Kwanza niseme hivi, bila jitihada za dhati kuufanya ualimu kuwa taaluma waalimu wataebdelea kuwa wahanga na ngazi za watu kisiasa.
Pili, hilo ni kosa kubwa sana kiutenda ikiwa kweli huyo mkuu wa mkoa atashawishi kifanyike hicho alichokisema. Maana hawo walimu wakuu wapya hawatapenda kushushiwa heshima km wenzao na pia kuzikosa posho za madaraka. Hivyo itapelekea waalimu kuweka mikakati ya wao kufanya mitihani badala ya wanafunzi. Ndiyo maana kati ya maajabu ya ulimwengu japo hili halijaandikwa ni kuwa mtoto anafaulu kwenda form one hajui kuandika hata jina lake. (alikuwa mtoro na siku ya mtihani aliingia darasa lakini alifanyiwa mtihani)
Nashauri viongozi hasa Waziri wa elimu abadiri mbinu ya upimaji ktk elimu isiwe kwa kigezo cha mitihani ya siku tatu kwa mafunzo ya miaka saba.
Kigezo za ufaulu wa mtihani wa mwisho hasa std vii kitumike vizuri.
Kwani hakuna uwiano sawa wa mazingira ya kujifunzia mjini Vs vijijini, idadi ya walimu kati ya mkoa/wilaya/hata vijiji.
Waziri asikurupuke tuu na matamko na awaonye viongozi wasiokuwa kwenye kada ya elimu kuzumzia masuala ya Elimu.
Kidogo itasaidia, iwapo walimu wenyewe waeleze yapi yafanyike ili elimu ipande na si kufaulisha.
Natamani kila hatua ya ngazi ya elimu iweze kuwa na tija/matunda ya moja kwa moja hata ikiwa mhusika atakosa kwenda kwenye ngazi inayofuata.
Mkuu wa mkoa piga chini hawo walimu uone madhara yake.