Mtwara Tunagombania Kivuli..

Mtwara Tunagombania Kivuli..

Tatizo la Mtwara ni ushirikishwaji hafifu na bora uongozi na si uongozi bora .

Kazi kubwa ya kiongozi ni kuwaelimisha anaowaongoza.Ikiwa kiongozi hanakosa sifa ya kuongoza kwa maana ya kuelimisha na kushrikisha anaowaongoza basi huyo hawezi kuitwa kiongozi ni lazima tumtafutie jina lingine linaloendana na matendo yake.

Kwa muda mrefu sasa labda miaka ishirini hizi Tanzania imekuwa dampo la viongozi wasiokuwa na sifa za uongozi,lakini wenye kulazimisha kuitwa viongozi hata kama ni kwa kutumia nguvu za vyombo vya dola kama jeshi la polisi na UWT.Tatizo la viongozi wasiokuwa na sifa za uongozi lipo hata katika vyama vya upinzani.Mfano unakuta kiongozi wa upinzani anajipachika sifa ya ugombea Urais wa kudumu hata kama sifa za kugombea nafasi hiyo zinazidi kuporomoka siku hadi siku.Utashangaa zaidi unakumbana na waziri mzima anafunga safari za mikoani badala ya kuondoa kero za wananchi anaziongeza.

Gesi ya Mtwara na Lindi ni mali ya waTanzania wote.Dhahabu ya Geita ni mali ya waTanzania wote,Tanzanite ya Mererani ni mali ya waTanzania wote,Mlima Kilimanjaro,Hifadhi za wanyama za Serengeti,Manyara,Mikumi,Saadani,Ngorongoro na nk ni mali za waTanzania wote bila kujali unaishi karibu na hifadhi hizo au mbali kiasi gani.Binafsi naishi Arusha lakini utashagaa tatizo la mpaka la ziwa Nyasa linanigusa sana kiasi ikitokea meza ya mazungumzo imeshindikana niko tayari kuitumikia nchi yangu hata ikibidi kwa kumwaga damu.

Tatizo linalotukabili waTanzania wengi sasa ni ukosefu wa uzalendo hasa upande wa uongozi.Wananchi wamekosa imani na uongozi/utawala kwasababu ya ubinafsi.Mikataba ya madini ni kielelezo namna watawala wetu walivyo walafi.Hata hili suala la gesi yamkini watawala wetu wameshaingia mikataba ya hovyo ndiyo maana tunaoana walivyotayari kutumia nguvu nyingi pasipo maelezo na pasipo ushirikiswaji.

Gesi ya Mtwara na Lindi ni mali ya waTanzania wote.Watawala tunahitaji mikataba iliyo ya uwazi na yenye kumnufaisha mTanzania.

Mungi ibariki Tanzania.
 
Lini watu wa Mtwara walisema gesi ni yao tuu? Upotoshaji huu ndio unaoamsha hasira kwao. Maana kwa makusudi mazima serikali (baadhi ya viongozi) wanapandikiza hilo kwa malengo yao na watu wa Mtwara wameshalielewa.
SULUHISHO; Ushauri wa kambi ya upinzani kuhusu kukaa pamoja na wadau wote na kujadili ndio suluhisho pekee.
 
Mimi labda sijaelewa kwani wanamtwara mamesema gesi ni yao....inasikitisha kuona mwandishi mkubwa kama wewe unapotosha...wanamtwara hawajasema gesi ni yao peke yao...ila wanachotaka kujua wao watanufaika vipi na gesi au watakua wanaona bomba la gesi tu linapita bila manufaa kwao..?Ikizingatiwa lile ni eneo mojawapolenye umaskini mkubwa tanzania....NARUDIA TENA TUACHE KUPOTOSHA WANAMTWARA HAWAJASEMA GESI IWE YAO PEKE YAO na kuileta DSM haimaanishi gesi ndo itakuwa ya watanzania wote...
 
Tunajifunza nini?

Kwamba ni kweli Mtwara na sehemu nyingine za nchi zimekuwa nyuma sana kimaendeleo. Na leo tunaposikia Mtwara kuna gesi, nakubaliana na Rais Jakaya Kikwete, kuwa gesi hiyo haiwezi kuwa ni ya WanaMtwara tu. Ni gesi ya Watanzania wote.

