Mtwara Tunagombania Kivuli..

Mtwara Tunagombania Kivuli..

Nimpongeze ndugu yangu maggid leo kajitahidi kweli kweli nimemzoea kila akianzisha thread anatimua mbio leo yuko hapa samba samba akidadavua hoja zenu bila chenga.

Ngongo,
Ahsante sana.
Hakika nimefurahia mjadala huu, maana, tofauti na mara nyingi, naona leo wengi wamejikitika kujadili hoja iliyo mezani badala ya kumjadili mtoa hoja. Ni mwelekeo wa mjadala kama huo wa mwisho ( kumjadili mtoa hoja) ndio mara nyingi hunifanya niishie kwenye kusoma comments tu lakini si kuchangia. Maana, ukianza kuchangia yenye kukujadili wewe mtoa hoja ina maana pia ya kuchangia kwenye kushusha kiwango cha mjadala.
Maggid,
Iringa.
 
Kwa jinsi maggid alivyo mchoyo huwa naona analalama kwenye blog yake pale bloggers wengine wanapochukua habari au picha toka kwake! Anawaandika kwenye blog yake na kulalama sijui ni kwa nini haoni mantiki ya hoja za wanamtwara!

Maggid acha unafiki vile ambavyo huwa unawalalamikia bloggers wengine kuchukua taarifa au picha toka kwako ndivyo hivyo hivyo na kwa kipimo hichohicho wana Mtwara wanalalamikia gas yao!
 
Ngongo,
Ahsante sana.
Hakika nimefurahia mjadala huu, maana, tofauti na mara nyingi, naona leo wengi wamejikitika kujadili hoja iliyo mezani badala ya kumjadili mtoa hoja. Ni mwelekeo wa mjadala kama huo wa mwisho ( kumjadili mtoa hoja) ndio mara nyingi hunifanya niishie kwenye kusoma comments tu lakini si kuchangia. Maana, ukianza kuchangia yenye kukujadili wewe mtoa hoja ina maana pia ya kuchangia kwenye kushusha kiwango cha mjadala.
Maggid,
Iringa.
maggid,

..mara nyingi post zako huwa zina ukakasi wa chama cha magamba.

..hicho ndicho kinachopelekea wachangiaji wakuandame binafsi.

..leo ume-post vitu vinavyoeleweka na umeona kila mtu anavyo-appreciate.

..hongera sana!! keep it up!!
 
Last edited by a moderator:
Mkuu. Nadhani hao wanaosema kuwa watu wa Mtwara hawataki gesi isitumike na watu wengine, wanajua fika kuwa hilo si kweli, bali wanasema kwa makusudi tu kupotosha ukweli wa kile watu wa Mtwara wanachokitaka. Wanapotosha usemi huo ili jamii ione kuwa watu wa Mtwara hawana hoja za msingi na ni wachoyo.

Kitu amacho watu wa Mtwara wanachokitaka ni gesi kufuliwa pale pale Mtwara ili kuongeza ufanisi wa kiuchumi wa sehemu hiyo kwa sekta mbalimbali. Hakuania haja ya kujenga bomba la gesi ipelekwe mbali wakati kuna uwezekano wa kufuliwa hapo hapo.

kiongozi kwani Gesi haitakua na matumizi mengine zaidi ya kufua umeme? na kama yapo vip itasambazwa vip?
Kwani nichofaham PM alikubali kua UMEME utafuliwa Mtwara na pia grid ya taifa itafika Mtwara na ndivy alivyorudia JK jana wakati anafungua barabara. sasa fujo zinatokana na nini wakati walikubaliana PM umeme utafuliwa huko.
 
Siongelei matumizi ya gesi wala chochote kitokanacho na hiyo gesi. Ninachoongelea hapa ni maneno ya viongozi kutuambia sisi wananchi kuwa watu wa Mtwara wanataka watumie hiyo gesi peke yao, na Watanzania wengine wasifaidike. Niliposikiliza manung'uniko ya watu wa Mtwara sikuelewa hivyo. Hata katika kutaka kuelimisha umma, kuna upotoshaji dhahiri wa habari. Kufanya hivyo si vizuri kwani kunaleta hisia za wananchi kutokuamini kauli za viongozi na serikali kwa ujumla.
 
We jamaaa mweupe kama karatasi, Ndio maan unandikaga upuzii na kukimbia badala ya kutetea hoja zako za kijinga kama hizi.

Mmejitahidi sana kupotosha kuwa wanmtwara hawatali gesi itoke kisa wanataka kufaidi wenyewe kitu ambacho sio kweli.

