‘Mtwara kushika mkia siyo bahati mbaya’

juve pauly

JF-Expert Member
Jul 26, 2015
506
433
leo gazeti la mwananchi limeripot kuwa mkuu wa mkoa wa mtwara mama Halima Dendego amesema alitarajia mkoa huo kuwa wa mwisho kitaifa kwenye matokeo yaliyotangazwa juzi na baraza la mitihani taifa.

alisema
"nimekuja mtwara nimegundua mambo hayako sawa, nikajaribu kutafuta kiini, ndio nikabaini hakuna mwamko wa elimu, waalimu sio wabunifu. wanashindwa kuangalia mazingira yaliyopo na kufundisha kulingana nayo. utoro pia umekithiri" Amesema.

aidha mkuu huyo wa mkoa alieleza licha ya kutofurahishwa na matokeo hayo, alitarajia hali hiyo kutokana na suala la Elimu kutopewa kipaumbele mkoani MTWARA.


source MWANANCHI jumanne. 17/01/2017
 
Back
Top Bottom