Mtwara: Mkuu wa Mkoa atumbua walimu wakuu 63

Mtwara: Mkuu wa Mkoa atumbua walimu wakuu 63

Haya mambo raha sana, sasa yeye kasema hivyo waziri aseme nini yaani ni shidaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
 
Vitendea kazi,havipo vya kutosha,mwalimu mmoja wanafunz 70 mpaka 100,mishahara midogo,motisha hakuna,mtihan wa mchujo darasa la nne mmefuta,harafu mnataka wanafunzi wafaulu,bila kutatua matatizo ya walimu na kuboresha miundombinu,mtafukuza walimu wote,maana hakutakua na maajabu ya kufaulu.
 
mwamko wa elimu mikoa hiyo uko chini sana,pia walimu feki wengi wametupwa kufundisha huko. hapo unatarajia nini?
 
Hao wasubiri kusimamia uchaguzi maana hiyo kazi wanaiweza vizuri
 
Mkuu wa mkoa hana mamlaka ya kumfukuza kazi au kumshusha cheo mtumishi yeyote wa umma..!!

Hana mamlaka hayo, amekurupuka huyo mkuu wa mkoa, yafaa UTUMISHI impe ONYO KALI..!! Sbb hajui mipaka ya madaraka yake, hafai kuwa mkuu wa mkoa..
 
Mkuu wa mkoa wa Mtwara ameagiza kuvuliwa madaraka kwa waalimu wakuu 63 wa shule za msingi mkoani humo na baadhi ya Maafisa Elimu ambayo idadi yake haikufahamika mara moja, kutokana na mkoa kupata matokeo mabaya kwenye mithani wa darasa la 7 mwaka jana 2016.

View attachment 460029
Wabafunzi na wazazi wanafanywaje? Maana kila mmoja anamchango wake katika kushinda au kushindwa.
 
Mkuu wa mkoa mwenyewe anastahili kutumbuliwa kwa kosa hilo hilo la mkoa kuwa wa mwisho
 
Mkuu Wa mkoa Wa Mtwara ameagiza kushushwa vyeo walimu wakuu shule za MSINGI kutokana na Matokeo mabaya ya mitihani ya kuhitimu Elimu ya MSINGI mwaka Jana ambapo mkoa huo umeshika nafasi ya pili toka mwisho.

View attachment 460026

Akiongea kupitia taarifa ya habari ITV usiku Leo SAA mbili amesema anaagiza mamlaka zichukue hatua Mara moja na anasubiria kuona utekelezaji haraka.

Je hatua hizi zitasaidia kweli kupandisha ufaulu Wa wanafunzi na kuboresha kiwango cha elimu?
Amefanya utafiti na kugundua kuwa ukuu wa shule ndio chanzo cha kufeli?? Au ndio kundi la viongozi wa maamuzi bila tafiti?
 
Wakuu Wa wote wachinjwe kwani wao ni washiriki wakubwa kuuwa watoto wetu kielimu
Nadhani hata bangi unatumia wewe mkuu wa shule anahusikajen hadi kufikia mawazo kama yako?? Kama hujui jambo funga bakuli lako.matatizo ya elimu tanzania ni makubwa tofauti na fikra zakozako ndogo hizo
 
Mh! ila kuna wakuu wa shule wengine hovyo sana japo hiyo idadi ni kubwa sana, yawezekana wengine wameonewa. huwa wanalishana Ujinga kwenye vikao vyao vya TAHOSA.
TAHOSSA inahusika vipi hapa? Hao waliondolewa ni waalimu wakuu wa shule za msingi. TAHOSSA ni wakuu wa shule za sekondari.
 
Kama tatizo anafikiri ni wakuu wa shule,tuchukue shule mmoja tumpe yeye ukuu wa hiyo shule alafu tuone kama atafanya vizuri
 
Mkuu wa mkoa si mwajiri wa Mwalimu hana mamlaka ya kumfukuza Nazi Mtumishi/Mwalimu. Apache kicki
Angalia vizuri kiongozi, sio kumfukuza kazi bali ni kuvuliwa madaraka. Mkuu wa mkoa ametoa agizo, mamlaka husika yaani Mkurugenzi wa Halmashauri anatekeleza agizo.
 
Rais ni Mwalimu, Mke wa rais ni Mwalimu, Waziri Mkuu ni mwalimu lakini walimu ndio kada inayopata msoto wa kutisha zaidi katika awamu hii.
 
Bora kujiajiri kuliko kuajiliwa kuajiriwa ni kero unaishi kwa hofu yaani kesho yako ya kazi hunauhakika nayo kama ndio mi2 naacha kazi
 
Maamuzi ya kukurupuka athari yake ni kubwa sana. Lakini kama alifanya upembuzi yakinifu basi labda hilo litaleta tija.

Mwalimu Mkuu ndiye msimamizi wa shule, ni wajibu wake kusimamia taaluma na mambo mengine kwa kushirikiana na waalimu wake, wazazi wa wanafunzi, jamii bila kusahau wakuu wake waliomtuma hapo.

Kufeli kwa mwanafunzi kuna sababu nyingi, chache kati ya hizo ni.

Mazingira
Wazazi
Jamii
Mwalimu wake
Mwanafunzi mwenyewe.

Hivyo ukifanya utafiti kuhusiana na hilo suala ni lazima vitu hivyo vikuongoze hapo ndipo unaweza kuja na jibu zuri kwanini watoto wamefeli.
 
Back
Top Bottom