We ni mbumbumbuu mwisho wa relin inauzi sana kunaokuwa na watu kama wewe walio tayari kupotosha umma.
 
kiongozi kwani Gesi haitakua na matumizi mengine zaidi ya kufua umeme? na kama yapo vip itasambazwa vip?
Kwani nichofaham PM alikubali kua UMEME utafuliwa Mtwara na pia grid ya taifa itafika Mtwara na ndivy alivyorudia JK jana wakati anafungua barabara. sasa fujo zinatokana na nini wakati walikubaliana PM umeme utafuliwa huko.

Sio grid ifike mntwara, Grid ianze Mtwara.
 
Siongelei matumizi ya gesi wala chochote kitokanacho na hiyo gesi. Ninachoongelea hapa ni maneno ya viongozi kutuambia sisi wananchi kuwa watu wa Mtwara wanataka watumie hiyo gesi peke yao, na Watanzania wengine wasifaidike. Niliposikiliza manung'uniko ya watu wa Mtwara sikuelewa hivyo. Hata katika kutaka kuelimisha umma, kuna upotoshaji dhahiri wa habari. Kufanya hivyo si vizuri kwani kunaleta hisia za wananchi kutokuamini kauli za viongozi na serikali kwa ujumla.

Serekali mufilisi haina majibu na ushahidi upo wazi, maana ukiendwa kila kwewnye songosongo ni umesikini tu umetamalaki,
Tuliahidiwa bidhaa kupugua bei lakini hadi leo kimyaaa!
 
watu wanapiga kelele gesi gesi,gesi ambayo hata hawajahi kuion,hivi mnajua kuwa gesi sonosongo isahaanza kuchimbwa miaka kadhaa na inakuja huku dar??imeshatusaidia nini hadi sasa???hiki ndio kitu watu wa mtwara wanahoji kwa sauti sasa,vip mradi wa Artumas,uliwasaidia nini watu hao zaidi ya changa la macho tu??na n i nani ajuajye gharama sahihi za kuchimba visima hivyo zaidi ya kuambiwa tu na wanasiasa ambao nao wanamezeshwa na hao wanaokuja na mkatab??sidhani kama wanasiasa wanaoingia mkataba wanaangalia uhalisia wa gharama za uzalishaji(Costs of production),kama sivyo tutaendelea kuumia tu
 
Kila mmoja anashauri pande zote zikae chini/mezani waongee na pia wanamtwara wapewe nafasi ya kusilizwa.
Hapa najiuliza mbona hayo siyo mapya tuliyasikia mara tu baada ya zile vurugu za kwanza na tumeyasikia kutoka kwa wengi akiwepo rais mstaafu Mh Mkapa naye ni wa huko. Tatizo langu ni je kwani wale viongozi wote walioenda huko kutoka serikalini na kuhitimishwa na Waziri Mkuu wao walifanya nini-mbona kama vile walikaa nao na kuyaongea ikiwa ni pamoja na kuwasikiliza? Au wapi palikosewa-isije ikawa badala ya kuwasilikiliza tuliwaambia na kutangaza tumeyamaliza.
 
Maggid,

Napingana na analogy yako kuwa "Mtwara tunagombania kivuli." Watu wa Mtwara wanagombana na serikali ambayo imewaweka pembeni kwa muda mrefu. Serikali ambayo inafikiria ya kuwa Tanzania kila kitu kinatakiwa kiwe-centralized au karibu na Dar es Salaam (Bagamoyo). Serikali ambayo inasign mikataba ya gesi kwa siri na bila ya kuaanda mazingira yatakayowanufaisha wananchi wa Mtwara na Tanzania kwa ujumla. Juzi hapa Mheshimiwa Zitto alikuja hapa na kulalamika juu ya mapungufu yaliyopo kwenye hiyo mikataba, tafadhali soma hii link: Zitto, Mnyika wapasua Bunge .

Kitu kinachotokea Mtwara ni symptoms tuu za tatizo kubwa litakaloikabiri nchi yetu kama hatutaanza kufikiri nje ya sanduku. Kusema kwamba watu wa Mtwara ni wa binafsi, hakutatua tatizo bali ni kuzidi kuweka mafuta ya taa kwenye moto. Tunachokiona Mtwara ni matokeo ya vijana wengi kukosa kazi na sera mbovu za serikali za CCM. Vijana wengi hawana ajira, na gap kati ya mwenye nacho na asiye nacho linazidi kuongezeka. Vijana wengi imefika sehemu wanaona hawana cha kupoteza " they have nothing to lose." Na mwanadamu akishafika hiyo point anahitaji kichocheo " catalyst" tuu na kugeuka mnyama.

