Mtwara Tunagombania Kivuli..

Mtwara Tunagombania Kivuli..

Naiunga mkono serikali yangu kwa 100%.

Hii tabia ni ya kukemewa! tukiwaruhusu wana Mtwara watuyumbishe kwenye gesi basi tujue tunatengeneza tatizo kubwa sana nchi hii. Kesho utasikia wana Kilimanjaro hawataki mlima wao, keshokutwa Mbuga ya mikumi nao watu wa Morogoro wanajimilikisha, mtongondogoo huko Ngorongoro nao wazawa wataidai na kule serengeti nao watatangaza jamhuri yao. Hii ni nchi moja wamarekani waliuana sana kwa ajili ya kuunganisha 50 states hii leo inaitwa USA. Kwa njia yeyote ile lazima wananchi wa Mtwara watambue gesi ni ya wote.
 
Hata kama tunakubaliana, kuwa rasilimali za nchi ziwasaidie pia watu wa eneo inakotoka rasilimali hiyo, lakini kamwe, tusikubaliane na hoja kuwa gesi iliyo Mtwara ni ya WanaMtwara. Kwamba dhahabu ya Geita ni ya watu wa Geita, twiga wa Ruaha ni wa Wahehe na kadhalika. Haya si mawazo mazuri kuyapandikiza katika nchi.

Mkuu maggid naona na wewe unaanza kupotoka kama hawa tunaowaita viongozi, hawana hata busara kwa wananchi na wewe pia unaelekea huko huko walipo hawa viongozi wanaoona ujeuri wao ndio utatatua matatizo ya WanaMtwara.

maggid hebu niambie ni wapi WanaMtwara wamesema gesi si ya Watanzania ni Wanamtwara? Naona unafanya makusudi kutotaka kuwaelewa watu wa Mtwara kama hao viongozi wako wasiotaka kuwaelewa watu wa Mtwara.

maggid Naona unaogopa kusema ukweli ni njaa ndio inayokusukuma kujikomba kwa viongozi Mafisadi ili hali unaujua ukweli wenyewe.

Grow up Man don't dumb like watu wa Magogoni
 
Maggid Mjengwa, ndugu, unaheshimika sana. Binafsi nimefatilia makala zako kwa muda mrefu sana. Sio siri uandishi wako na wakina Fr. Privatus Karugendo, M.M Mwanakijiji, Kondo Tutindaga, Jabir Idrisa, Joster Mwangulumbi, Said Kubenea, Nyaronyo Kicheere, Felix Mwakyembe, Msomaji Raia, Paul Sarwatt, Deus Bugaya, Jenerali Ulimwengu, Lula wa Ndali Mwananzela, Johnson Mbwambo, Ahmed Rajabu,Joseph Mihangwa,
Evarist Chahali n.k umewasaidia sana wananchi kufikiri na wengi wameanza kutambua haki zao za msingi. Sasa Mjengwa leo unaposema wakazi wa Mtwara wanataka gas hiwe yao tu! Wakazi wa Mtwara hawajasema hivyo. Mbona ueleweki!.
 
Air Tanzania,
Asante sana.
Hata kama hukubaliani nami, ukweli unabaki, kuwa kuna dhana potofu inajengeka juu ya gesi inayoitwa sasa ' gesi ya Mtwara' ambayo kimsingi ni gesi ya Tanzania inayopatikana eneo la Mtwara katika ardhi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Vinginevyo social media inatusaidia pia kupanua uhuru wa kujieleza. Ndio demokrasia. Mimi nimesema yangu na wewe umesema yako. Na kuna wanaosoma, kuna wanaochuja pia, kabla ya kumeza.
Maggid,
Iringa

Mkuu maggid naona na wewe unaanza kupotoka kama hawa tunaowaita viongozi, hawana hata busara kwa wananchi na wewe pia unaelekea huko huko walipo hawa viongozi wanaoona ujeuri wao ndio utatatua matatizo ya WanaMtwara.

maggid hebu niambie ni wapi WanaMtwara wamesema gesi si ya Watanzania ni Wanamtwara? Naona unafanya makusudi kutotaka kuwaelewa watu wa Mtwara kama hao viongozi wako wasiotaka kuwaelewa watu wa Mtwara.

maggid Naona unaogopa kusema ukweli ni njaa ndio inayokusukuma kujikomba kwa viongozi Mafisadi ili hali unaujua ukweli wenyewe.

