Muache ndoa za unafiki, kama huwezi chepuka

Goliath mfalamagoha

JF-Expert Member
Aug 3, 2012
602
2,505
Mke na Mume asubuhi moja wamegombana ndani ya nyumba. Mwanaume anadai kwamba mkewe ndio mwenye kosa na anapaswa kumuomba msamaha. Mke hakuona ni issue kwake na hakuona haja ya kusema "samahani" kwa mumewe.

Hii ni kawaida kwa Wanandoa na waliopo kwenye mahusiano, mmoja amefanya kosa ila analichukulia kirahisi rahisi tu.

Baada ya siku tatu, mgomo baridi ukawepo ndani ya nyumba. Mwanaume anasema lazima mke wake amuombe samahani. Mke hataki kuomba msamaha. Mke angepika chakuka lakini mume hakula. Kila siku alikuwa akirudi na chakula tokea hotelini (take away).

Mke akasema kama noma na iwe noma, akahama kabisa chumba na kwenda kulala na watoto.

Jumapili moja, walienda kanisani katika ibada. Kila mmoja alienda kivyake na gari yake. Ila ndani ya kanisa katika ibada walikaa pamoja wakijifanya kuwa ni wanandoa wanaopendana! Unafiki ulioje ndani ya nyumba ya Mungu! Mungu awasamehe Wanandoa wanaofanya hivi.

Lakini baada ya ibada mume alitangulia nyumbani na watoto wakati mkewe akisubiri kikao cha wanawake pale kanisani. Siku hiyo shetani aliamua aingilie kati ugomvi walioukaribisha ndani ya ndoa yao.

Mme alikuwa amefika nyumbani tayari, alipoiangalia simu yake, mke wake alikuwa amempigia mara tatu. Hakujisumbua kumpigia baada ya kuziona missed calls. Bifu kali lilikuwepo.

Mkewe akadrive kurudi nyumbani baada ya lisaa limoja. Mume akamuona mlinzi wa mlangoni akifungua geti na huku simu yake ilikuwa ikiita pia. Aliiangalia na kuona ni namba ya mkewe. Na alikuwa kashaingia na gari katika garage ya kupack gari.

"Anapiga kwanini na wakati ashaingia nyumbani? Asilete mahaba yake ya kihindi hapa huu ni upumbavu na utoto!" Mume alisema na kuzipotezea calls za mkewe. Simu iliendelea kuita mume ndio kwanza akakunja nne akitazama sinema

Baada ya nusu saa, mke hakuingia ndani. Kitu kikamwambia mumewe atoke nje akatizame kwanini mkewe haingii ndani. Bado yupo ndani ya gari? Ndio lazima atakuwemo ndani ya gari. Ila kabla akamwita mlinzi wa getini.

"Mama yupo ndani ya gari?" mume aliuliza, mlinzi akajibu " ndio madam amelala ndani ya gari"

Mume akainuka mbio huku akipiga kelele kama mtoto "PUMU! PUMU! PUMU MUNGU WANGU, ITAKUWA IMEMKAMATA KAMA KAWAIDA YAKE, ATAKUWA ALISAHAU KIFAA CHA KUPUMULIA (INHALER).

Haraka haraka akaingia chumbani na kuchukua kifaa cha kupumulia (Inhaler). Alipofika nje katika gari baada ya kufungua mlango alihisi pumzi inataka kumtoka!

Mkewe alikuwa ameegemea usukani wa gari hajitambui.

Yeye pamoja na mlinzi walimbeba na kumweka siti ya nyuma na mume akaliondoa gari kwa kasi kuelekea hospitali ya karibu. Kufika hospitalini baada ya vipimo ikathibitika mke amefariki kwa PUMU!

Kama angepokea simu ya mkewe mapema inawezekana angeokoa maisha ya mkewe. Kama mtaacha ugomvi wenu ndani ya ndoa kwa muda mrefu hupelekea shetani kuingilia huo ugomvi na kusababisha matatizo makubwa.

Mume alilia mno na kujilaumu kwa kuchangia kifo cha mkewe.

Mungu mwenyewe anajua wake wangapi, waume wangapi, watoto wangapi katika familia wamefariki katika mazingira kama hayo ya kukosa msaada kwa sababu tu ya kuchukulia mambo kirahisi rahisi.

Tafadhali sana rafiki wa nuru usiache jua lizame huku bado ukiwa na hasira. Vyovyote vile itakavyokuwa tengeneza amani na mpendwa wako. Hakuna kitu kinauma katika maisha kuishi huku ukijua ulichangia kifo cha mtu fulani. Kumbukumbu hua haifutiki.

Shuka katika farasi wako alie juu sana, omba msamaha pale ulipokosea. Kamwe hauwezi badilika jinsia yako kama utajishusha na kuomba msamaha.

Ndoa ngapi zingeokolewa kama wanandoa kwa umoja wao wangeamua kula kwa pamoja papai nono?

Make a conscious effort today to keep your home intact. I pray you will never weep over your family.
 
Uzi mzuri na unafundisha haswa, hongera mleta uzi huu.

Japo maudhui yaliyomo ndani ya uzi huu, hayaendani kamwe na kichwa cha habari ulichoweka.

Jamaa nafsi itamsuta sana, yaani itamchukua miaka haswa kujifuta hiyo kumbukumbu, wakati mwengine maisha yake yote.

Ahsante!
 
Inauma sana lakini pia mimi ni muhanga wa hasira kali na mgumu wa kutamka neno "nisamehe"
 
Hii stori kila siku mnaileta tu ina nini kwani. Tangu 2009 ipo tu! Khaaa
 
safi sana ila next time usiishie tuuu
kucopy na kupaste tuuu kuwa mbunifu kidogo
 
Daaaah!!! Very very sad ndio maana nasema ndoa huwa na mapenzi siku za mwanzo ila mkishazaa watoto tu yanabaki mazoea.Hii mara nyingi huchangiwa sana na wanawake maana siku hizi ndio style msichana anaku force umuoe huku akionyesha mahaba ya ku pretend,shida yake harusi apate keek akiingia ndani anatamani kutoka nje.
 
Kwenye mahusiano lazima mmoja ajishushe...wote mkiwa mabeberu ugomvi hautoisha
ni kweli, hakuwezi kuwa na mabeberu wawili ndani ya nyumba, saa zingine ni rahisi kujifanya mjinga tu kwa vitu visivyokuwa na msingi saaana
 
Back
Top Bottom