Maggid, wewe mwenyewe umeandika kwenye Blog yako vijana wanavyochoma mji wa Stockhlom, jee itakuwa sawa kusema vijana wale ni wabinafsi na wanataka kuwanya'nganya wazawa kazi? Ukiangalia vizuri utaona vijana wale wa Stockholm na wa- Mtwara wana vitu vingi vinavyofanana...Wote wanaona ya kuwa wamesahaulika katika gawiwo la taifa.

Mwisho, wakati umefika kwa viongozi kutambua ya kuwa dunia hii ya leo sio ya jana. Amani haipatikani kwa kupitisha Polisi kwenye kila nyumba Mtwara na kukamata vijana wote wa kiume ni kukosa busara na kuzidi kujenga chuki kati Jeshi la Polisi na wananchi. Jeshi la Polisi lazima lijifunze kushinda mafikirio na mioyo (to win hearts and minds) za Wana-Mtwara. Wamarekani walifanya makosa kama yanayofanywa na Jeshi letu huko Iraq, waliingia kila nyumba usiku na kuwakuta watu wakiwa na wake zao faraga! Jambo hili liliwaudhi sana Wa-Iraq na lilijenga mbegu mbaya za chuki.

Itaendelea....
 
Ndugu zangu,
Mwanafalsafa Jean- Paul Sartre anasema; “ Hell is the other people” – Kwamba jehanam ni wale wengine, anataka pia tukubaliane, kuwa pepo yaweza kuwa ni wale wengine.

Na hakika, tofauti ya mwanadamu na mnyama iko kwenye kufiri. Mnyama anaongozwa na hisia, lakini mwanadamu anapaswa aongozwe na kufikiri. Ndio maana ng’ombe anaweza kumpanda mama yake. Ni hisia tu zitakazoongoza tendo lake.

Hivyo, mwanadamu kwenye mambo ya msingi hapaswi kabisa kuongozwa na hisia ikiwamo ushabiki. Anapaswa kfikiri.

Vinginevyo, ni ukweli, kuwa kijamii, mwanadamu anaweza kuwa kiumbe anayeishi kwenye mahusiano ya kirafiki na kiadui na wenzake. Na katika hilo la uadui, wanadamu, kama ilivyo kwa wanyama, wanaweza kushindania na hata kugombania vingi; iwe fedha, mashamba, wanawake na hata kivuli cha mti.

Ndio, unaweza kabisa kuwakuta wanadamu wawili wanagombania kivuli cha mti, kwamba nani mwenye haki ya kukaa kivulini. Na wanaweza kugombana mpaka akatokea mwendawazimu atakayekuja kuukata na huo mti wenyewe. Na wanadamu hao watabaki wakitazama juani.

Hoja yangu hapa, kuwa lililo la msingi ni kuwa wanadamu tunategemeana. Kwamba panapo kushindania jambo, mwanadamu, tofauti na mnyama, anapaswa kufikiri sana. Atangulize kwanza hekima na busara.

Na kwenye mgogoro wowote ule, mwanadamu ayape mazungumzo nafasi ya pekee katika kufikia muafaka, na si vurugu au mapigano. Kwenye mgogoro, na kwenye kuitafuta amani, panakosekana mazungumzo ina maana ya uwepo wa mazingira ya kuvunjika kwa amani. Hapa Serikali inapaswa iandae haraka mazingira ya mazungumzo katika kuitafuta suluhu.

Ndugu zangu,

Nilikuwa shuleni miaka ile ya 80 pale aliyekuwa Waziri Mkuu, Dr. Salim Ahmed Salim alipotembelea Mtwara na kukutana na umasikini uliomstusha sana. Kule Mtwara Dr. Salim alikutana na Watanzania waliovaa magunia na miguuni hawana hata kandambili. Na kwenye jua kali walijipanga kando ya barabara kumpokea. Kwenye jua kali walikusanyika kumsikiliza Waziri Mkuu wao.

Ni kule Mtwara inasemekana Dr. Salim, kwa mara ya kwanza, alipofikia maamuzi ya kutoa ruhusa ya mitumba kuingizwa nchini. Maana, kulikuwa na Watanzania wengine wengi nje ya Mtwara waliokuwa kwenye hali ya umasikini wa kufikia kuvaa nguo za viraka na kushindwa hata kuvaa viatu vya matairi ya magari.

Tunajifunza nini?

Kwamba ni kweli Mtwara na sehemu nyingine za nchi zimekuwa nyuma sana kimaendeleo. Na leo tunaposikia Mtwara kuna gesi, nakubaliana na Rais Jakaya Kikwete, kuwa gesi hiyo haiwezi kuwa ni ya WanaMtwara tu. Ni gesi ya Watanzania wote.

