Katibu wa Umoja wa Madiwani
  24.Charles Mwera(MB) na Mwenyekiti wa Halmashauri Tarime
  25.Nyangaki Silungushela- Mwenyekiti Baraza la Wazee CHADEMA
  26.John Mnyika-Mkurugenzi
  27.John Mrema-Mkurugenzi
  28.Benson Kigaila-Mkurugenzi
  29.Msafiri Mtemelwa-Mkurugenzi
  30.Victor P Kimesera-Mkurugenzi

  For more refer here https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/45947-yaliyotokana-na-kikao-cha-kamati-kuu-ya-chadema.html
   
 5. Monsignor

  Monsignor JF-Expert Member

  #5
  Nov 20, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 523
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mmmmh! Zito na Ndesamburo walitoka hawakutoka ukumbini? Acha kuwatukana wabunge wa CHADEMA kuwa hawana maamuzi yao wenyewe.
   
 6. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #6
  Nov 20, 2010
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  They didnt walk-out on the President.
   
 7. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #7
  Nov 20, 2010
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  zemarcopolo ...waache wasio na taarifa rasmi utawamaliza....!
   
Loading...