Muarobaini wa CHADEMA kuibwaga CCM chaguzi zijazo

The Phylosopher

JF-Expert Member
Mar 11, 2015
1,503
2,046
Ni ukweli usiopingika kwamba chama pekee chenye walau rasilimali za kutosha kuweza kupambana na CCM kwenye ulingo wa siasa za Tanzania ni Chadema. Hata hivyo kwa mtazamo wangu chama hiki lazima kijiangalie upya namna kinavyoendesha siasa zake.

1. CHADEMA iache kufikiri kwamba itashinda uchaguzi kwa huruma ya CCM.

2. CHADEMA ing'oe mapanndikizi yoote kwa kuwafukuza na si kungoja waondoke wenyewe alafu tuje kuambiwa walikua mamluki.

3. CHADEMA iongeze uvumilivu kwa wanachama iliyowalea na kuwakuza kwa muda mrefu pale wanapoonekana kufanya makosa ya kawaida.

4. CHADEMA iache kushobokea mialiko ya ikulu labda tu kama wanampango wa kujoin na CCM, kwani nijuavyo mimi hakuna kiongozi wa ccm anayetamani chadema imshinde.

5. CHADEMA imejijenga miaka mingi na tumeijua kwa namna ilivyojipambanua kusimamia hoja kuendesha siasa kisasa na si kulialia.

6. CHADEMA ijikite kwenye utafiti wa shida za watu wa ngazi ya chini sana ili ijulikane kwa kujinasibisha na shida za watu badala ya kujiongelea tu.

Mf. Hivi sasa kule nyanda za juu wakulima wanalia bei za mahindi ni mbaya wakati mbolea bei ipo juu. Sasa mkulima anawasha tv/radiobadala ya kusikiliza hiyo kero yake inajibiwaje, anasikia mambo ya haki. Unaweza ukawa sahihi kiufundi lakini mwananchi wa kawaida atachelewa sana kukuelewa.

7. CHADEMA ifanye utafiti kujua ni kwa nini lile vuguvugu la watu kutoka vyama vingine kuhamia CHADEMA limepoa badala yake wamekua wakiondoka tu na hatuoni wala kutangaziwa replacement.

8. CHADEMA imshinikize makamu mwenyekiti bara ndugu Lisu aidha arejee nyumbani au ajiuzulu umakamu mwenyekiti maana haina mantiki chama kikubwa namna hii kinaongozwa na mtu anaishi nje ya nchi.

9. Suala la kina mdee linakipaka matope chama kwani Ndugai na CCM kwao lina faida wananufaika kwa chadema kuendelea kugawika. Nawashauri ili kujitenga n.a. huu uchafu badala ya kuongeaongea tu, waende mahakamani.

10. CHADEMA iunde uongozi kuanzia ngazi ya nyumba kumikumi nchi nzima badala ya kuridhika na vijana wanaojitokeza kwenye mikutano yao mijini.

Nakubaliana na hoja kwamba inahitajika tume huru ya uchaguzi, uchaguzi huru na wa haki, nk hata hivyo nachelea kwamba ukitengeneza wanachama na wafuasi wa kutosha, automatically wataingia kwenye system na kua watetezi wa chama.

Tukikaa tunasubiria tume huru ya uchaguzi na katiba mpya, badala ya kutengeneza social pressure vs dola hatutavipata.
 
Back
Top Bottom