Ni vema na ni busara, na kwa kuwashirikisha wazee wa Mtwara, kuwa WanaMtwara wakasikilizwa. Kuna ya msingi ambayo WanaMtwara na Serikali wanaweza kukubaliana kwenye meza ya mazungumzo.

Hata kama tunakubaliana, kuwa rasilimali za nchi ziwasaidie pia watu wa eneo inakotoka rasilimali hiyo, lakini kamwe, tusikubaliane na hoja kuwa gesi iliyo Mtwara ni ya WanaMtwara. Kwamba dhahabu ya Geita ni ya watu wa Geita, twiga wa Ruaha ni wa Wahehe na kadhalika. Haya si mawazo mazuri kuyapandikiza katika nchi.

Ni mawazo ya hatari yanayoweza kupandikiza chuki, sit u miongoni mwa wananchi na Serikali, bali hata miongoni mwa wananchi wenyewe wa maeneo tofauti. Ni mawazo yenye kupandikiza pia fikra za kibaguzi.

Na tufikiri hili, je, kama gesi ile iliyopatikana kule Mtwara, Tanzania na Msumbiji nayo ingesema ni ya kwake, WanaMtwara wangesemaje kama watu wa mikoa mingine ya nchi hii nao wangesema wapelekwe wanajeshi wa Kimakonde, Kiyao na Kimakua tu wakambapane na majeshi ya Msumbiji kutetea ‘ Gesi ya Mtwara!’?

Naam, ya kule Mtwara isije ikawa yale yale ya kugombania kivuli.

Maggid Mjengwa,

Iringa,
0754 678 252
http://mjengwablog.co.tz
....swadakta ulichosea..! kinachoendelea mtwara ni tatizo pana ambalo kadri muda utakavyoendelea ndivyo, litakavyozidi kukua, labda tu...! (siasa na) wanasiasa waache kucheza mchezo wa siasa kupitia haki za wanamtwara juu ya gesi inayotoka mtwara"....vijana wa kawaida wa mtaani wa mtwara kwa kiasi kikubwa hawajaeleweshwa vya kutosha namna mipango iliyopo kuhusiana na gesi,(ipo) itakavyoinufaisha mtwara, na wakazi wake,( na lindi na wakazi wa lindi pia)..lakini pia, maandali na mikakati ya kivitendo kuwaandaa vijana wa mitaani wa mtwara kuingia katika( chambilecho, rais jakaya kikwete) uchumi mkubwa wa gesi inaelekea ni ya kusuasua, ikiwa imeachwa mbali na mikakati, na maandalizi ya wanasiasa, na wajanja wengine katika kuwaandaa vijana " wa kawaida wa mitaani" kufanya yanayofanyika , na tunayoyashuhudia sasa..!..kwa kina sisi ambao tunayumba na ukweli, sasa tuko kwenye fursa ya kushuhudia ukweli wa "kauli tata" iliyowahi tolewa na wanasiasa( nadhani wa vyama pinzani na kinachoongoza nchi), kwamba tatizo ni udhaifu wa raisi...na kama anavyotufundisha marehem shaaban roberts katika kazi yake ya " adili na nduguze", kwamba mbwa wa msasi mkali, ni wakali kama msasi mwenyewe..basi na tutazame...!
 
Huyu Jamaa, huwa ni ******* sana, Kila makala / andiko lake anaanza mara oh, "nikiwa jongging", mara... "wazo la Leo", mara "Ya..na mtazamo wangu." mara.."Tafakari ya usiku" huwa hana lolote lile, mtun makini ukimfuatilia haina haja wala ya kusoma makala za maggid wala thread zake zinazokuja kwa jia ya matangazo ya kiji-blog chake.

Like haitoshi nakuunga mkona kwa haswa
 
Binafsi sijui process ya gas kuanzia kuvunwa hadi kutumika, sijui kama inapitia process za kusafishwa kwenye matanuru kama dhahabu au inaanza kutumika baada ya kuvunwa kutoka ardhini: vyovyote vile inavyokuwa mimi nadhani pande zote mbili zina hoja ya msingi, serikali wana hoja ya msingi na wana mtwara pia wa hoja ya msingi. Ninavyojua mimi matumizi ya gas sio kuzalishia tu umeme, bali ni pamoja na kuendeshea mitambo kwenye viwanda, inaweza kutumika kwenye magari lakini pia inaweza kutumika majumbani na mahotelini kwa ajili ya kupikia ambako Dar es Salaam ndo kuna soko kubwa na huo ndo umhimu wa hilo bomba kujengwa. Lakini pia kama inapitia process za kusafishwa na kama processing plants zikijengwa mtwara wana mtwara watapata ajira.