Grow up Man don't dumb like watu wa Magogoni
 
Ni aibu sana kuona watu wenye akili timamu wanapotosha malengo ya wanamtwara. Ni wapi watu wa mtwara wamesema kuwa wanataka mapato ya gesi yawanufaishe wao tu? Mbona mmeingia katika cheap propaganda za Serikali?
 
Nyie akina maggid endeleeni na Propaganda zenu za as if Hamuelewi ( For the sake ya Kuwafurahisha watawala wa CCM) nini Dai la Msingi la Wana Mtwara.
Matokeo yake Mtazidi Kuyaona Jinsi wana Mtwara wanavyowashughulikia watu watu kama Nyie Kule Mtwara.
Nina Uhakika Kabisa Siku wana Iringa wakilianzisha Seke seke kama Hili.
You will be one of the Pesron to first Suffer the Consequences.....
 
Nilikuwa nimekasirishwa sana na upotoshaji wa huyu ndugu lakini baada ya kusoma komenti yako nimecheka sana.
Unaulizia hadi jogging?, nadhani ilikuwa ni siku ile ya vurugu za polisi kuwaonea machinga ndio aliamua kufanya jogging, teh teh teh!
Huyu Jamaa, huwa ni ******* sana, Kila makala / andiko lake anaanza mara oh, "nikiwa jongging", mara... "wazo la Leo", mara "Ya..na mtazamo wangu." mara.."Tafakari ya usiku" huwa hana lolote lile, mtun makini ukimfuatilia haina haja wala ya kusoma makala za maggid wala thread zake zinazokuja kwa jia ya matangazo ya kiji-blog chake.
 
Last edited by a moderator:
Ndugu zangu,
Mwanafalsafa Jean- Paul Sartre anasema; " Hell is the other people" – Kwamba jehanam ni wale wengine, anataka pia tukubaliane, kuwa pepo yaweza kuwa ni wale wengine.

................

Tunajifunza nini?

Kwamba ni kweli Mtwara na sehemu nyingine za nchi zimekuwa nyuma sana kimaendeleo. Na leo tunaposikia Mtwara kuna gesi, nakubaliana na Rais Jakaya Kikwete, kuwa gesi hiyo haiwezi kuwa ni ya WanaMtwara tu. Ni gesi ya Watanzania wote.

Ni vema na ni busara, na kwa kuwashirikisha wazee wa Mtwara, kuwa WanaMtwara wakasikilizwa. Kuna ya msingi ambayo WanaMtwara na Serikali wanaweza kukubaliana kwenye meza ya mazungumzo.

Hata kama tunakubaliana, kuwa rasilimali za nchi ziwasaidie pia watu wa eneo inakotoka rasilimali hiyo, lakini kamwe, tusikubaliane na hoja kuwa gesi iliyo Mtwara ni ya WanaMtwara. Kwamba dhahabu ya Geita ni ya watu wa Geita, twiga wa Ruaha ni wa Wahehe na kadhalika. Haya si mawazo mazuri kuyapandikiza katika nchi.

Ni mawazo ya hatari yanayoweza kupandikiza chuki, sit u miongoni mwa wananchi na Serikali, bali hata miongoni mwa wananchi wenyewe wa maeneo tofauti. Ni mawazo yenye kupandikiza pia fikra za kibaguzi.

Na tufikiri hili, je, kama gesi ile iliyopatikana kule Mtwara, Tanzania na Msumbiji nayo ingesema ni ya kwake, WanaMtwara wangesemaje kama watu wa mikoa mingine ya nchi hii nao wangesema wapelekwe wanajeshi wa Kimakonde, Kiyao na Kimakua tu wakambapane na majeshi ya Msumbiji kutetea ' Gesi ya Mtwara!'?

Naam, ya kule Mtwara isije ikawa yale yale ya kugombania kivuli.