Ni vema na ni busara, na kwa kuwashirikisha wazee wa Mtwara, kuwa WanaMtwara wakasikilizwa. Kuna ya msingi ambayo WanaMtwara na Serikali wanaweza kukubaliana kwenye meza ya mazungumzo.

Hata kama tunakubaliana, kuwa rasilimali za nchi ziwasaidie pia watu wa eneo inakotoka rasilimali hiyo, lakini kamwe, tusikubaliane na hoja kuwa gesi iliyo Mtwara ni ya WanaMtwara. Kwamba dhahabu ya Geita ni ya watu wa Geita, twiga wa Ruaha ni wa Wahehe na kadhalika. Haya si mawazo mazuri kuyapandikiza katika nchi.

Maggid Mjengwa,

Iringa,
0754 678 252
http://mjengwablog.co.tz

'.........
Neno La Leo: Mtwara Tunagombania Kivuli....'

Kejeli kama hizo hapo kwenye kichwa cha habari, ndio zinazoamsha hasira za wana-Mtwara.
Juzi juzi waziri wa nishati aliwaita wana-Mtwara kuwa ni chura..!!
Kwa nini ?? kwa sababu wanapigania haki yao ya kufaidika na gesi inayochimbwa huko Mtwara..!!

Ulichoandika hapo kwenye blue, ni uwongo mkubwa wa shetani...
Wana-Mtwara hawajawahi hata siku moja kusema kuwa gesi ni yao peke yao..!!
Wanachotaka ni kufaidika na gesi hiyo inayochimbwa Mtwara.

Wewe mleta mada maggid unashiriki kwenye udhalimu wa serikali..!!
Sera ya CCM inasema kuwa raslimali za nchi ziongezewe thamani pale pale zinapozalishwa..!!
Sasa kwa nini gesi isiongezewe thamani kule Mtwara..??
Mleta mada upo hapo ..??

Mleta mada unaandika kama vile wewe ni msemaji wa serikali..!!
Unawaponda wana-Mtwara kuwa wanapigana na kivuli..!!

Kwako wewe mtu kudai haki ya maendeleo ni kupigana na kivuli..!!
Kwako wewe mleta mada, mikataba mibovu ya gesi ni bora kuliko haki ya wana-Mtwara..!!

Umelaaniwa wewe mleta mada maggid pamoja na wale wote wanaoendeleza udhalimu dhadi ya wana-Mtwara.
Mungu ibariki Tanzania.
 
Mu Israel,
Asante,
Lakini nawe unashiriki kupotosha kwa nia ovu kile nilichokiandika kwa nia njema. Inasikitisha.
Maggid

Embu tuzungumze ukweli gesi ni ya wana mtwara. Ni mali yao kwakuwa wamezaliwa na kukulia hapo kwenye ardhi ambayo ni yao lakini kwakuwa sisi ni jamhuri na ni nchi moja ni lazima mali za taifa zitumike katika maslahi ya pamoja. Kitu cha msingi hapa ni kwa serikali kuacha percent Fulani kwaajili ya maendeleo ya mtwara. Watu wa mtwara wamejifunza kutoka SHINYANGA, MWADUI na sehemu nyingine rasilimali zinapochimbwa. Kusema gesi si ya wana MTWARA ni uvivu wa kufikiri wana haki nayo ni yao. Ni lazima tufikie muafaka kwa mazungumzo kwakuwa tunajenga nchi moja.
 
Hivi gesi ya Songo Songo-Kilwa, mkoa wa Lindi, nani anaifaidi kama siyo ile Kampuni inayoiuzia Tanesco kwa dola za kimerikani badala ya Tshs wakati ni maliasili yetu!
 
Ndugu zangu,
Mwanafalsafa Jean- Paul Sartre anasema; " Hell is the other people" – Kwamba jehanam ni wale wengine, anataka pia tukubaliane, kuwa pepo yaweza kuwa ni wale wengine.

Na hakika, tofauti ya mwanadamu na mnyama iko kwenye kufiri. Mnyama anaongozwa na hisia, lakini mwanadamu anapaswa aongozwe na kufikiri. Ndio maana ng'ombe anaweza kumpanda mama yake. Ni hisia tu zitakazoongoza tendo lake.