Serikali ingekaa na hawa watu waongee wapate kuelewana na kama watatumia ubabe hujuma dhidi ya bomba linalojengwa haitakoma. Ndugu zetu kule Kahama walipambana sana mwaka 96 wakati machimbo ya bulyanhulu yanabinafisishwa kwa Barrick matokeo yake ndugu zetu wengine waliishia kufukiwa. RIP wote mliofukiwa 1996 na RIP wote wana mtwara mliokufa kwenye sakata hili la gesi.
 
.......vijana wa mtwara(kama walivyo vijana wengine wengi katika maeneo mengine ya jamhuri ya muungano), wanaendelewa kutumiwa na watu wenye maslahi yao binafsi yaliyojificha ya kisiasa, na kiuchumi...! inatia shaka kama kuna anaewaambia ukweli..serikali, ina ukweli labda, lakini imeshindwa kuoanisha ukweli wa mipango na mikakati yake ya kuwaingiza vijana wa mtwara na lindi (na hapa tunazungumzia vijana wa kawaida wa mitaani), kivitendo, labda kwa hofu ya kutakuwa hakuna nafasi kwa vijana (watoto) wao na wanaowapigia kura katika majimbo yao ( nakumbuka taarifa za miaka ile kwenye mgodi mmoja mkubwa wa dhahabu ktk mkoa wa shinyanga ambao, walinzi walikuwa ni vijana wa kimasai) ...na hofia, kwa sababu tanzania ni kubwa na kila mahali kuna utajiri ambao una mchango mkubwa katika jamhuri ya muungano...namuwahi diwani wangu anieleze mikakati ya kuhakikisha namna vijana wa maeneo yetu, jirani na uwanja wa taifa, tunavyoweza kunufaika moja kwa moja na "biashara zote, na zabuni zote zenye kuweza toa ajira na zenye maslahi ya kiuchumi ili tupewe kipaumbele...!
 
Ndugu zangu,
Mwanafalsafa Jean- Paul Sartre anasema; “ Hell is the other people” – Kwamba jehanam ni wale wengine, anataka pia tukubaliane, kuwa pepo yaweza kuwa ni wale wengine.

Na hakika, tofauti ya mwanadamu na mnyama iko kwenye kufiri. Mnyama anaongozwa na hisia, lakini mwanadamu anapaswa aongozwe na kufikiri. Ndio maana ng’ombe anaweza kumpanda mama yake. Ni hisia tu zitakazoongoza tendo lake.

Hivyo, mwanadamu kwenye mambo ya msingi hapaswi kabisa kuongozwa na hisia ikiwamo ushabiki. Anapaswa kfikiri.

Vinginevyo, ni ukweli, kuwa kijamii, mwanadamu anaweza kuwa kiumbe anayeishi kwenye mahusiano ya kirafiki na kiadui na wenzake. Na katika hilo la uadui, wanadamu, kama ilivyo kwa wanyama, wanaweza kushindania na hata kugombania vingi; iwe fedha, mashamba, wanawake na hata kivuli cha mti.

Ndio, unaweza kabisa kuwakuta wanadamu wawili wanagombania kivuli cha mti, kwamba nani mwenye haki ya kukaa kivulini. Na wanaweza kugombana mpaka akatokea mwendawazimu atakayekuja kuukata na huo mti wenyewe. Na wanadamu hao watabaki wakitazama juani.

Hoja yangu hapa, kuwa lililo la msingi ni kuwa wanadamu tunategemeana. Kwamba panapo kushindania jambo, mwanadamu, tofauti na mnyama, anapaswa kufikiri sana. Atangulize kwanza hekima na busara.

Na kwenye mgogoro wowote ule, mwanadamu ayape mazungumzo nafasi ya pekee katika kufikia muafaka, na si vurugu au mapigano. Kwenye mgogoro, na kwenye kuitafuta amani, panakosekana mazungumzo ina maana ya uwepo wa mazingira ya kuvunjika kwa amani. Hapa Serikali inapaswa iandae haraka mazingira ya mazungumzo katika kuitafuta suluhu.

Ndugu zangu,

Nilikuwa shuleni miaka ile ya 80 pale aliyekuwa Waziri Mkuu, Dr. Salim Ahmed Salim alipotembelea Mtwara na kukutana na umasikini uliomstusha sana. Kule Mtwara Dr. Salim alikutana na Watanzania waliovaa magunia na miguuni hawana hata kandambili. Na kwenye jua kali walijipanga kando ya barabara kumpokea. Kwenye jua kali walikusanyika kumsikiliza Waziri Mkuu wao.