Maggid Mjengwa,

Iringa,
0754 678 252
http://mjengwablog.co.tz
Sina hakika kama unaielewa hoja ya wanaMtwara, na kama inaielewa basi umeamua kuipotosha kwa makusudi au kwa maslahi yako binafsi!

Hakuna hata siku moja wanaMtwara wamedai kuwa gesi ni mali yao peke yao! WanaMtwara wanafahamu kuwa gesi iliyoko kusini ni rasilimali ya taifa kwa manufaa ya waTanzania wote!

Lakini kwa kuzingatia kuwa Mtwara na kusini kwa ujumla uwekezaji ni mdogo, na kwa kuwa umaskini unaowakabili watu wa kusini una historia ndefu wanataka kupitia gesi iwe chachu ya maendeleo kusini! Kwamba kupitia gesi uwekezaji mkubwa utafanyika kusini na hivyo kupelekea wakazi wa kusini wakajikwamua kiuchumi!

Sasa ni jukumu la serikali kukaa na wana kusini pamoja na wadau wote wa maendeleo kuandaa na kuweka mipango mkakati wa kufanikisha ndoto yao!
 
Air Tanzania,
Asante sana.
Hata kama hukubaliani nami, ukweli unabaki, kuwa kuna dhana potofu inajengeka juu ya gesi inayoitwa sasa ' gesi ya Mtwara' ambayo kimsingi ni gesi ya Tanzania inayopatikana eneo la Mtwara katika ardhi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Vinginevyo social media inatusaidia pia kupanua uhuru wa kujieleza. Ndio demokrasia. Mimi nimesema yangu na wewe umesema yako. Na kuna wanaosoma, kuna wanaochuja pia, kabla ya kumeza.
Maggid,
Iringa

Bwana maggid hebu itazame hii picha hapa chini. Hii ndio barabara ya kwenda Mtwara kwa miaka mingi sana. wakati kule Iringa kuna TANZAM Highway huku hakuna na yet yote ni Tanzania hiyohiyo.
Maji%20yajaa,%20yaziba%20Barabara%20Mtwara.JPG

Inawezaje kuwa rahisi leo hii unafika Mtwara na kutaka kujenga bomba la mafuta kwa mwaka na nusu ilhali kwa miaka hamsini barabara imekushinda? Kifupi ni kuwa watawala wetu wameshindwa ku balance fursa sawa kwa maeneo mbalimbali ya nchi.

Suala la gesi ya Mtwara pamoja na uharaka wake lilipaswa kutolewa elimu ya kutosha kwa wananchi na sio kutumia mabavu kulazimisha hoja. Kwa kauli ya waziri yule jana nilijua kuwa yatatokea haya. Angalitamka kwa namna nzuri wala tusingefikia hapa. Sasa ona hata bajeti yake imeahirishwa. Mpiga kura wako unapomwambia "utake usitake hili litafanyika" hata kama ana mapungufu ya kifikra hatokubaliana n wewe.
 
Last edited by a moderator:
Ndugu zangu,
Mwanafalsafa Jean- Paul Sartre anasema; “ Hell is the other people” – Kwamba jehanam ni wale wengine, anataka pia tukubaliane, kuwa pepo yaweza kuwa ni wale wengine.

Na hakika, tofauti ya mwanadamu na mnyama iko kwenye kufiri. Mnyama anaongozwa na hisia, lakini mwanadamu anapaswa aongozwe na kufikiri. Ndio maana ng’ombe anaweza kumpanda mama yake. Ni hisia tu zitakazoongoza tendo lake.

Hivyo, mwanadamu kwenye mambo ya msingi hapaswi kabisa kuongozwa na hisia ikiwamo ushabiki. Anapaswa kfikiri.

Vinginevyo, ni ukweli, kuwa kijamii, mwanadamu anaweza kuwa kiumbe anayeishi kwenye mahusiano ya kirafiki na kiadui na wenzake. Na katika hilo la uadui, wanadamu, kama ilivyo kwa wanyama, wanaweza kushindania na hata kugombania vingi; iwe fedha, mashamba, wanawake na hata kivuli cha mti.

Ndio, unaweza kabisa kuwakuta wanadamu wawili wanagombania kivuli cha mti, kwamba nani mwenye haki ya kukaa kivulini. Na wanaweza kugombana mpaka akatokea mwendawazimu atakayekuja kuukata na huo mti wenyewe. Na wanadamu hao watabaki wakitazama juani.