Hivyo, mwanadamu kwenye mambo ya msingi hapaswi kabisa kuongozwa na hisia ikiwamo ushabiki. Anapaswa kfikiri.

Vinginevyo, ni ukweli, kuwa kijamii, mwanadamu anaweza kuwa kiumbe anayeishi kwenye mahusiano ya kirafiki na kiadui na wenzake. Na katika hilo la uadui, wanadamu, kama ilivyo kwa wanyama, wanaweza kushindania na hata kugombania vingi; iwe fedha, mashamba, wanawake na hata kivuli cha mti.

Ndio, unaweza kabisa kuwakuta wanadamu wawili wanagombania kivuli cha mti, kwamba nani mwenye haki ya kukaa kivulini. Na wanaweza kugombana mpaka akatokea mwendawazimu atakayekuja kuukata na huo mti wenyewe. Na wanadamu hao watabaki wakitazama juani.

Hoja yangu hapa, kuwa lililo la msingi ni kuwa wanadamu tunategemeana. Kwamba panapo kushindania jambo, mwanadamu, tofauti na mnyama, anapaswa kufikiri sana. Atangulize kwanza hekima na busara.

Na kwenye mgogoro wowote ule, mwanadamu ayape mazungumzo nafasi ya pekee katika kufikia muafaka, na si vurugu au mapigano. Kwenye mgogoro, na kwenye kuitafuta amani, panakosekana mazungumzo ina maana ya uwepo wa mazingira ya kuvunjika kwa amani. Hapa Serikali inapaswa iandae haraka mazingira ya mazungumzo katika kuitafuta suluhu.

Ndugu zangu,

Nilikuwa shuleni miaka ile ya 80 pale aliyekuwa Waziri Mkuu, Dr. Salim Ahmed Salim alipotembelea Mtwara na kukutana na umasikini uliomstusha sana. Kule Mtwara Dr. Salim alikutana na Watanzania waliovaa magunia na miguuni hawana hata kandambili. Na kwenye jua kali walijipanga kando ya barabara kumpokea. Kwenye jua kali walikusanyika kumsikiliza Waziri Mkuu wao.

Ni kule Mtwara inasemekana Dr. Salim, kwa mara ya kwanza, alipofikia maamuzi ya kutoa ruhusa ya mitumba kuingizwa nchini. Maana, kulikuwa na Watanzania wengine wengi nje ya Mtwara waliokuwa kwenye hali ya umasikini wa kufikia kuvaa nguo za viraka na kushindwa hata kuvaa viatu vya matairi ya magari.

Tunajifunza nini?

Kwamba ni kweli Mtwara na sehemu nyingine za nchi zimekuwa nyuma sana kimaendeleo. Na leo tunaposikia Mtwara kuna gesi, nakubaliana na Rais Jakaya Kikwete, kuwa gesi hiyo haiwezi kuwa ni ya WanaMtwara tu. Ni gesi ya Watanzania wote.

Ni vema na ni busara, na kwa kuwashirikisha wazee wa Mtwara, kuwa WanaMtwara wakasikilizwa. Kuna ya msingi ambayo WanaMtwara na Serikali wanaweza kukubaliana kwenye meza ya mazungumzo.

Hata kama tunakubaliana, kuwa rasilimali za nchi ziwasaidie pia watu wa eneo inakotoka rasilimali hiyo, lakini kamwe, tusikubaliane na hoja kuwa gesi iliyo Mtwara ni ya WanaMtwara. Kwamba dhahabu ya Geita ni ya watu wa Geita, twiga wa Ruaha ni wa Wahehe na kadhalika. Haya si mawazo mazuri kuyapandikiza katika nchi.

Ni mawazo ya hatari yanayoweza kupandikiza chuki, sit u miongoni mwa wananchi na Serikali, bali hata miongoni mwa wananchi wenyewe wa maeneo tofauti. Ni mawazo yenye kupandikiza pia fikra za kibaguzi.

Na tufikiri hili, je, kama gesi ile iliyopatikana kule Mtwara, Tanzania na Msumbiji nayo ingesema ni ya kwake, WanaMtwara wangesemaje kama watu wa mikoa mingine ya nchi hii nao wangesema wapelekwe wanajeshi wa Kimakonde, Kiyao na Kimakua tu wakambapane na majeshi ya Msumbiji kutetea ' Gesi ya Mtwara!'?