Ni kule Mtwara inasemekana Dr. Salim, kwa mara ya kwanza, alipofikia maamuzi ya kutoa ruhusa ya mitumba kuingizwa nchini. Maana, kulikuwa na Watanzania wengine wengi nje ya Mtwara waliokuwa kwenye hali ya umasikini wa kufikia kuvaa nguo za viraka na kushindwa hata kuvaa viatu vya matairi ya magari.

Tunajifunza nini?

Kwamba ni kweli Mtwara na sehemu nyingine za nchi zimekuwa nyuma sana kimaendeleo. Na leo tunaposikia Mtwara kuna gesi, nakubaliana na Rais Jakaya Kikwete, kuwa gesi hiyo haiwezi kuwa ni ya WanaMtwara tu. Ni gesi ya Watanzania wote.

Ni vema na ni busara, na kwa kuwashirikisha wazee wa Mtwara, kuwa WanaMtwara wakasikilizwa. Kuna ya msingi ambayo WanaMtwara na Serikali wanaweza kukubaliana kwenye meza ya mazungumzo.

Hata kama tunakubaliana, kuwa rasilimali za nchi ziwasaidie pia watu wa eneo inakotoka rasilimali hiyo, lakini kamwe, tusikubaliane na hoja kuwa gesi iliyo Mtwara ni ya WanaMtwara. Kwamba dhahabu ya Geita ni ya watu wa Geita, twiga wa Ruaha ni wa Wahehe na kadhalika. Haya si mawazo mazuri kuyapandikiza katika nchi.

Ni mawazo ya hatari yanayoweza kupandikiza chuki, sit u miongoni mwa wananchi na Serikali, bali hata miongoni mwa wananchi wenyewe wa maeneo tofauti. Ni mawazo yenye kupandikiza pia fikra za kibaguzi.

Na tufikiri hili, je, kama gesi ile iliyopatikana kule Mtwara, Tanzania na Msumbiji nayo ingesema ni ya kwake, WanaMtwara wangesemaje kama watu wa mikoa mingine ya nchi hii nao wangesema wapelekwe wanajeshi wa Kimakonde, Kiyao na Kimakua tu wakambapane na majeshi ya Msumbiji kutetea ‘ Gesi ya Mtwara!’?

Naam, ya kule Mtwara isije ikawa yale yale ya kugombania kivuli.

Maggid Mjengwa,

Iringa,
0754 678 252
http://mjengwablog.co.tz

another propagandist on board, nani kakuambia watu wa mtwara wanataka gesi itumike mtwara tu, acha unafiki
 
Hiyo tafasiri uliyotoa nadhani mtu yeyote angeitafasiri, siyo kiphilosophia kama unavyodai wewe ni msomi wa vitabu hiyo ni sisisi tafasiri...hebu hilo la usomi wako ngonja nikuachie mwenyewe na maono yako.
Kwanini machingas wanajulikana kila kona ya Tanzania? hawa ni vijana wa Mtwara wa kimakonde na makabira mengine ya kusini. na ukiangalia hili neno machinga limetokea katika miongo miwili iliyopita....katika miaka ya awali halikuwa ni tatazo hata hivyo wenye akili waliona hili lilikuwa ni tatizo lililolala. wanasiasa waliona ni sehemu tu kurupushani za kutafuta maisha. Sasa katika kuangalia kwa kina hii generation iliyoenda kutafuata maisha dar haijanikiwa, huku nyuma korosho hailipi, bandari haitumiki na wenyeji wa mtwara wanajua haya yote. yumkini Mungu si Athumani gesi imengunduliwa wananchi wamtwara wanaona neema hiyo inakuja.....wait a minute! no gesi hiyo itasafirishwa kwenda dar- labda bagamoyo ambako kuna mchakato wa ujenzi wa bandari mpya...kweli hapa "adui mwombee njaa". mwananchi wa kawaida haelewi kwanini mauza mauza yanatokeo mbele yao. na hapa wanamtwara waimbe TANU yajenga nchi na sina uhakika kama wanajua tumepata uhuru na kama wanajua basi nyerere yuko hai......wala hajui Benjamin mkapa alikuwa rais kwa miaka kumi na sasa kuna rais anayesafiri nchi za nje kama mgeni nchini kwake ......haya baadhi ya maajabu ya uongozi tanzania.
Sasa kwanini watu wa Geita hawapingi dhahabu yao kuibiwa na serikari kuambulia peanut percent ya dhahabu inayopatikana. au inahusu nini wananchi wa Tarime kumwangiwa chemically katika vyazo vya maji, na wewe mjengwa mwandishi wa kutafasiri falsafa za vitabu vya kale na kujifanya unaidea original kumbe copy and then tafasiri....na cha kushangaza zaidi ukiwaponda waandishi wa Tanzania eti hawasomi vitabu...really? una haki ya kuongea chochote kile lakini usiwafanye watanzania wamechelewa "SIAFU WAMEKAZANA" ni matter of time na muda ndio huu. ....waandishi mahiri kama akina Ulimwengu wanayajua matatizo ya uongozi wa nchi hii lakini wewe meno juu kila linalotukia katika tanzania unatafasiri yake...really! give me a break!
 