Hoja yangu hapa, kuwa lililo la msingi ni kuwa wanadamu tunategemeana. Kwamba panapo kushindania jambo, mwanadamu, tofauti na mnyama, anapaswa kufikiri sana. Atangulize kwanza hekima na busara.

Na kwenye mgogoro wowote ule, mwanadamu ayape mazungumzo nafasi ya pekee katika kufikia muafaka, na si vurugu au mapigano. Kwenye mgogoro, na kwenye kuitafuta amani, panakosekana mazungumzo ina maana ya uwepo wa mazingira ya kuvunjika kwa amani. Hapa Serikali inapaswa iandae haraka mazingira ya mazungumzo katika kuitafuta suluhu.

Ndugu zangu,

Nilikuwa shuleni miaka ile ya 80 pale aliyekuwa Waziri Mkuu, Dr. Salim Ahmed Salim alipotembelea Mtwara na kukutana na umasikini uliomstusha sana. Kule Mtwara Dr. Salim alikutana na Watanzania waliovaa magunia na miguuni hawana hata kandambili. Na kwenye jua kali walijipanga kando ya barabara kumpokea. Kwenye jua kali walikusanyika kumsikiliza Waziri Mkuu wao.

Ni kule Mtwara inasemekana Dr. Salim, kwa mara ya kwanza, alipofikia maamuzi ya kutoa ruhusa ya mitumba kuingizwa nchini. Maana, kulikuwa na Watanzania wengine wengi nje ya Mtwara waliokuwa kwenye hali ya umasikini wa kufikia kuvaa nguo za viraka na kushindwa hata kuvaa viatu vya matairi ya magari.

Tunajifunza nini?

Kwamba ni kweli Mtwara na sehemu nyingine za nchi zimekuwa nyuma sana kimaendeleo. Na leo tunaposikia Mtwara kuna gesi, nakubaliana na Rais Jakaya Kikwete, kuwa gesi hiyo haiwezi kuwa ni ya WanaMtwara tu. Ni gesi ya Watanzania wote.

Ni vema na ni busara, na kwa kuwashirikisha wazee wa Mtwara, kuwa WanaMtwara wakasikilizwa. Kuna ya msingi ambayo WanaMtwara na Serikali wanaweza kukubaliana kwenye meza ya mazungumzo.

Hata kama tunakubaliana, kuwa rasilimali za nchi ziwasaidie pia watu wa eneo inakotoka rasilimali hiyo, lakini kamwe, tusikubaliane na hoja kuwa gesi iliyo Mtwara ni ya WanaMtwara. Kwamba dhahabu ya Geita ni ya watu wa Geita, twiga wa Ruaha ni wa Wahehe na kadhalika. Haya si mawazo mazuri kuyapandikiza katika nchi.

Ni mawazo ya hatari yanayoweza kupandikiza chuki, sit u miongoni mwa wananchi na Serikali, bali hata miongoni mwa wananchi wenyewe wa maeneo tofauti. Ni mawazo yenye kupandikiza pia fikra za kibaguzi.

Na tufikiri hili, je, kama gesi ile iliyopatikana kule Mtwara, Tanzania na Msumbiji nayo ingesema ni ya kwake, WanaMtwara wangesemaje kama watu wa mikoa mingine ya nchi hii nao wangesema wapelekwe wanajeshi wa Kimakonde, Kiyao na Kimakua tu wakambapane na majeshi ya Msumbiji kutetea ‘ Gesi ya Mtwara!’?

Naam, ya kule Mtwara isije ikawa yale yale ya kugombania kivuli.

Maggid Mjengwa,

Iringa,
0754 678 252
http://mjengwablog.co.tz

Mawazo mazuri Majid. Lakini basi kumbe kiwanda cha kusaga kahawa ya Kilimanjaro na Bukoba na Mbinga vikajengwe Ntwara kama gesi inavyokwenda DSM kusafishwa! Patamu hapo. Kiwanda cha kusafisha Tanzanite zote za Mererani kijengwe Lindi ati ili kuonyesha mfano.

