Mtwara: TAKUKURU yaomba Kibali kwa DDP kuwafikisha Mahakamani Wahasibu Watatu wa Mahakama

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,379
8,124
Kibali kinachosubiriwa kutoka kwa Mwendesha Mashtaka (DPP), kinahusu Kesi yenye Tuhuma za Ubadhirifu wa Tsh. Milioni 234 dhidi ya Watumishi wa Kada ya Uhasibu wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mtwara.

Naibu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa, Jumbe Makoba, amesema walipata taarifa za kuwepo kwa Ubadhirifu katika Mahakama Kuu juu ya Fedha za Mirathi zinazowahusu wanufaika ambao Ndugu zao walifariki.

Aidha, amesema wanaendelea kukamilisha uchunguzi mwingine wa Tsh. Milioni 460 zinazohusiana na tuhuma hizo na upelelezi ukikamilika watafikisha taarifa kwa DPP ili hatua za Kisheria zichukuliwe.
 
Mkuu kweli DDP atakubali kweli kutoa kibali?

Kwasababu DDP yupo ofisini ili kulinda wezi na kuwafutia kesi Mafisadi.
 
Back
Top Bottom