Ndugu zangu,
Mwanafalsafa Jean- Paul Sartre anasema; “ Hell is the other people” – Kwamba jehanam ni wale wengine, anataka pia tukubaliane, kuwa pepo yaweza kuwa ni wale wengine.

Na hakika, tofauti ya mwanadamu na mnyama iko kwenye kufiri. Mnyama anaongozwa na hisia, lakini mwanadamu anapaswa aongozwe na kufikiri. Ndio maana ng’ombe anaweza kumpanda mama yake. Ni hisia tu zitakazoongoza tendo lake.

Hivyo, mwanadamu kwenye mambo ya msingi hapaswi kabisa kuongozwa na hisia ikiwamo ushabiki. Anapaswa kfikiri.

Vinginevyo, ni ukweli, kuwa kijamii, mwanadamu anaweza kuwa kiumbe anayeishi kwenye mahusiano ya kirafiki na kiadui na wenzake. Na katika hilo la uadui, wanadamu, kama ilivyo kwa wanyama, wanaweza kushindania na hata kugombania vingi; iwe fedha, mashamba, wanawake na hata kivuli cha mti.

Ndio, unaweza kabisa kuwakuta wanadamu wawili wanagombania kivuli cha mti, kwamba nani mwenye haki ya kukaa kivulini. Na wanaweza kugombana mpaka akatokea mwendawazimu atakayekuja kuukata na huo mti wenyewe. Na wanadamu hao watabaki wakitazama juani.

Hoja yangu hapa, kuwa lililo la msingi ni kuwa wanadamu tunategemeana. Kwamba panapo kushindania jambo, mwanadamu, tofauti na mnyama, anapaswa kufikiri sana. Atangulize kwanza hekima na busara.

Na kwenye mgogoro wowote ule, mwanadamu ayape mazungumzo nafasi ya pekee katika kufikia muafaka, na si vurugu au mapigano. Kwenye mgogoro, na kwenye kuitafuta amani, panakosekana mazungumzo ina maana ya uwepo wa mazingira ya kuvunjika kwa amani. Hapa Serikali inapaswa iandae haraka mazingira ya mazungumzo katika kuitafuta suluhu.

Ndugu zangu,

Nilikuwa shuleni miaka ile ya 80 pale aliyekuwa Waziri Mkuu, Dr. Salim Ahmed Salim alipotembelea Mtwara na kukutana na umasikini uliomstusha sana. Kule Mtwara Dr. Salim alikutana na Watanzania waliovaa magunia na miguuni hawana hata kandambili. Na kwenye jua kali walijipanga kando ya barabara kumpokea. Kwenye jua kali walikusanyika kumsikiliza Waziri Mkuu wao.

Ni kule Mtwara inasemekana Dr. Salim, kwa mara ya kwanza, alipofikia maamuzi ya kutoa ruhusa ya mitumba kuingizwa nchini. Maana, kulikuwa na Watanzania wengine wengi nje ya Mtwara waliokuwa kwenye hali ya umasikini wa kufikia kuvaa nguo za viraka na kushindwa hata kuvaa viatu vya matairi ya magari.

Tunajifunza nini?

Kwamba ni kweli Mtwara na sehemu nyingine za nchi zimekuwa nyuma sana kimaendeleo. Na leo tunaposikia Mtwara kuna gesi, nakubaliana na Rais Jakaya Kikwete, kuwa gesi hiyo haiwezi kuwa ni ya WanaMtwara tu. Ni gesi ya Watanzania wote.

Ni vema na ni busara, na kwa kuwashirikisha wazee wa Mtwara, kuwa WanaMtwara wakasikilizwa. Kuna ya msingi ambayo WanaMtwara na Serikali wanaweza kukubaliana kwenye meza ya mazungumzo.