Mie nasema, wanantwara sio wajinga kivile, lazima wasikilizwe na sio kuburutwa. Jaribu kupeleka maji ya Kilimanjaro yakasafishwiwe Dodoma tu pale ukione cha moto. Acha Majid, acha! Wameenda shule nao Ntwara, wapeni fulsa msisingizie upinzani na nini nini. The core issue here is not to be cheated but be explicit when it come to discussing on real issues that has gross impact to the people around. Kwa nini wasijenge kiwanda cha kusafishia gesi hiyo Ntwara na kingine ndipo wavutie DSM? Huhitaji kwenda shule, Pinda aliwadanganya wazee wa Ntwara ndo maana wamechukia. Wamesota miaka mingi katika dimbwi la umaskini, hakuna hasara kusafisha gas Ntwara ili kuvutia wawekezaji na kuchochea maendeleo kwa kasi zaidi ukweni kwa nzee. AMEKOSEA!
 
Hata kama tunakubaliana, kuwa rasilimali za nchi ziwasaidie pia watu wa eneo inakotoka rasilimali hiyo, lakini kamwe, tusikubaliane na hoja kuwa gesi iliyo Mtwara ni ya WanaMtwara. Kwamba dhahabu ya Geita ni ya watu wa Geita, twiga wa Ruaha ni wa Wahehe na kadhalika. Haya si mawazo mazuri kuyapandikiza katika nchi.

Ni mawazo ya hatari yanayoweza kupandikiza chuki, sit u miongoni mwa wananchi na Serikali, bali hata miongoni mwa wananchi wenyewe wa maeneo tofauti. Ni mawazo yenye kupandikiza pia fikra za kibaguzi.

Iringa,
0754 678 252
http://mjengwablog.co.tz

Mkuu nadhani hata wewe hujawaelewa wanamtwara wanataka nini, au unafanya makusudi kutokuwaelewa, hawajasema gesi ni yao wanasema kuwa wanataka iwanufaishe wao pia, sasa mambo yakuweka mabomba na kuwanufaisha watu wa dar tuu huoni kama mnataka kuzidi kuididimiza mtwara, unakumbuka ni sababu zipi wanazitoa za kwanini mtwara mpaka leo haiendelei? Kanini tusisafirishe final product na viwanda vyoote vya kusafisha na hata mitambo ya umeme isijengwe mtwara? kwanini ile Kinyerezi tuu dar kila kiru? bandari kule imekufa na hakuna hatua zozote zakuiokoa unategemea nini? HAYA MAMBO YANAHITAJI MJADALA MPANA SANA MKUU!
 
Ndugu zangu,
Mwanafalsafa Jean- Paul Sartre anasema; “ Hell is the other people” – Kwamba jehanam ni wale wengine, anataka pia tukubaliane, kuwa pepo yaweza kuwa ni wale wengine.

Na hakika, tofauti ya mwanadamu na mnyama iko kwenye kufiri. Mnyama anaongozwa na hisia, lakini mwanadamu anapaswa aongozwe na kufikiri. Ndio maana ng’ombe anaweza kumpanda mama yake. Ni hisia tu zitakazoongoza tendo lake.

Hivyo, mwanadamu kwenye mambo ya msingi hapaswi kabisa kuongozwa na hisia ikiwamo ushabiki. Anapaswa kfikiri.

Vinginevyo, ni ukweli, kuwa kijamii, mwanadamu anaweza kuwa kiumbe anayeishi kwenye mahusiano ya kirafiki na kiadui na wenzake. Na katika hilo la uadui, wanadamu, kama ilivyo kwa wanyama, wanaweza kushindania na hata kugombania vingi; iwe fedha, mashamba, wanawake na hata kivuli cha mti.

Ndio, unaweza kabisa kuwakuta wanadamu wawili wanagombania kivuli cha mti, kwamba nani mwenye haki ya kukaa kivulini. Na wanaweza kugombana mpaka akatokea mwendawazimu atakayekuja kuukata na huo mti wenyewe. Na wanadamu hao watabaki wakitazama juani.