Naam, ya kule Mtwara isije ikawa yale yale ya kugombania kivuli.

Maggid Mjengwa,

Iringa,
0754 678 252
http://mjengwablog.co.tz

Kwa muda mrefu sasa, nimekuwa ni msomaji wa makala za Bwana Majjid Mjengwa hasa katika gazeti la raia mwema, lakini kadiri siku zinavyoenda nimejikuta naanza kuzipuuza na hata kufikia hatua naziruka tu na kusoma mambo mengine.

Ndugu Majjid ameamua kukengeuka na kuacha weledi na kukubali kutumika katika propaganda nyepesi nyepesi ambazo hazija tija.

Kinachoniuma zaidi ni upotoshaji wa makusudi unaofanywa na watu kama akina Majjid.

Mfano mmojawapo ni pale juu nilipopapaka rangi nyekundu,

Ni lini wanamtwara wamedai kuwa gesi iwe ni ya wanamtwara tu?, Kwa uelewa wa Majjid, kudai kuwa iwanufaishe wana mtwara ndio kumaanisha kuwa iwe ni ya wanamtwara tu?

Ina maana wanavyotaka kuisafirisha kupeleka Dar es salaama itakuwa ni ya wana Dar es salaama tu?.

Acha kutumika bwana Majjid.
 
. maggid, Who is next after David Mwangosi? RIP. maana swwaiba kamuhanda amesema kuna wandishi 7 watakufa Iringa, vipi umemuanda yupi baada ya Mwangosi?
Vipi leo Jogging?
Nilikuwa nimekasirishwa sana na upotoshaji wa huyu ndugu lakini baada ya kusoma komenti yako nimecheka sana.
Unaulizia hadi jogging?, nadhani ilikuwa ni siku ile ya vurugu za polisi kuwaonea machinga ndio aliamua kufanya jogging, teh teh teh!
 
Mjuni,
Asante,
Katika dunia hii hakuna nyeusi tu wala nyeupe tu. Kama unaukana ukweli huo basi ni vigumu pia kujadili zaidi hapa. Na katika dunia hii kuna wenye kusikia wanavyopenda kusikia, kuna wenye kusoma wanavyopenda kusoma, na kuna wenye kuona wanavyopenda kuona. Wanadamu hawa huwa hawana mengi mapya ya kujifunza zaidi ya yale wanayodhani wanayajua. Sasa hilo ni tatizo la wenye matatizo hayo. Natumaini wewe si mmojawapo.
Maggid,
Iringa.
Kwa muda mrefu sasa, nimekuwa ni msomaji wa makala za Bwana Majjid Mjengwa hasa katika gazeti la raia mwema, lakini kadiri siku zinavyoenda nimejikuta naanza kuzipuuza na hata kufikia hatua naziruka tu na kusoma mambo mengine.

Ndugu Majjid ameamua kukengeuka na kuacha weledi na kukubali kutumika katika propaganda nyepesi nyepesi ambazo hazija tija.

Kinachoniuma zaidi ni upotoshaji wa makusudi unaofanywa na watu kama akina Majjid.

Mfano mmojawapo ni pale juu nilipopapaka rangi nyekundu,

Ni lini wanamtwara wamedai kuwa gesi iwe ni ya wanamtwara tu?, Kwa uelewa wa Majjid, kudai kuwa iwanufaishe wana mtwara ndio kumaanisha kuwa iwe ni ya wanamtwara tu?

Ina maana wanavyotaka kuisafirisha kupeleka Dar es salaama itakuwa ni ya wana Dar es salaama tu?.

Acha kutumika bwana Majjid.
 
Na katika dunia hii kuna wenye kusikia wanavyopenda kusikia, kuna wenye kusoma wanavyopenda kusoma, na kuna wenye kuona wanavyopenda kuona. Wanadamu hawa huwa hawana mengi mapya ya kujifunza zaidi ya yale wanayodhani wanayajua. Sasa hilo ni tatizo la wenye matatizo hayo.