Hata kama tunakubaliana, kuwa rasilimali za nchi ziwasaidie pia watu wa eneo inakotoka rasilimali hiyo, lakini kamwe, tusikubaliane na hoja kuwa gesi iliyo Mtwara ni ya WanaMtwara. Kwamba dhahabu ya Geita ni ya watu wa Geita, twiga wa Ruaha ni wa Wahehe na kadhalika. Haya si mawazo mazuri kuyapandikiza katika nchi.

Ni mawazo ya hatari yanayoweza kupandikiza chuki, sit u miongoni mwa wananchi na Serikali, bali hata miongoni mwa wananchi wenyewe wa maeneo tofauti. Ni mawazo yenye kupandikiza pia fikra za kibaguzi.

Na tufikiri hili, je, kama gesi ile iliyopatikana kule Mtwara, Tanzania na Msumbiji nayo ingesema ni ya kwake, WanaMtwara wangesemaje kama watu wa mikoa mingine ya nchi hii nao wangesema wapelekwe wanajeshi wa Kimakonde, Kiyao na Kimakua tu wakambapane na majeshi ya Msumbiji kutetea ‘ Gesi ya Mtwara!’?

Naam, ya kule Mtwara isije ikawa yale yale ya kugombania kivuli.

Maggid Mjengwa,

Iringa,
0754 678 252
http://mjengwablog.co.tz

Brother Maggid,

Ktk watu ambao nawaheshimu ktk tasnia ya habari ni pamoja na wewe, mara nyingi nasoma makala zako kwenye magazeti na hata humu jamvini.Na mara nyingi mawazo yako au mitazamo yako huwa inafanana na yangu isipokuwa leo naomba uniwie radhi, nitakukosoa.Na natambua kuwa wewe ni muungwana, na muungwana yeyote anakubali kukosolewa.Nitakukosoa ktk kipengele kimoja tu lakini ni muhimu sana kwa kuwa ndiyo kina beba maudhui ya rai yako.Brother unaonekana hukufanya utafiti kujuwa wanamtwara madai yao ni nini hasa, umeisikiliza serikali na kutoa hukumu, hukutenda haki kwa upande wa pili yaani wanamtwara wanasema nini kuhusu suala hili.Ktk hili bro umeteleza.

Iko hivi; Nakuhakikishia kuwa Hakuna mwanamtwara hata mmoja anayesema kuwa hataki gesi iende kwa wengine eti waitumie wao peke yao LA HASHA brother Maggid.
Huu ni upotoshaji mkubwa unaofanywa na serikali na watu wa habari(sijuwi kwa sababu gani). Na wewe ni mwana habari.

WANA MTWARA WANATAKA NINI?

1.Wanataka gesi isisafirishwe kwa bomba, anayetaka kuitumia aje aichukuwe pale na iende sehemu yoyote tz na hata nchi za nje

2.Gesi isichukuliwe ghafi. Lile bomba linalojengwa bro ni la gesi ghafi na mikataba ilishafungwa siku nyingi kwa ajili ya kusafirisha ghafi

3.Power plant ijengwe mtwara kama ambavyo imepangwa kujengwa kinyerezi na kupeleka umeme sehemu zingine za tz.
Haya yakifanyika kutakuwa na movement nyingi ambazo zitaongeza shughuli za kiuchumi hatimae kusukuma maendeleo ya lindi na mtr ambako kuna umasikini wa kutisha kuliko sehemu nyingine yoyote ya tz.

Kwa kufanya hayo, kutakuwa na umeme wa uhakika ambao mtu yeyote atakuwa na imani ya kuweka kiwanda maeneo yale hatimaye kutoa ajira za kutosha na kuinua kipato cha wanamtwara na watz wengine.

Wanamtwara wanaona hii ni fursa pekee iliyobaki kwao ktk kujikomboa ktk lindi la umasikini walilonalo ambalo limetokana na kutengwa na serikali kwa muda mrefu na kuwafanya waishi kama wakimbizi kwenye nchi yao ilihali wao wanalipa kodi kama wengine huku wakipewa ahadi lukuki kila uchao.

Namalizia kwa kurudia kusema kuwa nakuheshimu sana brother, lakini ktk hili umefanyia kazi propaganda.

Narudia HAKUNA MWANA MTWARA YEYOTE ANAYEZUIA GESI ETI ISIWAFIKIE WATU WA MAENEO MENGINE, LA HASHA.

WANAHABARI WANAPOTOSHA UKWELI.

Nawasilisha.
 
Umepewa sh ngapi? Hujui unachokizungumzia. Usilolijua ni usiku wa giza. Usiwe mvivu wa kusoma na kujua habari za dunia inavyokwenda.nasikitika hujui hata hali ya gas inavyosafiridhwa. Yaelekea hata elimu ya sekondari huna. Maskini?
 
Back
Top Bottom