Hoja yangu hapa, kuwa lililo la msingi ni kuwa wanadamu tunategemeana. Kwamba panapo kushindania jambo, mwanadamu, tofauti na mnyama, anapaswa kufikiri sana. Atangulize kwanza hekima na busara.

Na kwenye mgogoro wowote ule, mwanadamu ayape mazungumzo nafasi ya pekee katika kufikia muafaka, na si vurugu au mapigano. Kwenye mgogoro, na kwenye kuitafuta amani, panakosekana mazungumzo ina maana ya uwepo wa mazingira ya kuvunjika kwa amani. Hapa Serikali inapaswa iandae haraka mazingira ya mazungumzo katika kuitafuta suluhu.

Ndugu zangu,

Nilikuwa shuleni miaka ile ya 80 pale aliyekuwa Waziri Mkuu, Dr. Salim Ahmed Salim alipotembelea Mtwara na kukutana na umasikini uliomstusha sana. Kule Mtwara Dr. Salim alikutana na Watanzania waliovaa magunia na miguuni hawana hata kandambili. Na kwenye jua kali walijipanga kando ya barabara kumpokea. Kwenye jua kali walikusanyika kumsikiliza Waziri Mkuu wao.

Ni kule Mtwara inasemekana Dr. Salim, kwa mara ya kwanza, alipofikia maamuzi ya kutoa ruhusa ya mitumba kuingizwa nchini. Maana, kulikuwa na Watanzania wengine wengi nje ya Mtwara waliokuwa kwenye hali ya umasikini wa kufikia kuvaa nguo za viraka na kushindwa hata kuvaa viatu vya matairi ya magari.

Tunajifunza nini?

Kwamba ni kweli Mtwara na sehemu nyingine za nchi zimekuwa nyuma sana kimaendeleo. Na leo tunaposikia Mtwara kuna gesi, nakubaliana na Rais Jakaya Kikwete, kuwa gesi hiyo haiwezi kuwa ni ya WanaMtwara tu. Ni gesi ya Watanzania wote.

Ni vema na ni busara, na kwa kuwashirikisha wazee wa Mtwara, kuwa WanaMtwara wakasikilizwa. Kuna ya msingi ambayo WanaMtwara na Serikali wanaweza kukubaliana kwenye meza ya mazungumzo.

Hata kama tunakubaliana, kuwa rasilimali za nchi ziwasaidie pia watu wa eneo inakotoka rasilimali hiyo, lakini kamwe, tusikubaliane na hoja kuwa gesi iliyo Mtwara ni ya WanaMtwara. Kwamba dhahabu ya Geita ni ya watu wa Geita, twiga wa Ruaha ni wa Wahehe na kadhalika. Haya si mawazo mazuri kuyapandikiza katika nchi.

Ni mawazo ya hatari yanayoweza kupandikiza chuki, sit u miongoni mwa wananchi na Serikali, bali hata miongoni mwa wananchi wenyewe wa maeneo tofauti. Ni mawazo yenye kupandikiza pia fikra za kibaguzi.

Na tufikiri hili, je, kama gesi ile iliyopatikana kule Mtwara, Tanzania na Msumbiji nayo ingesema ni ya kwake, WanaMtwara wangesemaje kama watu wa mikoa mingine ya nchi hii nao wangesema wapelekwe wanajeshi wa Kimakonde, Kiyao na Kimakua tu wakambapane na majeshi ya Msumbiji kutetea ‘ Gesi ya Mtwara!’?

Naam, ya kule Mtwara isije ikawa yale yale ya kugombania kivuli.

Maggid Mjengwa,

Iringa,
0754 678 252
http://mjengwablog.co.tz
mikataba ikwekwa mezani na watu wakaijua tu nadhani fujo zitapungua otherwise hako kampango kampango ka choma nyumba za waheshimiwa kataendelea
 
Air Tanzania,
Asante sana.
Hata kama hukubaliani nami, ukweli unabaki, kuwa kuna dhana potofu inajengeka juu ya gesi inayoitwa sasa ' gesi ya Mtwara' ambayo kimsingi ni gesi ya Tanzania inayopatikana eneo la Mtwara katika ardhi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Vinginevyo social media inatusaidia pia kupanua uhuru wa kujieleza. Ndio demokrasia. Mimi nimesema yangu na wewe umesema yako. Na kuna wanaosoma, kuna wanaochuja pia, kabla ya kumeza.
Maggid,
Iringa