Wewe unapata ujumbe gani kutoka kwa Masoud?

kp09012013.jpg

kp10012013.jpg
 
Mjengwa umeeleweka vyema;
Hakika Serikali na viongozi wake hawafikiri; wanatumia spinal code kwenye maamuzi ya mambo magumu; nasisitiza kwamba gesi ya Mtwara ni ya watanzania wote; na kwakuwa Mtwara pia ni Tanzania kuna haja gani ya kuisafirisha hadi Dar? Tafakari.
Very logical. you are a Great Thinker (GT).
 
Kwamba ni kweli Mtwara na sehemu nyingine za nchi zimekuwa nyuma sana kimaendeleo. Na leo tunaposikia Mtwara kuna gesi, nakubaliana na Rais Jakaya Kikwete, kuwa gesi hiyo haiwezi kuwa ni ya WanaMtwara tu. Ni gesi ya Watanzania wote.

Hata wana Mtwara wamelikubali Hilo, Kila Mtanzania Mwenye akili Timamu analijua Hilo
Manufaa yataokanayo na Gesi ni Kwa Ajili ya Wa Tanzania wote,
Haina Haja ya Rais Kusema Ndo watu waelewe, Hilo liko Very Obviousy.

Na tufikiri hili, je, kama gesi ile iliyopatikana kule Mtwara, Tanzania na Msumbiji nayo ingesema ni ya kwake, WanaMtwara wangesemaje kama watu wa mikoa mingine ya nchi hii nao wangesema wapelekwe wanajeshi wa Kimakonde, Kiyao na Kimakua tu wakambapane na majeshi ya Msumbiji kutetea ‘ Gesi ya Mtwara!’?

Hakuna aliyesema Kuwa Gesi iliyoko Mtwara ni Ya wana Mtwara na Kwa ajili ya Wana Mtwara.
Hapa ndo Mnapokosea na Kupandisha Hasira Za Wa Tanzania wa Mtwara, mnawalisha Maneno ambayo hawajasema.
Wao kilio Chao ni Gesi iwe Processed Mtwara From the Beggining na Products zake zisambazwe Nchi Nzima.
Sisi hatutaki Kula Gesi, tuna Kula Products za Gesi na Wana Mtwara wameridhia Hilo.

How come Msumbiji waseme Gesi liyo Mtwara ni Yao???
Kwani Mtwara ni sehemu ya Msumbiji, acha Kujenga Hoja Dhaifu na Mfu kwa Masuala yenye Kuhitaji Kufikirisha Kichwa.

Naam, ya kule Mtwara isije ikawa yale yale ya kugombania kivuli.

Unaposema Kugombania Kivuli Unamaana gani with Refference to what is Happeing in Mtwara.

My Take.
Wewe ni Mmoja ya Wachumia Tumbo ambao Mko tayar kusema Kijani ni Nyekundu for the sake ya Mkono Kwenda Kinywani.
Mnajitahidi sana Kujaribu Kupotosha Madai ya Wana Mtwara.
Kwanini Serikali yako ya CCM haitaki Kusema Kutakuwa na Hasara Kiasi gani kama Hiyo Gesi ikiwa Processed Mtwara na Products zake kuwa Distributed
Al over the Country?????????????
Hii ndo Point ya Msingi ya Wana Mtwara.

Kwenye Masuala yenye Kuhitaji Kufikirisha Kichwa kama Haya Ni Bora ukawa unakaa Kimya
 
Lini watu wa Mtwara walisema gesi ni yao tuu? Upotoshaji huu ndio unaoamsha hasira kwao. Maana kwa makusudi mazima serikali (baadhi ya viongozi) wanapandikiza hilo kwa malengo yao na watu wa Mtwara wameshalielewa.
SULUHISHO; Ushauri wa kambi ya upinzani kuhusu kukaa pamoja na wadau wote na kujadili ndio suluhisho pekee.

unataka wakae pamoja mala ngapi pinda alienda kukaa nao wakamuona katuni sasa leo unatka washilikishwe nini.si busala kupotosha watu.
 
kama wananchi wa mtwara wangekuwa na nia ya dhati hayo mabomu waliyatoa wapi kama wanahitaji tu kushirikishwa,inakuwaje watu wamejiandaa kivita kabisa.
 
Back
Top Bottom