Maggid, mimi naona wewe ndio umeamua siku hizi kutokueleweka katika presentations zako maana wakati unatoka Ilala unataka kwenda Kariakoo badala kupitia shule ya Uhuru wewe unaamua kwenda Kigogo, Ubungo Mwenge na baadae unapitai Sinza kuelekea Kariakoo. Waingereza wanaiita beating about a bush. Hukupaswa kuja na heading ambayo contraversial badala na mifano ambayo ni uncorrelative kama kugombania kivuli. You could have stated blatatantly kuwa serikali inapaswa ikae na wakazi wa Mtwara kupitia wawakilishi a wide population ya Mtwara from the beginning ili wawe na mwafaka as to how the revenues generated from gas and products will equally and equitably slacided. Halafu baada ya hapo serikali ingetunga sera and policies that will guide gas exprolation and exploitation na baadae ikaita wawekezaji wa ndani na nje kupitia matangazo ya wazi ya kitaifa na makitaifa. Wawekezaji wangeomba na kushindanishwa na baadae the best bidder be awarded a contract. Mkataba ungewekwa wazi kwa wananchi kupitia bungeni ili tuone kama una maslahi mapana. Sasa kumekuwa na usiri wa mkataba wa bomba na sera ya hesi haipo. Wanamtwara amabao watakuwa wanapata madhala yatokanayo na uzalishaji wa gesi kwanini wasishtuke? Hapa hakuna kutafuta mchawi iambie serikali/CCM wafute mkataba wa bomba la gesi na uzalishaji wakae kwanza na WanaMtwara waafikiane kwa uwazi na their resoloutions should be documented and baadae wapitie kwenye competitive procedures whereby all prosprct investors will submit their tenders. To err is human but to exist in error is devilish. Tushakosea kwenye mikataba ya nyuma tena wahusika ni walewale. Sasa wanakuja tena kwa style ileile lakini katika wakati tofauti
 
Hili andiko mbona limeelemea upande mmoja?
maggid huu ni udhaifu usiokuwa wa kawaida kutoka kwa mtu wa kaliba yako.
 
Very right Brother Maggid, huyo huyo Dr. Salim akiwa PM alipokuwa Lindi katika sherehe ya kumpokea, kulikuwa na wasichana [miaka 10-15] wakamchezea ngoma wakiwa wamevaa vitambaa viunoni bila kitu juu, yaani maziwa wazi. Dr. Salim alifedheheka sana, ikawa ndiyo kama asemavyo Maggid, sababu ya kuruhusu mitumba. Sasa, watu wa Mtwara na Lindi wanajua kwa usahihi zaidi, umasikini maana yake nini. Mtu akija kuchezea fursa waliyopata na kutaka kufanya ya Nyamongo, Geita, Bulyankuru, ama BUZWAGI nk, hapa hata mimi nawaunga mkono. Maana si tunajua serikali inavyofanya katika miradi kama hii? Kaeni mzungumze siyo kupiga mabomu hakusaidii, mabomu yalipigwa kwa Libya, Tunisia, Misri sasa Syria. Msichezee maisha ya watu, mnajitafutia LAANA iliyomkuta Hitler.
 
Ni aibu sana kuona watu wenye akili timamu wanapotosha malengo ya wanamtwara. Ni wapi watu wa mtwara wamesema kuwa wanataka mapato ya gesi yawanufaishe wao tu? Mbona mmeingia katika cheap propaganda za Serikali?

maggid anajifanya hajui madai ya wanamtwara, yote ni njaa inayomsumbua maggid hana tofauti na Nape au Nchemba

maggid anafanyamakusidi kutoelewa madai ya wanamtwara
 
Nimpongeze ndugu yangu maggid leo kajitahidi kweli kweli nimemzoea kila akianzisha thread anatimua mbio leo yuko hapa samba samba akidadavua hoja zenu bila chenga.
 
Last edited by a moderator:
nadhani huyu kijana maggid hajaua wanamtwara tunataka nni
hebu fanya research ya kutosha ndo uongee
 
Back
Top Bottom